Jinsi ya kupakua videos za YouTube | How to download YouTube videos

Google utapata maelekezo kuna application nyingi tu za kutumia aidha kwenye simu au kwenye computer
 
Tumia torch browser, kupitia hii unaweza kudownload kutoka kwenye source yoyote ile sio YouTube tu. Try it hutojutia
 
Namna ya "ku-download" video toka youtube.
Fungua video unayotaka kuipakua, nenda kwenye link ya video mf https://www.youtube.com/watch?.....replace hiyo sehemu ya red kwa kuandika ss halafu Enter.Ukishafanya hivyo itakuletea option ya kupakua nawe utafanya hivyo. Hakuna haja ya kuwa na Downloader.
 
1479400593404.png
 
Pakua videoder kutoka browser yoyote install kwenye simu yako,imeandikwa videorder beta,kwenye PC pakua torch browser install kwenye PC yako,utadownload chochote kutoka youtube
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Habari wakuu, nimeona niandike kifupi njia ambazo huwa nazitumia kupata video/Sauti(audio za youtube). Nitajaribu kuelezea njia mbalimbali hasa extensions, kutumia softwares au sites ambazo utaweka link kisha zenyewe zitakusaidia.

EXTENSIONS
Njia nayotumia muda mrefu na rahisi, hii ni kwa wanaotumia computers ambapo browser ya mozilla nadhani ndio yenye extension nyingi zaidi. Unachofanya ni kuiwekea extension browser yako unayotumia. Mfano ukifungua browser yako ya mozilla unaenda sehemu ya menu kisha palipoandikwa Adds On na kutafuta kati extension zifuatazo ambazi kwa maono yangu ndio bora.

Youtube.JPG

1.Download youtube video as MP4: Nzuri sana na haijawahi kunisumbua tatizo lake inashusha video yako kwa mfumo mmoja tu wa MP4, hivyo kama una matarajio zaidi ya MP4 inaweza isiwe nzuri kwako.

2. Youtube video and audio downloader: Nzuri pia na inashusha video na audio kwa mifumo mingi(Unaweza kupata video unayoangalia kama audio). Tatizo lake pamoja na kuweza kudownload sauti lakini huwezi kupata MP3 ambayo ndio rahisi kutumia na inakubalika sehemu nyingi.

3. Youtube MP3: Inakuja kusahihisha udhaifu wa extension ya pili hapo juu kwa kupata MP3 lakini haina option nyingine zaidi ya MP3.

4: Download helper: Hii ni nzuri zaidi, inakwenda mbali zaidi ya yotube, unaweza kupata video kutoka kwenye sites nyingi sana. Unaweza kuweka kuweka kwenye browsers za Mozilla na Chrome

NB: Unaweza kuziweka zote nne kwa pamoja na kuchagua ipi utumie kulingana na muktadha wa wakati huo.

SOFTWARES
1. IDM:
Baba lao, popote unapocheza video yenyewe inajitokeza(pop) na kama utapenda kuwa nayo video unayoangalia basi utapobofya na kuipata papo hapo. Hii zaidi ya kukuwezesha kupata kama video pia ni accelerator nzuri sana na kwangu ni nzuri zaidi nikipenda zaidi uwezo wake mzuri wa ku-pause na resume download yako pale internet inaposumbua, kuzima PC na kadhalika. Udhaifu wake inauzwa hivyo itabidi ununue ama uipate kupitia njia za panya(Torrents).

TOVUTI(SITES)
Kutumia tovuti: Unacopy link ya video na kuweka kwenye tovuti na yenyewe inakupa video yako. Site gani? Zipo nyingi sana, Just google upate site kulingana na unavyopenda

SIMU
TUBE MATE: Tube mate ni app ambayo unaweka kwenye simu yako na utaangalia video za youtube kupitia app hii ambapo itakupa uwezo wa kuzidownload endapo utazihitaji. App hii haipo play store ya google hivyo itabidi uiweke bila kupitia playstore kwa kuipata kwenye site ya tubemate. Ukishaidownload(APK) utaibofya ili uweze install(Baadhi ambazo haziwezi kuweka apps zisizotoka google play utaenda kwenye security setting za simu na kuruhusu apps zisizotoka google play kwa kutick sehemu palipoandikwa 'Unknown sources).

Asanteni.
 
Habari wanajamvi!

Naomba kuelekezwa jinsi ya kudownload video za kwenye youtube kwa kutumia opera.

Maana natumia simu aina ya Nokia E5!
 
Back
Top Bottom