Jinsi ya kudhibiti matumizi ya mtandao ya mtoto

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,852
2,000
Katika ulimwengu wa Teknolojia wa sasa watoto wanalazimika kuwa na vifaa kama simu, laptops nk ili kuwezesha mawasiliano ya mzazi na mtoto.

Kwa kiasi kikubwa wazazi wanadhana kwamba vifaa hivi vinaweza kumuharibu mtoto hivyo wengine huwanyima watoto vifaa hivyo ambapo wanakuwa wamewanyima haki ya kupata taarifa.

Mtoto kuwa na simu janja sio tatizo, tatizo ni namna ambavyo ataitumia. Na katika hilo kunahitaji muongozo wa mzazi. Lakini kwa sasa wazazi hawako muda wote na watoto ili kuwachunga katika matumizi yao.

Ili mzazi kuwa na uwezo wa kuchunga matumizi ya simu janja au laptop kwa mtoto atahitaji kuwa na vifaa vingine ambavyo inaweza kuwa ni Google Family Link For children and teen au hata baadhi ya antivirus ambazo zinatoa huduma ya Parental Control.

Huduma hizo zinaweza kumfanya mzazi aweze kujua na kuzuia anachofanya mtoto kwenye simu yake hata kama hayupo naye jirani. Mzazi anaweza akapanga muda wa mtoto wake kuwa mtandaoni, kuzuia baadhi ya Apps nk.

Vitu hivyo unaweza kufanya bila kuwa na mtoto jirani, mathalani mzazi uko nyumbani, mtoto yuko shuleni na ukaweza kuzuia vitu ambavyo anavifanya kwenye simu. Hapa utakuwa umemuachia mtoto haki ya mawasiliano lakini umedhibiti matumizi yake.


1612862123283.png

Baadhi ya apps ambazo unaweza kuzitumia kudhibiti matumizi ya simu kwa mtoto
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
26,004
2,000
Kwamba hao watoto wana maujanja zaidi ya Chief
Ni Tatizo la android mkuu si langu,

Mfano mtoto Ana click notification kwa ku hold notification husika inampeleka moja kwa moja kwenye properties za app then Ana force close, security ina pause for a moment anaingia app aliokatazwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom