Jinsi ya kudhibiti hasira kwenye mapenzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
1. Kama jambo limekuudhi kupita kiasi, badala ya kufoka, kupiga kelele hadi wakati mwingine majirani wanasikia, jaribu kutuliza kwanza akili yako kwa kujipa muda wa kuvuta pumzi ndipo useme unachotaka kusema.

2. Usithubutu kuacha hisia na hasira zako zikutawale kwani hizo ndio hukusababishia kufanya mambo ya ajabu kama vile kuvunja vitu, kutukana, kukejeli au kuamua tu kununa bila kutafuta suluhu ya tatizo.

3. Aidha ni vyema ukajipa muda na kutafakari kwani wakati mwingine huenda umekasirika kwa sababu ya kufikiria upande mmoja tu wa jambo lililokupata, yaani, sehemu iliyokukasirisha wewe.

4. Jitahidi pia kuelewa jinsi mwenza wako naye anavyohisi. Hata hivyo, washauri wa masuala ya saikolojia ya uhusiano wanadai kuwa endapo wenza wakiona ugomvi kati yao umekuwa mkubwa na hakuna maelewano, ni vyema mmoja wao akaondoka eneo husika ili kutoa muda kwa kila mmoja wao kutafakari juu ya kilichotokea.

5. Tiba njema inapotokea tatizo kama hilo ni kupeana na muda na baada ya kila mmoja kutuliza hasira na hisia zake kuhusu kilichotokea, mnaweza kuzungumzia tatizo kwa pamoja na kulitafutia ufumbuzi kwa utulivu bila kukwaruzana.
 
1. Kama jambo limekuudhi kupita kiasi, badala ya kufoka, kupiga kelele hadi wakati mwingine majirani wanasikia, kutuliza kwanza akili yako kwa kujipa muda wa kuvuta pumzi ndipo useme unachotaka kusema.

Back
Top Bottom