Jinsi ya kuchonga SMS kama ushahidi kwenye kesi mbali na kifaa anachosema Mabere Marando

Gaspery lasway Mkuu hii njia ndiyo inatumika sana hata kuibia watu kwa njia ya M Pesa na kuna watu wamelizwa sana town, watu wananunua line anabuni njia au kama anakufahamu anatengeneza line yako anakublock wewe halafu line yake inakuwa active yenye namba zako.
Sasa nadhani kwa suala ulilolieleza shida itakuwa location ya mtu kama ni mahakamani labda huyo mtu itabidi akufuate mahali ulipo kwa siku husika.. mf. hawezi kutumia namba yako yeye akiwa dar na aka act ni wewe ambae uko dodoma. They need to be extra smart.
 
Last edited by a moderator:
kwa tanzania makampuni ya simu yanatumika,utakuta unatumiwa sms na chama fulani unajiuliza nani kawapa namba yako?
 
hiyo sio isue kubwa sana kwa tech ya leo, ila ni ujinga tu wa magamba wakijua kitu wanakikurupukia wakizani kwamba wao ndo wajanja kumbe ndo mizuga. jaribu hii kama una simu zako wewe mwenye fata maelezo kweny page hii SMS Spoofing - SpoofCard. unapoingiza namba anza na +255
 
Walichofanya hawa magamba NCHEMBA bin LIWALO NA LIWE walitumia mfumo wa computer na divyo walivyofanya maana kuna program hizo nyingi sana hata kwenye IPHONE ipi unaweza kutuma SMS na ukaweka sender namba yoyote wewe upendayo hata kama ukitaka iwe ya Kamanda KOVA Inaweza tu.Kwa maelezo zaidi jinsi magamba wanavyotumia tembelea Spoof SMS Service. Send anonymous SMS from any number or name - SMSGang.com Utaona ujaja wao wote wanaotumia kudhalilisha watu.
 
Mnyika alituma msg za vitisho na matusi,huo ndio ukweli mchungu.lazima abinywe huko chini kwa aliyoyatenda ili akome.
 
Kitu rahisi sana ni kuangalia Message Center number ya hiyo sms......Kila mesage unayotumiwa ukiscorl hadi mwisho itakuonyesha tarehe iliyotumwa kwako na Message center number (Nokia Torch inaonyesha vizuri sana).......Hii utajua tu kama hiyo message imetumwa kweli kutokea hapa Nchini au ni ya magumashi maana kama ni kweli imepitiakwenye mitandao ya simu ya hapa nchini basi message center number lazima ianze na +2557xxxxxxx.
 
Nafikiri bado kuna namna ya kujua sms imeoriginate kwenye aina gani ya simu siyo tu kwenye namba fulani. Ukienda kwenye detail zaidi za ki uchunguzi utakuta msg inasema imetumwa kutoka NOKIA phone type fulani so bado kumbambkia mtu msg siyo issue provided uchunguzi wa kitaalamu ukifanyika, itajulikana kama kweli muhusika ana hiyo aina ya simu.
 
Kwa 'wenzetu' wenye akili zao na wanaojua wanachokifanya kuna kitu kinaitwa Customer Information Disclosure Policy - CIDP ambayo inaelekeza kuhusu usiri wa taarifa za wateja.

Sijui kanuni, sheria, na taratibu zetu zinasemaje kuhusu issue kama hii. Kutokana na sakata hili la Nchemba, ambalo kimsingi ni la hatari, ni muhimu mno ku-review sheria zetu ili kuhakikisha taarifa za wateja zinalindwa kwa kiwango cha juu.

Makampuni ya mawasiliano (simu, n.k.) wana wajibu wa kuhakikisha takwa hili linatimizwa na wateja wawe na haki ya fidia kubwa pale taarifa zao zinapovuja.

Binafsi huwa inaniudhi sana kupokea ujumbe wa ajabu ajabu kutoka namba za ajabu ajabu - mfano mzuri ni kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2010. Upuuzi huu ukomeshwe mara moja.
 
Nakumbuka kuna kesi mahakamani against mtu mmoja aliyejifanya anampigia mke wa mfanyabiashara fulani akipretend kuwa yeye ni mmewe tena kwa kutumia number ya mmewe huyo huyo kuwa anamtuma mtu aje kuchukua hela dukani maana kapatwa na matatizo.

Mkewe akashangaa kupata text toka kwa mme wake wakati wapo wote tena simu yake anayo mkononi japo inaonekana haipo hewani.
Wakatoa taarifa police, mwizi alipofika kuchukua pesa akatiwa mbaroni.

Alipohojiwa akawataja wafanyakazi wawili wa shirika la simu. Alikamatwa mfanyakazi mmoja mwingine akakimbia sijui kama alishakamatwa.
Simu zetu si salama tena.
 
Gaspery lasway kila line ina namba inayoitofautisha na line ingine, kama waki-swap system inajua kuwa kuna hicho kitu kimefanyika, rahisi sana kujua, sidhani kama kuna mpuuzi anaweza kufanya hivi, labda asiyejua kitu kuhusu taarifa gani zinabaki kwenye system unaposwap, tena ni kitu unakipata hata kwa customer care wala sio kwa system engineers :)

 
Last edited by a moderator:
Chief it is simple kupata data hasa kwa Magamba cos wapo wenye share kwenye hizo kampuni pamoja na positions zao....kwa wewe VI mimi na co VIP wao...inakuwa tabu

Mkuu wangu, pamoja na kwamba maelezo ya mtoa mada hayajitoshelezi; lakini ni simpo game tu hapo ambayo wala haina haja ya kupata data!!! Suala la ku-swap namba ya mtu ni simple kama kufumba na kufumbua....unaweza kuwatumiwa hata Freelancers....na kama utatumia Customer Care Executive ndo even more simple!!

So, ni kweli kabisa kwamba unaweza ku-swap namba ya Mnyika on the spot ile anayoimiliki yeye ikashindwa kufanya kazi na chip yako wewe yenye namba ya Mnyika ndo ikaanza kufanya kazi hapo hapo!! Baada ya hapo, wewe unaweza kuitumia ile sim card (ya mnyika) uliyonayo na kufanya chochote na kuonekana kitu hicho kimefanywa na Mnyika! Hilo, ni jambo jepesi kama kufumba na kufumbua!

Tatizo lililopo ni kwamba; as far as namba ya "mnyika" ilishakuwa Swaped; hapo ni kwamba ni lazima yeye apate chip nyingine na yenye serial number nyingine ili iwe renewed.....so, i don' think kama inawezekana kwamba hata baada ya hiyo namba kui-swap; tena unaweza kuifufua papo kwa papo!! So, kama kweli itathibitika watuhumiwa waliwahi ku-renew namba zao baada ya Nchemba kuwa alishatumiwa hizo meseji; then madai ya mtoa mada yanaweza kuleta sense kwa over 90%! Lakini kama haikuwahi kutokea jambo hilo....basi ni ngumu kuthibitisha kwamba namba zao zilikuwa swapped!

Hata hivyo, my concern ni kwamba iliwezekana vipi mtu mwenye akili zake timamu atume ujumbe wa vitisho kwa mbunge kwa kutumia namba yake ambayo inafahamika! Hapa ndipo ilipo shaka yangu.....!!!
 
sasa naanza kuamini kweli wabunge wa Chadema walimtumia Mwigulu kwa thread hii ya kutapatapa!
Mwigulu ni mtu mwenye hila na fitina za kijinga daima, nyie mnaemtetea mtakuja jilaumu pale hila zake za kishetani zitakapowekwa hadhari bila kificho. kumbukeni hakuna mhalifu anayedumu milele. Mbaya zaidi uhalifu anaoufanya Mwigulu ni kinyume na elimu yake.
 
hiyo sio isue kubwa sana kwa tech ya leo, ila ni ujinga tu wa magamba wakijua kitu wanakikurupukia wakizani kwamba wao ndo wajanja kumbe ndo mizuga. jaribu hii kama una simu zako wewe mwenye fata maelezo kweny page hii SMS Spoofing - SpoofCard. unapoingiza namba anza na +255
Yes.it works but how to remove the signature ya huo mtandao?
 
Back
Top Bottom