Jinsi ya kuchonga SMS kama ushahidi kwenye kesi mbali na kifaa anachosema Mabere Marando

The Don

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,499
1,163
Hii hufanywa na makampuni ya simu makao makuu kama ifuatavyo؛mf. Mnyika na nchemba
1.kufunga mawasiliano kwa mlengwa aliyedhamiriwa kupakaziwa kesi(network low au unavailable at all) line ya mnyika.
2.kuifunga line husika(block line)(mnyika)
3.kuchukua line mpya na kuipa access ya number ileile ya mlengwa(swap)
ikiwa na deteils za mnyika
4.kutuma sms(kwa ushahidi) au au kutoa vitisho kwenda kwa mlalamikaji(toka kwenye hii line ya mnyika asiyoijua kwenda kwa nchemba),hii huwa na details za mnyika mf.sms yenye tarehe,siku mwaka na muda,ushahidi tosha mahakamani.
5.kufunga hii line mpya(mnyika feki) iliyotumika baada ya kufanikisha na kuwa na uhakika kwa kilichofanyika,hapa mlengwa haelewi nini kinaendelea
6.kuirudisha line ya mlalamikiwa(mnyika) na kuipa full network(swap).
7.kesi kufunguliwa wakiwa na ushahidi tosha unaokutia hatiani.
Note;si wote wanaokwenda jela ni wahalifu wengine ni michezo michafu kama hii
 
Huu mchezo ni hatari na mara nyingi ni vigumu kufanyika kutokana na makampuni ya simu nchini kuwa wakali kwenye kutoa datta za wateja wao.. Juzi nilikuwa nafuatilia Print Out za Mwizi wangu mmoja hadi kupata ilinichukua muda mrefu sana pamoja na kuwa na kibali toka kwa DCI
 
Chief it is simple kupata data hasa kwa Magamba cos wapo wenye share kwenye hizo kampuni pamoja na positions zao....kwa wewe VI mimi na co VIP wao...inakuwa tabu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Makampuni ya simu huwa hayahusiki kabisa, na wala sms zenyewe huwa hazipitii kwenye mitandao yao. Ni mchezo fulani wa wajanja. Hakuna cha kifaa toka Israel wala nini.
 
Ni dhahiri makampuni ya simu nchini yana kesi ya kujibu (walau kwa wateja wao). Badala ya kula hela wanazopata, walitakiwa wawekeze kwenye huduma na kuondoa matatizo kama haya ambayo potentially yanahatarisha maisha ya wateja.

Kama number ya mteja inatumika bila yeye kujua na hivyo kumuingiza mteja huyo kwenye matata, kampuni husika ya simu lazima nayo iwajibike. Na hapa ndipo regulator na shareholders wanatakiwa wawahakikishie watanzania wanaotumia huduma za hii mitandao kwamba usalama upo. Ningeomba kujua kama number iliyotumika ni kampuni gani. Kuna haja ya kuanzia huko huko kwa main shareholder.
 
Mnyika ni PM please. Nadhani Mkoloni amekwambia kwamba nakutafuta.
 
Huu mchezo ni hatari na mara nyingi ni vigumu kufanyika kutokana na makampuni ya simu nchini kuwa wakali kwenye kutoa datta za wateja wao.. Juzi nilikuwa nafuatilia Print Out za Mwizi wangu mmoja hadi kupata ilinichukua muda mrefu sana pamoja na kuwa na kibali toka kwa DCI

HAPO kwenye red sio kweli

Push Mobile wana simu ya kila mtu ( unakumbuka 2010 watu tulikuwa tunapokea msg za vitisho nyingine inakuja imeandikwa IKULU,

sasa hivi msg inakuja imeandika TIBA CLINIC sijui hawa watu wanapataje number zetu
 
Hii kitu ni rahisi sana tu hata kwa wale wa miamvuli barabarani. Pia kuna vitu kama Bluetooth Hacker and so vinaweza kazi hii kirahisi.

Na kwa Tanzania yetu wao wao walioko kwenye maofisi ya mitandao ndio wanahusika sana tena wengine bure kwa urafiki.
 
Huu mchezo ni hatari na mara nyingi ni vigumu kufanyika kutokana na makampuni ya simu nchini kuwa wakali kwenye kutoa datta za wateja wao.. Juzi nilikuwa nafuatilia Print Out za Mwizi wangu mmoja hadi kupata ilinichukua muda mrefu sana pamoja na kuwa na kibali toka kwa DCI

mimi nilipata za demu wangu kwa elfu kumi tu, ndani ya nusu saa
 
Jamani msumbuke bule kwa sasa kuna makampuni yanatoa huduma ya ujumbe kupitia computer kwenda simu ya mkononi. Pale kuna options kuna sehemu ya utaandika ujumbe wako na sehemu ya namba yaani ujumbe unako kwenda, sehemu nyimgine ni sender.
Sasa hapa kwenye sender unaweza kuandika jina au namba, mfano ukiandika kwenye sender 1234567 itaonekana ujumbe umetoka kwenye Jambalaya hiyo.
 
Back
Top Bottom