Namna ya kuchangia faini ya Tsh. Milioni 350 waliyohukumiwa kulipa Viongozi wa CHADEMA

kingunge wa jf

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
452
416
Naomba viongozi wa CHADEMA Taifa watoe Account Namba tusaidiane kuchangia hii Hukumu. Asante

=======

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo jioni makamu mwenyekiti wa Chadema (Zanzibar), Said Issa Mohammed amesema hukumu hiyo ni dhuluma ya demokrasia na wapo tayari kukata rufaa na watanunua haki yao.

"Mtakumbuka tangu 2018 kulikuwa na kesi ya kubambikia viongozi wetu. Baada ya ushahidi tulikwenda mahakamani tukijua tutashinda," amesema Mohammed.

Amesema Chadema wataendelea na mapambano na kwamba hadi leo saa 6 usiku wanataka wawe wamepata fedha hizo.

"Hukumu imetolewa saa 10 wakijua benki zote zimefungwa viongozi wetu wabaki. Ikifika kesho twende tukawatoe viongozi wetu. Tunao mawakili tutakata rufaa. Tutahakikisha tunafikia lengo saa 6 usiku," amesema.

Amewataka wanachama wao kutumia akaunti ya CRDB yenye jina la Chadema M4C 01J1080100600 na namba za mkurugenzi wa fedha, Rodrick Lutembeka 0754275531 na 0655 275 531 kufanikisha mchango huo.

Akihamasisha michango hiyo, Mwenyekiti wa Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu amesema hukumu hiyo ilikuwa ni jaribio la kidemokrasia ambalo wamelishinda.

"Nasimama hapa kwa sababu mwenyekiti wetu hatalala kwake, viongozi wetu hawatalala kwao kwa kupigania haki.

Tutasonga mbele, kufikia kesho saa 2 asubuhi tuwe tumefanikiwa," amesema Nyalandu.

Amewaomba Watanzania wa vyama vyote na wapenda demokrasia kuchangia faini hiyo.

"Wale ambao wamefurahi kwa kuumizwa kwa kina Mbowe na watakwenda kunywa soda na bia wajue tutashinda."

Naibu Katibu mkuu (Bara), Benson Kigaila amesema michango hiyo ina lengo la kuonyesha Serikali mshikamano wao.

"Tuwaonyeshe Serikali waliowaweka viongozi wetu ndani. Tuwaonyeshe, tukalipe hiyo hela, tuchange kila hela. Tunao wanachama milioni saba Kaskazini, Kusini, Kati na Magharibi na Mashariki tuchange. Kesho kabla ya misa ya kwanza wawe wametoka," amesema Kigaila.

Chanzo:
Mwananchi

IMG-20200311-WA0000.jpg

1583907141973.png

Pia, soma:

Breaking News: - Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini Milioni 350 au kwenda jela miezi 5 kwa kila kosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu,
Uongozi Wa chadema wekeni akaunti hadharani ya Benki ili tuchange tuwape hao waliotuonea kwa kumuua akwilina.

Msiogope wote mliobambikiwa kesi kwenye hili tumemshinda shetani, wao wamepanga hukumu na kuona kama wametukomoa kumbe LA hasha, chadema ni mpango Wa MUNGU na Kato ndio chama kitakachoongoza serikali ya Tanzania baada ya October 2020.

Sisi wapenzi na wanachama Wa chadema tutatoa shilingi mia tano(500) nchi nzima kuwachangia ili shetani apate anachokitaka lkn na kwa sababu tunaitoa pesa kwa uchungu huku akiwa ametuyumbisha kiuchumi ili kutukomoa nawahakikishia kabla ya uchaguzi 2020 huyu shetani atakuwa yuko hoi taabani, hoi pesa yetu ndio inakwenda kummaliza, hawezi kuua na kuumiza na bado atutake kuchukua ugali wetu ambao tumeutolea jasho ili yeye ajifaidishe harafu maombi yetu yamuache salama haiwezekani, ajiandae shetani kututoka hatumtaki kama ambavyo MUNGU alimkataa na kumtupa nasi tutamzika.

Wekeni akaunti tuwachangie pesa hill limepita tugange yajayo.

Swelana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba viongozi wa CHADEMA TAIFA watoe account namba tusaidiane kuchangia hii Hukumu. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja yako mkuu watupe hata Tigo pesa, Airtel money na M-pesa, mimi najisemea niko tayari kutoa mchango wangu,

Wakati wao wana polisi, jeshi, mahakama, magereza... Sisi chadema tuna watu fanyeni utaratibu wa namba tutachangia. Tena leo
 
85 Reactions
Reply
Back
Top Bottom