SoC01 Jinsi ya kuboresha Sekta ya Kilimo kupitia Mapinduzi ya Viwanda

Stories of Change - 2021 Competition

Robertson1

New Member
Sep 13, 2021
2
2
Mwishoni mwa miaka 1700's kuelekea mwanzoni mwa 1800 huko Uingereza kulikuwa na mapinduzi makubwa sana ya kilimo. Mapinduzi haya yalichochea kuongezeka kwa idadi ya watu kutokana na wingi wa chakula, hali ambayo ilipelekea watu kuzaliana kwa wingi sana. Mapinduzi haya yalipelekea kutokea kwa mapinduzi makubwa sana yaliyobadili maisha ya Waingereza na Ulaya kiujumla nayo ni mapinduzi ya viwanda.

Licha ya kilimo kuwa msingi wa mapinduzi haya, Kuna tofauti kubwa Sana kati ya kilimo kabla ya mapinduzi ya viwanda na kile kilimo baada ya mapinduzi ya viwanda.

Matumizi ya teknolojia yalichagiza uzalishaji wa viwango vya juu Sana tofauti na mwanzo kabla ya viwanda, pia kukawa na ongezeko la faida kwa wakulima kutokana na kupunguza kutegemea binadamu kama wafanya kazi na kutumia mashine kama mbadala mfano majenereta kwenye umwagiliaji, matrekta ambayo yalisaidia kupanua kiwango cha kilimo.

Tupo kwenye karne ya 21 karne mbili baada ya mapinduzi ya viwanda huko Ulaya, cha kushangaza na kusikitisha bado tuna tumia mbinu za kizamani katika kilimo chetu.

Huwezi amini asilimia 70 huenda na zaidi ya watanzania ni wakulima wanaolima kienyeji bila ya kutumia njia za kisasa na kisayansi ili kuboresha uzalishaji katika kilimo chao.

Tunahitaji kubadilika na kujifunza kupitia mapinduzi ya viwanda ya Ulaya, serikali inahitajika kusimamia suala hili ili kuokoa jamii ya wakulima kutoka kwenye kilimo kisicho na tija.

Moja ya faida ya kutumia kilimo cha kisasa ni kupata uzalishaji mkubwa kwenye eneo dogo.

Pili kutanua wigo kwa wakulima kutoka kilimo cha Kati Ghafi kilimo kikubwa kama watatumia mashine kama trekta kulimia.

Tatu ongezeko la uzalishaji litapunguza au kuondoa kabisa tatizo sugu la njaa kwenye jamii zetu.

Lakini pia maendeleo ya kilimo yatachagiza maendeleo ya sekta zingine kama biashara, uchumi, miundominu ya uchukuzi na usafirishaji kutokana na mazao yanahitajika Sana kwenye masoko mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kumekuwa na sera mbalimbali katika Serikali za awamu tofauti katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Kilimo kwanza chini ya Rais mstaafu Dr Jakaya Mrisho Kikwete, sera ambayo ilitaka watanzania kufanya kilimo chenye tija japo haikufanikiwa kwa kiasi kile kwani bado hatujafikia matamanio hayo

Awamu ya tano ikaja na sera ya viwanda, ikifufua baadhi ya viwanda vilivyokuepo ili kuwezesha uchakataji wa mazao yatokanayo na kilimo, hivyo kuongeza soko na ajira kwa watanzania.

Jitihada hizi zinalenga kuboresha uzalishaji kwenye kilimo lakini bado tunahitaji Serikali kupitia wizara husika(kilimo) kuja na sera mbadala kama plani ya muda mfupi na mrefu ili kuboresha sekta hii muhimu kabisa kwenye uchumi na maisha ya watanzania kiujumla.

Kwa mtazamo wangu binafsi serikali kupitia wizara ya Kilimo na ufugaji inahitaji kuja na sera zifuatazo kwaajili ya kuboreha nyanja hii muhimu na uti wa mgongo katika uchumi wa nchi yetu na maisha ya wananchi kiujumla.

Kwanza, kuongeza idadi ya wataalamu kwenye sekta hii. Ukitathmini idadi ya wahitimu wa elimu ya juu nchini namba ya wahitimu kwenye sekta ya kilimo ni chache na haikidhi mahitaji ukilinganisha na sekta nyingine kama Elimu na Afya. Hi inaathiri maendeleo ya kilimo nchini kwa sababu wananchi wanakosa Elimu na mawazo chanya jinsi ya kufanya kilimo chenye tija kama kutakua na ongezeko la wataalamu kwenye sekta hii kutakua na urahisi wa mabadiliko kwani watasaidia kuwlimisha jamii juu ya ulimaji wa kitaalamu.

Mbili, kuwe na sera elekezi kwa kila familia kuwa angalau na heka mbili za kulimwa kitaalamu. Serikali kupitia wizara ya kilimo ije na sera ya kutumia wataalamu waliopo kuhakikisha kwamba kila mkulima anafanya kilimo cha kisasa japo kwa heka mbili, hii itawafanya watu kuelewa na kuona faida ya kilimo cha kisasa tofauti na kile cha holela. Jinsi watu wataona faida yake ndivyo mabadiliko yatashika hatamu mwisho wa siku mabadiliko ya kweli yatatimia.

Tatu, serikali ifadhili mbegu na pembejeo za kisasa kwa wakulima wa hali ya chini. Baadhi ya wananchi wanatamani kufanya kilimo cha kisasa, bahati mbaya wannashindwa kutokana na uchumi mbaya kwenye familia zao.

Serikali inahitaji kuwafadhili watu wa hali hii kwa kuwasaidia pembejeo kama mbegu za kisasa, madawa ya kilimo na mbolea za kisasa ili kuwawezesha kuona faida ya kilimo cha kisasa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom