Jinsi watu wanavyolizwa na Tigo Niwezeshe

Mjasiriamali1

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
891
237
Watanzania wengi wanaishi maisha ya kukopakopa. Huko kwenye kukopa ndiko watu wanalizwa vibaya sana. kama watanzania wengine nikaingia account ya tigo nikakopa airtime. Sasa nikasema ngoja ni clear deni lote leo. Haya ndo madudu niliyoyagundua; imebidi niandike ili watu tuwe macho kabla ya uamuzi wa kukopa, nikapiga *149*49# nikacheki Salio la deni airtime nikakuta 3225.

Baada ya kuweka airtime yote 3225 ili wakate, walichofanya wakakata 1400, kisha nikaambiwa salio lilibaki ni 2400 nikashtuka kidogo.

1. Deni ni 3225
2. Kichokatwa ni 1400
3. Deni lilobaki ni 2400
4. Ukichukua 1400 + 2400 = 3800
5. Tofauti ya 3800 na 3225 ni 575
6. 575 ndio tigo walitaka kuiba
7. Unaweza kuona ndogo but chukua
8. Wateja mil 6 kwa mfano mara 575
9. Utapata 3,450,000,000
10. Kwa huo uwizi mdogo tuu, sasa swali je serikali inapata kodi? kwa mfano huo iyo ni karibia 3.5bil.

Kilichotokea sasa baada ya kuwapigilia simu kuwabana, yule mhudumu anasema ndugu siyo 2400 ni 1825, nikamwambia unachoniambia na message mliyonitumia ni tofauti, nikamwambia nime screen short message zote. Na haya maongezi nimeyarekodi, unasemaje? Akasema mteja iyo 1825 itakatwa baada ya masaa 24 akaruka lile swala anang'ang'ania kama una shida ingine nikusaidie. Nikakata simu.

KABLA YA KUKOPA JAMANI TUWE WANGALIFU, NI BORA KUNUNUA VOCHA MOJAKWAMOJA. HII MIKOPO YA SIMU HIZI IMEKUJA KUWALIZA WATANZANIA
 
Kumbe ndio maana wanapenda kuwakopesha watu bila wao kuhitaji kukopa, jana nimekaa nashangaa meseji imeingia kwamba nimekopeshwa kifurushi cha dk za mitandao yote, nikabaki najiuliza nimekopa saa ngapi,kumbe wanaiba hivi, laini yao imebaki ya kupokelea simu na sms napo sio sana, ninampango kuachana nao, wizi wa vifurushi vya intaneti ndio ulionifanya kuwaweka pembeni
 
Kwa ujumla mikopo huwa sio mizuri, kokote mikopo huwa sio mizuri hata humu benki tunakokopaga huwa wanatunyonya sana.

Mikopo haifai ila ni basi tu. Sijui ni nani alaumiwe. UMASIKINI? UJINGA??
 
Watanzania muwe mnasoma kwanza vigezo na masharti kabla kabla ya yote na muelewe.
 
Back
Top Bottom