Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
Unajua ukiwa juu unaweza kuviona vitu vyote vilivyoko chini kuwa ni vidogo; Na kwa kadiri unavyoenda juu zaidi ndivyo vitu hivyo vinaonekana kuwa vidogo zaidi. Hata hivyo ukweli wa mambo ni kuwa siyo udogo wa vitu bali ni umbali uliopo kati ya wewe na vitu hivyo ndivyo vinavyokufanya uvione kuwa vidogo. Sasa ukividharau na kuvitendea kama vile ni vidogo utakapoanguka na kujikuta umeangukia majabari kosa halitakuwa kwa majabari hayo!
Kwa muda mrefu sasa watawala wetu yaonekana wanazidi kwenda mbali na wananchi na kwa kadiri wanavyokwenda mbali ndivyo wanazidi kutuona wadogo na kutudharau. Na bila ya shaka kwa kadiri wanapigiwa makofi, wanavimulimuli kwenye misafara yao na saluti zikiangushwa kila wapitapo basi ndivyo na wenyewe wanavyojiona wako juu zaidi.
Katika hiki ambacho naweza kukiita kuwa ni kiinimacho cha madaraka (the illusion of power) basi wale walio katika madaraka hujiona kuwa siyo tu wanastahili bali ni haki yao kuwa hapo walipo. Kwa hawa wazo la "cheo ni dhamana" halipo tena na kwao cheo kinageuka kuwa "haki" yao. Kwa watu hawa ambao mawazo yao yamepotoka "kutumikia wananchi" kwao kunamaanisha "kujitumikia mwenye nchi".
Hivyo inapotokea wananchi wanapoanza kuwahoji na kuwauliza; au pale wanapotakiwa kutoa maelezo majibu yao hao watawala yanakuwa ni ya dharau (contempt) na ya kibabe. Majibu yao yanaenda kwenye wigo wa kejeli kana kwamba wao miungu wasiokufa (immortals) hawatakiwi kuulizwa maswali na binadamu wafao (mortals).
Sakata zima la ufisadi uliokubuhu ambao umepotezea nchi yetu zaidi ya Shilingi trilioni moja kwa muda mrefu ni ushahidi wa jinsi gani watawala wetu wameamua kujikweza na sisi wengine kututweza. Hadi leo hii wizi uliotokea Benki Kuu ungetosha siyo tu kumfukuzisha mtu mmoja kazi bali kuifumua benki nzima hiyo na kuinda upya.
Wakati wanajeshi wetu walipoasi mwaka 1964 na kusababisha hali ya wasiwasi nchini hadi kutaka Waingereza waingilie kati kuzima maasi hayo, uzito wake ulionekana. Ndugu zangu hoja yangu ni kuwa Benki Kuu ilikuwa imeasi Taifa na uongozi wake kufanya financial mutiny na kusababisha Taifa letu kuwa na wasiwasi. Kitendo cha kuacha watu wachache waiteke Benki Kuu na kuchota fedha za maskini wa Tanzania kwa vile tu wanaweza ni sababu tosha ya kuomba hata wageni waje waisimamie Benki Hii na hatimaye kuirudisha kwenye mikono ya Watanzania.
Leo hii waliopewa jukumu la kuchunguzu suala la EPA wanatetemeka mbele ya wezi wa mali zetu na kama wanaogwaya mbele ya mizimu wanawabembeleza watuachilie. NI kama vile tumewekewa nira kwenye shingo zetu na tunatumikishwa pasipo ridhaa yetu! Saa imefika ya kuvunja nira hiyo na kugoma kuwalimia mashamba yao na kuwaparuia nafaka zao!
Tutaweza vipi kuongozwa na watu ambao wanatuzuga? Ni kweli sanduku la kura litawaamulia lakini hatutafika huko hadi tukatae katika fikra na mawazo yetu kuwa na viongozi kama hawa licha ya uzuri wa nyimbo zao, na umahiri wa rangi za nguo zao! Lazima tuwakatae katika fikra zetu kuwa wameshindwa kuliongoza Taifa letu na kimsingi wanajiongoza wao wenyewe kufikia mafanikio ya watoto na wana familia zao!
Leo hii baada ya kuuliza sana Mkapa anaenda kulia na yeye ni Bangusilo na ya kuwa ameonewa na kusingiziwa hivi wanatuchukuliaje sisi? Binafsi sitaki kusikia tena maneno yao hasa ya kizugaji hadi pale kwenye suala la Ballali kwanza watakapotoa majibu ya maswali nitakayowavurumishia kesho!
Sitaki tena kuzugwa, sitaki kufanywa duni, sitaki kuonwa mdogo, sitaki tena kuburuzwa kama debe liburuzwazo na gari mkweche! Sitaki tena kuambiwa "Serikali imesema" halafu iwe mwisho. Nataka serikali ikisema iseme kitu ambacho kinaeleweka, chenye ukweli, ukweli mtupu, na ukweli wote! Sitaki tena kusikia kuwa kuna mtu anaoenewa.
Wito wangu kwa watawala wetu!! Sitisheni mazungumzo na mafisadi, ichukueni nchi yetu kwa nguvu toka mikononi mwao, na vunjeni majadiliano yenu na wezi!! Imetosha kuwabembeleza, imetosha kukaa nao na kuwaomba waturidishie mali zetu! Wakati umefika kama kuwaachia hizo fedha zetu tuwaachie lakini tunataka waiachilie nchi yetu ili na sisi hatimaye tupate nafasi ya kuijenga nchi yetu sisi wenyewe!!
Mkataba na kuzimu lazima ukome, na majadiliano na mapepo yasitishwe!! Tunataka uhuru wetu, uhuru wa kufikiri, uhuru wa kutenda, uhuru wa kupata habari za kweli, uhuru wa kuwapinga usiku na mchana, uhuru wa kuamua na kwenda!! Tunataka uhuru wetu wa kuwa na Taifa la kisasa tukinyang'anya ukiritimba wa madaraka yao na kuwapora ubwanyenye wa uhodhi wa mamlaka yao.
Kama wanatuona sisi ni duni na wadogo kwa vile wao wako mbali... ngoja basi watuone kwa kadiri tunavyowasogelea karibu! Watakimbia~~!