Jinsi wanaume wa kisasa wanavyomezwa na matakwa ya wanawake

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,650
Katika lugha ya kiingereza kuna maneno mawili muhimu sana: NICE na GOOD. Katika suala la mahusiano tunapata maneno nice guy na good guy. Twende kwenye mada.

Zamani ambayo ndiyo asili haswa, mwanamume alijifunza ama alifundishwa kuwa good guy, yaani ni mwanamume anayejua majukumu yake, aliweza kusimama kutetea familia yake dhidi ya mtu yeyote, mipaka ya mwanamke kwake wala hakuruhusu mwanamke kumpanda kichwani. Huyu ndiye alichukuliwa kuwa mwanamume halisi. Akiwa na mji wake jamii yote inajua kwenye mji ule pana mwanamume. Si mtu wa kulia lia, ni solutiton oriented, hahitaji semina za kila wiki kuweza kuelewa jinsi ya kukabili changamoto za maisha. Habari za mwanamume suruari hazikjwepo kwa sababu wanaume wote walikuwa wanaume!! Huyu ndiye GOOD GUY!!

Vijana wa kileo, modernists, new agers, wanafundishwa kuwa nice guys, waonekane wako poa kwa mambebez na watetezi wa haki za wanawake, wenye kutafuta usawa kati ya mwanamke na mwanamume. Wanaume wa namna hii wamepoteza uasilia wao na wamegeuka kama misukule, wakitafuta sifa kwa wanawake. Wakati mwingine hata ukweli ukiwa mbele ya macho yao hujifanya kutokuuona ili waonekane "nice guys." Ndio asili ya wanaume suruali, neno jipya ambalo limekuja baada ya wanaume kujikana asili yao kutaka kujilinganisha na wanawake!! Ukweli mchungu mno huu!! Unabisha? Pita mtaani uone vijana wanavyojipodoa kama dada zao, wanavyoshusha sauti zao wanapoongea na wanawake, yaani ukisikiliza maongezi utadhani wote ni wanawake!! Hakuna kibesi.

Good guys walikuwa wazuri kwa kusimamia majukumu yao, kusimamia uhalisia na pia walikiwa ni viongozi wa familia. Nasema walikuwa ni viongozi kwa sababu walikwenda wa uasili wao. Wanawake waliwaheshimu na kuijua mipaka yao vema, familia zilikuwa imara na zenye malezi bora. Watoto wa kiume walikuwa katika malezi bora na watoto wa kike hali kadhalika, kila mmoja akifurahia nafasi yake. Hakukuwa na manung'uniko wala masikitiko kwa sababu familia ilijiona bora na imara. Hakuna aliyejihisi kunyanyaswa mpaka pale wanawake walipofundishwa kwamba mwanamume kuwa juu ya mwanamke ni manyanyaso, mateso uvunjifu wa haki za mwanamke, ndipo walipofumbua macho na kuona kumbe wanaweza kuwa sawa na wanaume!!

Enter the nice guy!! Hawa jamaa wao mtazamo wao ni kusifiwa na wanawake. Na baada ya wanawake kugundua uwepo wa spicies hii ya wanaume, hakulaza damu. Mwanamke ni mjanja kiasili, mara moja alibadili matakwa ya mahusiano. Ndipo zikazaliwa lists ndeeefu za mahitajio, mimi mpenzi wangu awe hivi, au awe vile. Mfano awe mcheshi, awe na dimpoz, awe na pesa nyingi, awe mwenye sura nzuri ya kuvutia n.k. Mwanamume wa aina hii akiingia kwenye ndoa atatumikia matakwa ya mke na sio matakwa ya uhalisia.

Mke akikasirika atahangaika siku nzima kujaribu kumbembeleza, kama ndiye aliyekosea (mke) akamwonyesha makosa yake (maana wanaume hawa huwa hawakemei makosa, hummwonyesha tu mke), mke akanuna (ni kawaida yao zama hizi), basi jamaa atakwenda kumnunulia vijizawadi ili asinune tena. Mr Nice guy!!!! Yaani yeye ndio anaomba radhi kwa kugundua kosa la mke au mpenzi! Watu hawa hawa familia zao huwa ni liberal, yaani hazina mipaka. Watoto wana mitazamo huru, hakuna mwanamke wala mwanaume.

Mwanamke mara zote ndio anaongoza njia. Hebu watazame kuku wa kisasa, hybrid, huwa yamezubaa full time!! Hata mtoto wa miaka miwili anamkamata tu, kucha zake zipo kwa sababu ni kiungo cha kuku, hana jinsi ya kuzitoa, hawezi kumparua anauejaribu kumchezea!! Ndivyo walivyo wanaume hawa, yaani maisha yao ni kama kuku wa kienyeji, ni wanaume kwa sababu wamezaliwa hivyo. Tumetengeneza neutral gender, kilaatini inaitwa neuter. Tofauti ni kwamba wanawake wamehama kwenye asili yao na kupandisha viwango, huku wanaume wakishusha viwango vya uanaume wao kuwafuata!! Ni heri basi wanawake wangepandisha viwango vyao, wakahama kwenye asili yao na kujilinganisha na wanaume, huku mwanamume akibaki pale alipo, yaani akaendelea kuwa mwanamume!

Unawatambuaje? Wakati wa mahusiano ya kawaida nje ya ndoa na kwenye ndoa wanaume hawa wanatumia muda mwingi kuwafurahisha wapenzi wao. Wao wamejikinai na hivyo wameuza uanamme wao. Furaha ya wapenzi wao ndio furaha yao, mpenzi akinuna tu, siku imeharibiki. Wanawake wenye wapenzi walio na tabia hizi hutamba hata mbele za rafiki zao na mama zao, wakiwananga wanaume hawa. Zamani zile yaliibuka maneno kama mume bwege, bushoke n.k. Mwanamke akigundua tu udhaifu katika wanaume hawa, humburuza kama smart tv mbele ya rimoti. Siki zote mume hatakuwa na amani kwa hofu ya kumuudhi mamsapu. Huku ni kujitwisha jukumu ambalo hata Adamu lilimshinda, ka Eva kaliona Adamu hana mistari ya kuvutia, kakaenda kupiga stori na snake. You know what were the results!!

Hata leo mahusiano mengi yameingia kweenye mkondo huu, wanaume wanajiita vidume kwenye keyboard tu. Utawala umekuwa wa mwanamke, watoto wa kike wanalelewa kwenye malalamiko, wanafundishwa kumlalamikia mwanamume ili asithubutu kusikaka kwenye nafasi yake. Mfano wanafundishwa kuna mfumo dume, usikubali kunyanyaswa na mwanamume, wewe na mwanamume mko sawa n.k. Mabinti wanakuwa na negative thinking dhidi ya wanaume, ndio hao wanaokuja na viji-list vireefu vya aina ya mwanamume wamtakaye!! Vitoto vya kiume navyo vinakuzwa kujiona havina tofauti na mabinti zaidi ya kuheshimu periods zao!! Yaani kilichopo ni wanaume kujisikia kama mabinti, na si vinginevyo. Mwanamume ameikana asili yake na kujivika asili ya mwanamke, ndio dunia ya leo.

JESUS? This was a real man! Kubali kataa, Yesu alikuwa mwanamume kwelikweli. Yeye alikuwa mtu wa kusimamia asili yake, tazama jinsi alivyokuwa akiwanyookea wale waliomuuliza maswali ya majaribu! Hakuwa mtu wa kujipendekeza, alisimamia kweli tupu. Alipokuta mijitu inapiga hela hekaluni aliibua bonge ala vurugu, jeshi la mtu mmoja!! Masoja walipojipendekeza eti wafanye nini aliwachana live, hata maTRA akawaambia msichukie mlungula. Wanawake waliokutana naye aliwapa makavu, wewe huna mume ila ni nyumba ndogo, tena una mijemba mitano. This was a man. Hakujipendekeza kwa wanawake wala wanaume, He was real.

Wanaume tunakwama wapi? Tumesalimu amri kwa tamaa ya mwanamke? Tamaa ya mwanamke tangu Adamu na Hawa ni kumtawala mwanamume, ila Mungu aliona udhaifu wao wakiwa juu, akawaweka chini ya mwanamume, halafu wanaume wa kisasa wakampinga Mungu na kurudisha utawala kwa mwanamke, na wao kujifanya ni kama wanawake!! Matokeo yake? You know the answer. Kama hujui sikiliza wanawake live!!!

Have a blessed sunday.
 
It all starts with spouse selection.

A man has to defend his position no matter what, ujue ni kwa nini unaoa na ni nani anafaa kuwa mke.

Wanawake mara zote mpaka milele watatamani kupata utawala juu ya mwanamme, utawala ni raha usiskie kabisa. Mwanamme halisi anatakiwa (Pasi na chembe ya shaka) ajue kwamba nafasi ya uongozi ni yake yeye and there should not be any type of discussion over that.

Kwa hiyo, young fellas kwa ustawi na usalama wa maisha yenu hakikisheni mnaoa wanawake ambao wanastahili kuolewa, mwanamke ambae without doubt and with full submission kwa mdomo na matendo yake (kipindi cha uchumba) atakubali wewe ndio mwanamme na wewe ndio final sayer (of course by considering her ADVICE as well). Mwanamke abaki na nafasi yake ya ushauri na "A REAL MAN" atafuata ushauri mwema tu wa mwanamke wake.

By the way, naelekea mwaka wa tano sasa ndoani. Ukinibishia usisite pia kuniambia umeoa/umeolewa?? For how long now?? Have a blessed time.
 
Fact brother umesema wanaume tumepoteza uhalisia wetu
Kuna wengine waandaa matamasha kwa ajili ya kuwapa wanawake jeuri about Life all men are equal
Ile reality ya ndoa imepotea now devorce kawaida tena mwanamke ndo anakuwa priority kuomba talaka
Kuna ndoa na ndoano
 
Back
Top Bottom