Menejimenti SCI yatuhumiwa
na Mwandishi Wetu
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya SCI Tanzania Limited wameutuhumu uongozi wa kampuni yao kwa kukiuka taratibu za ajira na za uhamiaji.
Wakiongea juzi katika ofisi za gazeti hili, walisema wamefikia hatua ya kutoa malalamiko yao hadharani baada ya viongozi wao kuanza kuwafukuza kazi bila kuwalipa stahili zao na kuajiri raia wa kigeni kinyume cha taratibu.
Wafanyakazi hao ambao waliomba majina yasitajwe gazetini kwa kuhofia usalama wa ajira zao, walisema kumekuwa na mkakati wa siri wa kunyakua ajira za wazawa na kuwapa wageni.
Walisema, licha ya kuajiri wageni, taratibu za ajira zimekuwa hazifuatwi na baadhi ya maofisa wa Uhamiaji wamekuwa wakifika katika ofisi hizo na kufanya mazungumzo ya siri na mkurugenzi wao waliyemtaja kwa jina la Ravishankar Rajamani kisha wanaondoka.
Tumekwishafikisha malalamiko yetu Uhamiaji kuwa katika kampuni hii kuna wageni ambao hata hawana ujuzi wala uzoefu wa kazi, lakini wamepewa kazi zisizo za kitaalamu huku wakiwa hawana hata vibali vya kufanya kazi nchini. Maofisa Uhamiaji wanakuja, wanaongea na bosi wanaondoka kimya kimya, alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Rajamani alisema suala hilo amekwishazungumza na maofisa wa Uhamiaji na kulimaliza. Ramajani alisema, Uhamiaji wanazo taarifa kuwa ana wafanyakazi ambao hawajapata vibali, lakini utaratibu wa kupatiwa unaendelea na kwamba anayo ruhusa kutoka kwa maofisa hao ya kuendelea kuwatumia wakati taratibu za kuwapatia vibali vya kufanya kazi nchini zikiendelea. Jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Uhamiaji kuzungumzia suala hilo juzi na jana hazikufanikiwa kwa maelezo yaliyotolewa na mmoja wa wasaidizi wake aliyekataa kutaja jina lake, kwamba ana kazi nyingi za nje wiki hii.