Dua
JF-Expert Member
- Nov 14, 2006
- 3,236
- 667
Katika kipindi cha maswali na majibu ya Bunge suala la kuwepo kwa wageni wanaofanya kazi nchini na hasa katika sekta ya utalii ni la kila mwaka.
Na swali hilo limekuwa linaelekezwa katika sekta ya Utalii na yenyewe imekuwa inatoka na jibu linalofanana na hivyo kuashiria kutokuwepo kwa utekelezaji wa kweli wa yale yanayosemwa.
Jibu limekuwa kila mara kuwa; hivi sasa kuna mkakati wa kufundisha na kuendeleza watu -vijana wetu kwa kiwango cha kimataifa, kuwapeleka nje ya nchi, kufungua vyuo vya utalii.....bla blah blah blah..
Hadi kesho ukitembelea hoteli nyingi nchini bado zina mameneja Wazungu, ok siyo lazima Wazungu kwa maana hiyo lakini raia kutoka Afrika Kusini, Kenya na nchi nyingine pamoja na kwamba tulipata Uhuru wetu mwaka 1961.
Bodi ya Utalii Tanzania imeanzishwa mwaka 1962 , mwaka mmoja baada ya kupata Uhuru wetu lakini bado imeshindwa kuibuka na vipaji vya Kibongo vya kuwapokea Watalii na kuwakirimia kwa kutumia Wabongo pekee yake?
Hii yote ni pamoja na kuwa na vivutio kibao vya utalii na kutembelewa na idadi kubwa ya watalii, lakini bado tunahitaji mameneja, maafisa na wakurugenzi kuja kutupiga jeki ya namna ya kuwahudumia.
Hakuna mikakati iliyowahi kutolewa bungeni na kutolewa takwimu juu ya jinsi Wizara ya Utalii inavyokabilia kiukweli na suala la kupunguza idadi ya wageni walioajiriwa katika sekta hiyo, ila ni maneno tu kila mwaka yasiyotekelezwa.
Chanzo: DarHotwire
Hivi kweli tumeshindwa nini kutafuta suluhu ya hili swala? Kwa nini waziri anayeshughulikia haya mambo hawajibishwi ili ajira ziwepo kwa WTZ.