Papa Mobimba
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 1,153
- 1,359
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikisoma kitabu kinaitwa The Slaughter: Mass Killings, Organ Harvesting, and China's Secret Solution to Its Dissident Problem. Kitabu hiki kimeandikwa na bwana Ethan Gutmann huyu ni mwandishi wa habari za uchunguzi. Kitabu hiki alikitoa mwaka mmoja baada ya ripoti nyingine iliyochapishwa na David Mantis pamoja na David Kilgour.
Mahitaji ya viungo vya binadamu nchini China yako juu sana kulinganisha na nchi nyingine pengine hii inatokana na taifa hilo kuwa na idadi kubwa ya watu. Licha ya kwamba mahitaji ya kupata viungo ni makubwa sana lakini muda wa kusubiri kupata kiungo ni mfupi kulinganisha na nchi nyingine. Kwa mfano nchini Marekani utalazamika kusubiri kupata kiungo kwa muda wa siku 1865 (miaka sita), nchini Uingereza ni siku 1095 lakini China ni siku 15 tu.
Je viungo hivyo vinatoka wapi
Wote watatu wanakubaliana kuwa idadi kubwa ya viungo vya binadamu inapatikana kwa njia isiyo kuwa halali. Viungo vingi vinavyuna kwa wafungwa waliohukumiwa kifo kutokana na makosa makubwa hasa yako uhaini, madawa ya kulevya, ujambazi.
Wachunguzi hawa wanaeleza kuwa muda mfupi kabla mtu hajapelekwa kunyongwa huchomwa sindano ya kuzuia damu kuganda. Timu ya Madaktari inakuwa iko tayari. Mara nyingi hawa ni Madaktari wenye uzoefu mkubwa pamoja na spidi ya hali ya juu.
"Baada ya mtu kupigwa risasi, mwili huchukuliwa haraka haraka na kupelekwa katika magari maalumu ambako upasuaji wa kuvuna viungo hufanyika", taarifa zinasema. Ili kuhakikisha viungo haviharibiki madaktari hutumia dakika 20 mpaka 30 kuondoa viungo vyote wanavyohitaji.
Tuhuma kama hizo zimetolewa katika nchi ya India. Ambako huaminika mania ya watu husafirishwa na kuuwa kwa ajili ya viungo vyao. Shirika la Afya duniani linapiga marufuku uvunaji wa viungo usiozingatia haki za binadamu.
Katika nchi nyingi viungo vya binadamu ambavyo hupandikizwa ni pamoja na figo, moyo, maini, ngozi ya jicho, uboho wa kwenye mifupa, mapafu na kadhalika.
Miaka michache iliyopita Tanzania imeanza kutoa huduma za upandikizaji figo. Ni muhimu kuweka sheria mahususi zinakazosimamia masuala ya upatikanaji wa viungo pamoja na matumizi yake.