Jinsi Wabunge walivyohongwa ili wambane Waziri Maige | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Wabunge walivyohongwa ili wambane Waziri Maige

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwitongo, Apr 23, 2012.

 1. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  chanzo: gazeti la MTANZANIA


  Mfanyabiashara awanasa wabunge

  *Awaandalia semina, awapa posho ya kujikimu
  *Awandaa wapinge ugawaji vitalu vya uwindaji
  *Matokeo ya kazi kuanza kusikika bungeni leo


  Na Mwandishi Wetu

  Mfanyabiashara ambaye pia ni mwanasheria maarufuku kutoka Arusha anayejihusisha na biashara ya uwindaji wa kitalii, ameandaa semina nono kwa wabunge wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.

  Matokeo ya semina hiyo yanatarajiwa kuanza kusikika bungeni leo kwani kuna kundi la wabunge walioandaliwa kuhakikisha wanatetea ugawaji upya wa vitalu vya uwindaji wa kitalii. Kama ilivyo mijadala mingine, wananchi watakuwa na fursa ya kuwasikia wabunge hao wakitetea wazungu wapewe vitalu zaidi.

  Mfanyabiashara huyo mwenye ukwasi kutoka kaskazini mwa nchi, aliandaa semina hiyo Jumatatu wiki hii katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma, akilenga kuwandaa wabunge hao ili wafanikishe mpango wake ambao mara zote umelemea kuwabeba wazungu kwenye tasnia ya uwindaji wa kitalii.

  Taarifa za kufanyika kwa semina hiyo zilitawaliwa na usiri wa hali ya juu. Zilisambazwa kwa wajumbe na mmoja wa wajumbe kwa njia ya mdomo na ujumbe mfupi wa maandishi wa simu, tofauti na semina zote zenye nia njema ambazo hutangazwa hadharani.

  Semina ilianza saa saba mchana katika ukumbi huo na kumalizika saa 10 jioni. Baada ya hapo, wajumbe hao walipewa posho ambayo mmoja wa wabunge ameeleza bayana kuwa ilikuwa "nono mno".

  Katika kuthibitisha usiri wa semina hiyo, mwandaaji wa mada hakuweka jina lake wala la taasisi anayoiwakilisha kwenye mada aliyoiandaa kwa maandishi. MTANZANIA ina nakala hiyo na nyingine ya Ripoti ya Uwindaji alizowapa wabunge hao.

  Wabunge hao waliitwa kwa ajili ya kuwekwa sawa na mfanyabiashara huyo ambaye ni miongoni mwa wanasheria wanaojihusisha sana na masuala ya uwindaji wa kitalii, akiwa amejiegemeza zaidi kwa raia wa kigeni.

  Mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo amesema kwamba semina hiyo iliandaliwa kama sehemu ya kuwaandaa wabunge ili wahakikishe kuwa wanatumia ushawishi wao wa kuzungumza bungeni ili kulishawishi Bunge liiamuru Serikali irejee ugawaji vitalu vya uwindaji.

  Habari za uhakika zinaonyesha kuwa Kamati Ndogo ya Bunge iliyoundwa kuchunguza usafirishaji wanyamapori leo inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake bungeni.

  Kuna habari kwamba kwenye uchunguzi huo haikubaini moja kwa moja kama kweli twiga wawili, na wanyama wengine walisafirishwa kinyemela.

  Hata hivyo, kwenye suala la ugawaji vitalu kunaonekanakuwa ndiko Kamati hiyo imeegemea zaidi kwa kutoa mapendekezo yanayohamasisha ugawaji vitalu ufanywe upya, huku ikielezwa kuwa kuna idadi ya kampuni za kizalendo zilizopewa vitalu bila kuwa na uwezo.

  Tangu mwaka jana, MTANZANIA imekuwa ikieleza kuwa baadhi ya mawakala wa wazungu waliokosa vitalu, wanawatumia Watanzania kuhakikisha wanawatubuni wabunge ili wakubaliane na mpango wa kugawa upya vitalu vya uwindaji wa kitalii.

  Taarifa ya kuwatisha Watanzania

  Kwenye mada iliyowasilishwa katika hoteli ya St. Gasper, mtoa mada ambaye ni mwanasheria wa kampuni zaidi ya nne za uwindaji, mmiliki wa kampuni moja na mmoja wa wanahisa katika kampuni nyingine mbili, anawaeleza wabunge hao kuwa ugawaji vitalu uliofanywa unahatarisha rasilimali ya wanyamapori.

  Licha ya kukiri kwenye mada yake kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee duniani yenye wanyamapori wasiokuwa na mfano, anasema ugawaji uliofanywa utawafanya wawindaji matajiri kutokuja nchini.

  Anapinga ugawaji vitalu kwa namna ulivyofanywa kwa kusema, "Ugawaji vitalu kwa ajili ya uwindaji wa kitalii kwa makampuni mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2013-2018 umeongeza tishio la wanyama wetu na viumbe mbalimbali kuongeza kasi ya kumalizika."

  Anatoa sababu kadhaa za kuwapo kwa hatari hiyo kuwa ni kuongezeka kwa idadi ya vitalu vya uwindaji, na ugawaji vitalu kutozingatia sheria ya uhifadhi wa wanyamapori na ikolojia ya eneo husika.

  Anatoa mfano wa ugawaji vitalu vilivyopo Ziwa Natron kuwa umeenda kinyume cha kifungu 16 (4 na 5) ambacho kinasema Waziri hatagawa eneo kabla ya kushirikisha Serikali za Vijiji na kutangaza maeneo hayo kwenye Gazeti la Serikali. Eneo jingine analolalamikia ni la Pori la Akiba la Ugala.

  Hata hivyo, imebainika kuwa juhudi za mfanyabiashara huyo ni kuhakikisha kuwa baadhi ya maeneo aliyowahakikishia wadau wake (Wazungu) kuwa wangeyapata, yametolewa kwa kampuni nyingine. Miongoni mwa maeneo aliyoapa kuyarejesha kwa udi na uvumba, ni ya Maswa ambayo kuna ahadi ya kutoa kiasi chochote cha fedha ili kuyapata kutokana na kuwa na wanyama wengi, kwa muda mrefu na wanaopenda na wawindaji wengi.

  Mara zote Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kwamba ugawaji vitalu katika maeneo hayo ulilenga kuongeza mapato ya Serikali na pia kuzifanya kampuni nyingine ziweze kupata wanyamapori ambao hawapatikani maeneo mengine.

  Safari ya kufanikisha matakwa ya wazungu

  Katika kuweka mambo sawa, mmoja wa wajumbe wenye ushawishi mkubwa kwenye Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, alisafiri kwenda Afrika Kusini ambako pamoja na mambo mengine yaliyompeleka, aliweza kuonana na baadhi ya mawakala wa Wazungu wanaotaka ugawaji vitalu ufanywe upya.

  "Alikwenda Novemba 26 hadi Desemba 7, 2010. Aliwekwa sawa na wanaotaka ugawaji urejewe upya, akawaahidi kuwasaidia kadri atakavyoweza. Akawahakikishia kuwa Spika ni ‘mwelewa', hivyo wasiwe na wasiwasi," kimesema chanzo chetu.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM).

  Ingawa suala la vitalu liliingizwa kwenye Kamati Ndogo inayoongozwa na Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah (CCM), habari za uhakika zinaonyesha kuwa hakuna malalamiko rasmi yaliyowasilishwa kwenye Kamati ‘mama' kama alivyonukuliwa na Lembeli.

  "Kwenye vitalu, Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira itueleze imekutana na wanachama au chombo gani cha wawindaji?

  "Kinachofanywa na Kamati ya Bunge ni kuingilia utendaji kazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Sheria imeainisha wazi kuwa suala la ugawaji vitalu linafanywa na Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu, Waziri mwenye dhamana na Mahakama.

  "Mtiririko uko hivi… Kamati ya Ushauri inapitia maombi yote, inatoa alama kwa kila kampuni na kushauri kampuni gani ipate kitalu gani kati ya vile ilivyoomba. Baada ya hapo inawasilisha kwa Waziri mwenye dhamana ambaye naye anatoa uamuzi. Kama yupo asiyeridhishwa anamwandikia Waziri, na Waziri anaiandikia Kamati ya Ushauri ili kujibu hoja za mlalamikaji. Ushauri wa Kamati unarejeshwa kwa Waziri anayepaswa kutoa uamuzi wa mwisho. Kama mlalamikaji hakuridhika anaruhusiwa kisheria kwenda Mahakama Kuu.

  "Utaona kuwa kama kulikuwa na malalamiko, bado mchakato upo kwenye Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu na kwa Waziri. Sasa kwa mazingira hayo unaweza kujiuliza, imekuwaje Kamati ya Lembeli iingilie suala ambalo bado lipo kwenye mpangilio wa kupata utatuzi kwa mujibu wa sheria zilizopitishwa na Bunge?

  "Kama kweli wapo waliolalamika, wameshindwa nini kwenda kwa Waziri au mahakamani? Hapo mwenye akili hawezi kushindwa kutambua kuwa Kamati ya Bunge inatumiwa na waliokosa vitalu.

  "Ndiyo maana kwenye mpango wao wanasema ile asilimia 15 kwa kampuni za kigeni iongezwe hadi kufikia asilimia 30. Hiyo maana yake ni kwamba ikitekelezwa wageni wengi watapata vitalu," kimesema chanzo chetu.

  Kampuni zilizopata vitalu 2013-2018

  Kampuni kadhaa zilipeleka maombi ya kupatiwa vitalu. Kati ya kampuni hizo ni 60 pekee zilizokidhi viwango kwa mujibu wa Sheria Namba 5 ya Wanyamapori ya mwaka 2009 na Kanuni zake za Mwaka 2010.

  Hapa chini kuna orodha ya kampuni hizo. Kampuni tisa kati yake ni za kigeni. Zinamilikiwa kwa asilimia 100 na raia wa kigeni. Kampuni zilizobaki ama zinamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100 au kwa ubia na wageni. Nyingi zina ubia na wageni. Kampuni hizo ni:

  1. Marera Lodges and Tours Ltd
  (Tanzania)
  2. Bunda Safaris Ltd (Tanzania)
  3. Siafu Safaris Ltd (Tanzania)
  4. Snfnf Hunting Safaris Ltd (Tanzania)
  5. Traditional African Safaris Ltd (Tanzania)
  6. Fereck Safaris Limited (Tanzania)
  7. Miombo Safaris Ltd (Tanzania)
  8. Tanzania Bundu Safaris (Tanzania)
  9. Royal Frontiers Ltd (Tanzania)
  10. Game Frontiers Ltd (Tanzania)
  11. Northern Hunting Ent. Ltd (Tanzania)
  12. Western Frontiers Ltd (Tanzania)
  13. Mkwawa Hunting Safaris Ltd (Tanzania)
  14. Ebn Hunting Safaris Ltd (Tanzania)
  15. Tanza Guides Ltd (Tanzania)
  16. African Buffalo Safari Trackers Ltd (Tanzania)
  17. Tanzania Wildlife Co Ltd (Tanzania)
  18. Old Nyika Safaris Ltd (Tanzania)
  19. Muhesi Safaris Ltd (Tanzania)
  20. Z. H. Poppe Ltd (Tanzania)
  21. Kilimanjaro Game Trail (Tanzania)
  22. Michael Matheankis Safaris (Tanzania)
  23. Safari Royal Holding (Tanzania)
  24. Tandala Hunting Safaris (Tanzania)
  25. Go Wildhunting (Tanzania)
  26. Bushman Hunting Safaris (Tanzania)
  27. Melami Hunting Safaris (Tanzania)
  28. Mwatisi Safaris (Tanzania)
  29. Tanganyika Game Fishing (Tanzania)
  30. Maasailand Hunting Co (Tanzania)
  31. Safari Club Ltd (Tanzania)
  32. Kiboko Hunting Safaris (Tanzania)
  33. Pori Tracker Safaris of Africa (Tanzania
  34. Green Miles Ltd (Tanzania)
  35. Rungwa Game Safaris (Tanzania)
  36. East Africa Trophy Hunters (Tanzania)
  37. Kilombero North Safaris (Tanzania)
  38. Wembere Hunting Safaris (Tanzania)
  39 Coastal Sable Safaris (Tanzania)
  40. Eshkesh Safaris (Tanzania)
  41. Palahala Safaris & Horizon (Tanzania)
  42. Maully Tours & Safaris (Tanzania)
  43. Giant Hunting Club Ltd (Tanzania)
  44. Mwanauta Co Ltd (Tanzania)
  45. Wild Foot Prints Ltd (Tanzania)
  46. Malagarasi Hunting Safaris Ltd (Tanzania)
  47. African Trophy Hunting Ltd (Tanzania)
  48. Hsksk Safaris Co Ltd (Tanzania)
  49. Green Leaf Ltd (Tanzania)
  50. Out of Africa Safaris (Tanzania)
  51. Said Kawawa Hunting Safaris (Tanzania)
  52. Tanganyika Wildlife Safaris Co Ltd (kigeni)
  53. Barlette Safaris Corp Ltd (kigeni)
  54. Gerald Pasanisi Safaris Corp (kigeni)
  55. Game Tracker Safaris (kigeni)
  56. Wengert Windrose (kigeni)
  57. Grumeti Reserves (kigeni)
  58. Robin Hurt Safaris (kigeni)
  59. Otterlo Business Corp (kigeni)
  60. Luke Samara Safaris (kigeni)

  Kuna habari kwamba mkubwa umesukwa na kundi la wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuhakikisha kuwa mchakato mzima wa ugawaji vitalu vya uwindaji wa kitalii unaanza upya.
  Baada ya kuona mbinu zote za kuwalegeza viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii zimeshindikana, sasa mpango huo umepenyezwa kwa wabunge.  ..tamati…..
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  huu ndio uandishi wa ovyo uliotawaliwa na rushwa, mwandishi ni mwehu na amehongwa na vigogo wa wizara kulichafua bunge, Waziri maige amekula rushwa katika kugawa vitalu, amekuwa na ukwasi wa kutisha ikiwa ni pamoja na ununuzi wa nyumba dar es salaam yenye thamani ya zaidi ya bilioni moja na milioni mia mbili, ni wizi wa kutisha huu.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,788
  Trophy Points: 280
  kamrani
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hata wewe umeandika kwa jazba bure... Mbona usifikirie kuwa huenda mwandishi ni Maige mwenyewe?
   
 5. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Penye udhia penyeza rupia nani msemakweli na nani muongo wote wako mstari mmoja! Tusipoacha kufikiri kwa matumbo tutafanyishwa vitu vya ajabu sana hapa duniani ambako tunapita.
   
 6. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  jukwaa linaangalia upande mmoja. Maige wanamuonea ukweli ndo huo mtaona matokeo
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tehetehetehetehetehetehetehetehe, inawezekana aisee.
   
 8. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Au kamuhonga mwandishi wa makala?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hili gazeti linaweza kutupa habari za kichunguzi kuhusu usafirishaji wa wanyama-pori hai? Au taarifa kuhusu Kamran wa Pakistan?
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Tatizo gazeti la Mtanzania linamilikiwa na Rostam Aziz na Rostam Aziz sasa hivi ndio amenunuwa kampuni ya uwindaji ya Miombo Safaris iko pale Masaki.

  Invisible, Bahati nzuri nimefanya kazi kwenye sekta ya uwindaji kwenye moja ya Kampuni kubwa zilizoorodheshwa hapo, hii ni vita ya kibiashara Watanzania hapa wanalishwa uongo na majungu tupu, hakuna mwenye huruma na nchi hii katika hizo kampuni zote.
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu Hiyo ni vita ya kibiashara inayoendelea hapo, hakuna hata kampuni moja ya uwindaji isiyotumia pesa kufikia malengo yake.

  Tusikubali kulishwa kila aina ya sumu, naelewa A to Z ni nini kinachoendelea hapo. Rostam Aziz ni mtu hatari sana si wa kuchekewa, hiyo kazi ya majungu alikabidhiwa Manyerere Jackton hapo Habari Corporation.
   
 12. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wizara imejaa rushwa,ngorongoro,tanapa,na tawiri ni wizi mtupu,matumizi mabaya ya magzri ya umma
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Unamfahamu Manyerere Jackton? kama unamfahamu basi huwezi kusumbuwa akili yako huyu jamaa njaa yake imepitiliza mpaka ameamuwa kuusaliti utu wake.

  Sijawahi kuona mkoa wa Mara ukitoa makuwadi wa mafisadi kama huyu Manyerere Jackton anatia aibu sana si utamaduni wa watu wa Mara kutumiwa kama ile mipira ya kiume.
   
 14. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Maige kahongwa, na moja ya makampuni linamjengea nyumba Masaki DSM na hata mmoja wa viongozi wa juu serikalini naye kahongwa.

  Huu ni mchezo wa kumlinda Maige, hafai kwa majibu aliyokuwa anatoa leo Bungeni ni ya hovyo sana sana.
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Yaani siasa za Tz ni zaidi ya "siasa uchwara". Gazeti ambalo ni chombo cha kuelimisha limeamua kwa makusudi mazima kuandika ***** kwa nia ya kupotosha na kulinda maslah ya watu fulani.

  Kwa hiyo ni sawa kwa mtu kukodishiwa ekari 1 kwa Tz Shs 220/= kwa mwaka? Je ni sawa watumishi wa wizara walio na kiburi na jeuri kuachwa kuendelea kufuja maliasili ya Tz bila kuulizwa?

  Kama hizo tuhuma za St. Gaspar na nyinginezo ni kweli kwa nini wahusika (na hasa mwandishi) asiende PCCB au Polisi kwani tuhuma hizo ni nzito na ushahidi si upo?

  Next time waandishi pumbavu mafisadi kama hawa wapewe hukumu sawa na wezi wenyewe maana wanashiriki katika uhalifu kwa makusudi mazima. Inatia hasira sana namna hii
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani Manyerere hayupo tena New Habari..... labda kama katumia washikaji aliowaacha kwa kuwa gazeti lao ni la wiki na habari husika ililenga kuingilia ripoti ya Kamati ya Bunge iliyowasilisha taarifa leo. Nakubaliana na waliosema sekta hii ni chafu sana na kuna UMAFIA wa hali ya juuu.

  Kwa kweli, nakumbuka matatizo makubwa tuliyowahi kukumbana nayo huko nyuma kwa kufuatilia ufisadi katika hii sekta. Kuna madudu mengi sana katika hii sekta wakuu na ni hatari sana hata kwa maisha ya watu.

  SI UTANI KUNATISHA SANA HUKO. Kuna baadhi ya wabunge wa zamani walipoteza nafasi zao kwa kuchezea maslahi ya wakubwa wa hiyo sekta ambao ni wachache sana ambao wana mikono katika karibu kampuni zote mnazoziona na wana mikono katika maeneo yote nyeti ya uwindaji.

  Pia waliowalamba miguu walineemeka kasoro mmoja tu ambaye pamoja na kutumia gharama kubwa alikwama kisiasa, lakini wengine walipata nafasi nzito katika siasa za TZ.
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Kama kuna Kampuni kweli inamjengea Nyumba kama unavyodai huko Masaki basi huyu atakuwa Reckless ila mimi ninafahamu fika na kwa ufasaha ni nini kilitokea kule Las Vegas walipokwenda kwenye Exhibition.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona kila mahala ni hongo tu? Yaani kila mtanzania sasa ana bei yake: Waziri bei yake, Naibu Waziri yake, Mbunge yake, Mtumishi wa Umma yake, nk.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Matola Jackton na Balile walishajitoa Habari Corporation wana gazeti lao linaitwa Jamhuri. Kuna jamaa anazifuatilia hizi habari za vitalu pale Habari Corporation kwa muda mrefu sana na ana habari nyingi mno kuhusu vitalu na uwindaji.
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Nafahamu vyema Mkuu hao watu kama wamehama pale New Habari Corporation, hakuna mwenye habari nyingi yeyote pale zaidi ya kulinda maslahi ya Boss wao Rostam Aziz ambaye amenunuwa kampuni ya Miombo Safaris, sasa vita iliyopo ni Rostam kwa kutumia Media zake analeta kampeni za majitaka.

  Hujaelewa vizuri ni kwa nini gazeti la Mtanzania ndio gazeti pekee hapa Tanzania ndio wanajaribu kuwaghiribu Watanzania kwamba wana uchungu na maliasili zetu kitu ambacho si kweli hata kidogo.

  Mkuu naifahamu vyema sekta ya uwindaji na hakuna Mwandishi wa gazeti lolote wa kunilisha mimi habari za kipuuzi ambazo lengo kuu ni kumfurahisha Rostam kwa maslahi ya Miombo Safaris, na kwa hakika nafahamu vyema ni nini kilichotokea Las Vegas wakati wa Exhibition miezi miwili iliyopita.
   
Loading...