Jinsi wababa wanavyokufa mapema

Kikubwa acheni kuwekeza kwa watoto, walee wakue wakajitegemee lakini KAMWE usisahau kujiwekea AKIBA ya kesho yako.

Kosa kubwa ni kulea MTOTO kama uwekezaji ili eti aje akulee ukizeeka, utakuwa DISAPPOINTED big TIME na utakufa ukilaumu.
 
Ngumu kumesa...

Nimejikuta nawazia hii.

Baba anapokuwa bado ana nguvu, yuko kazini huwa anakua na nguvu pamoja na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake, familia humsikiliza, huzingatia uwepo wake!

Muda wa tatizo.

Tatizo huanza pale baba anapozeeka, nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, amestaafu! Na pale watoto wanapokua wamekua watu wazima wameanza maisha yao. Hapo ndiyo mambo kwa baba humgeuka.

Mkewe huanza kumchukulia poa na ile heshima aliyokuwa akipewa huanza kupungua taratiib, baba hasikilizwi tena kama zamani. Isitoshe anakua hahusishwi sana tena kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa atasaidia nini na pesa hana?,badala yake mkewe huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe.

Baba anaachwa pembeni na Mama huanza safari kwenda kwa watoto, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake.

Watoto wanagombea mama aende kwao, lkn baba hakuna anayemtaka.

Wakiwa nyumbani na mkewe, simu toka kwa watoto 80% anapigiwa mama, baada ya maongezi marefu, ndiyo baba anapewa simu anasalimiwa dakika mbili tu.

Imeisha hiyo!

Baba simu anayo japo ni kuu kuu la kizamani tofauti na ya kamera ya mama ila haoni simu za watoto wakimpigia, na wakimpigia ni kwa sababu maalumu tena maongezi huwa mafupi.
Hawana muda nae.

Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe.

Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae. Pale baba anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake sababu ameshazeeka.

Familia humpa kisogo.
Upweke unamsonga. Sababu ya upweke mawazo humsonga, hili hupelekea kinga ya mwili kushuka na kufanya iwe rahisi kushambuliwa na magonjwa na haichukui muda anafariki.

Familia watalia, watachapisha matisheti, watatoa pesa kumnunulia sanduku la gharama na kumjengea kaburi la gharama, mitandaoni watampost sana. Lakini alipokuwa hai "No one cares".

Tuwajali baba zetu, walijitoa na kujinyima sana kufanya tufike tuliko. Ni dhambi mbele za Mungu tena ni laana mbaya kuwapuuza baba zetu.

Wakati unaendelea kumsifia mama yako kuwa ni bora,msifie hata baba kwa kukuchagulia mama aliye bora.Mwanaume unamtumia mama laki moja baba anatumiwa elfu tano hivyo unapoka madaraka ya baba nyumbani maana mwenye pesa ndiye mwenye mamlaka.

Baba anaambiwa usipotii hutakula umesahau nawe ni mwanaume yatakukuta kama hayo.

Ujumbe huu uwafikie wana JF wote na wauangalie kwa jicho la tatu.
Dawa ni kujiwekea akiba ya kutosha na kuanzisha vi-miradi vya kukuingizia mia 2, ukijumlisha na kiinua mgongo chako hautababaishwa nao. Mke kuzurura kwa wanae itategemea na ujinga wa mwanaume kumruhusu. Kwenye maisha nimejifunza kwamba, mwanadamu anaweza kukuacha lakini Mungu hawezi. Mke, watoto nao ni binadamu, haifai kuweka tumaini kwao. Ila mtoto mwenye akili lazima atambue kwamba baraka zao ziko kinywani mwa baba. Ili baraka hizo zitamkwe na baba ni lazima baba afurahi. Ni juu yao kuamua kumfurahisha baba au kumpuuza.
 
Back
Top Bottom