Jinsi Viwanja vya Ndege katika hifadhi hufanikisha ujangiri,Maoni "Tume ya Faru John" yazingatiwe

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Nilikuwa napitia sehemu ya "report" ya kamati iliyoundwa na PM Kassim Majaliwa kuchunguza kifo cha FARU JOHN na mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo.Mwenyekiti wa Kamati Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere ametoa mapendekezo mengi ili kuepukana na kadhia za aina hii katika hifadhi za wanyama pori ktk nchi yetu.

Ni dhahiri kuwa kamati imegundua usanii mwingi juu ya kuhamishwa kwa FARU JOHN.Lakini kuna suala moja ambalo kamati imebaini linalohusu uwepo wa viwanja vya ndege binafsi katika hifadhi na mbuga zetu za wanyama.

Kamati inasema "Kuhusu Viwanja vya ndege na ujangiri,viwanja vingi kwenye hifadhi zinazomilikiwa na wawekezaji havina ulinzi wa serikali.
Tume inaona uwepo wa viwanja hivi YAWEZEKANA kuwa njia za majangili au matajiri kufanikisha shughuli za ujangili nchini".

Jambo hili limekuwa likipigiwa kelele kwa muda mrefu sana.Kuwa viwanja (Airstrip) katika mbuga na hifadhi huko porini vimetumika sana kusafirisha au kuwezesha kusafirishwa kwa nyara za serikali kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kutumia ndege ndogo.Kuanzia mapori ya hifadhi ya Selous,Mbuga za Ruaha,Hifadhi ya Ngorongoro,Mbuga ya Serengeti,Mikumi,Saadani,Mkomazi nk viwanja hivi vimesaidia sana kupakua na kupakia nyara za serikali.

Tanzania bara ina viwanja 58 vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania(ukijumlisha kipya cha Chato vitakuwa 59).Zanzibar Airport Authority inamiliki viwanja viwili vya Unguja na Pemba,TANAPA inamiliki viwanja 26,NCAA(Ngorongoro) wanamiliki viwanja 2,Kilimanjaro Development Co. (KADCO) inamiliki kiwanja kimoja cha KIA na viwanja binafsi (Private Aerodrome) vipo 93.

Utaona katika viwanja vingi vya binafsi huwezi kukuta ulinzi na usalama wa vyombo vya serikali.Vingi ya viwanja hivi viko katika hifadhi za wanyamapori katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.Ambapo wawekezaji wa usafiri wa anga wakishirikiana na wawindaji wenye leseni wamekuwa wakisafirisha nyara za serikali kwa kiwango kikubwa sana.

JINSI INAVYOFANYIKA:
Ndege nyingi zinazoenda porini ni zile ndogo (vipanya) ambazo hubeba watu kati ya 12-14.Nyingi ni zile aina ya C206,C208(Caravan),C404 na Beechcraft KingAir.

Nyingi hutua eneo lenye viwanja korofi,na huenda kwenye viwanja vya porini kama Sasakwa,Behobeho,Siwandu,Likawage,Mtemere,Tishwa nk.Viwanja hivi havina ulinzi wa kutosha.Majangili huchukua nyara za serikali na kusafiri nazo hadi Dsm au KIA zikiwa ndani ya ndege ktk "buti",huweza kukaa ndani ya ndege hata siku mbili na baadae ndege ina-file flight plan ya kwenda matengenezo Nairobi au South Afrika.

Katika ile "General Declaration Form" hawaonyeshi chochote zaidi ya kusema ndege inakwenda kufanya matengenezo,hapo ndio mzigo unasafirishwa kwa urahisi kwenda nje tokea porini kupitia viwanja vikubwa.Makampuni ya ndege zinazofanya "biashara" hii yanafahamika.

Njia nyingine inatumika na matajiri wakubwa na majangili wa kimataifa,ambao huja na ndege zao binafsi katika viwanja vikubwa kama KIA na Dsm na kuziacha ndege uwanjani na kuchukua ndege ndogo zinazoweza kufika porini.Wengi huja kama wawindaji wenye vibari au watalii,na mabadilishano toka ndege waliyokuja nayo kwenda kwenye ndege za kuwapeleka porini hufanyika hapo hapo uwanjani.

Wakati wa kutoka porini,ndege huja moja kwa moja toka porini mpaka katika ndege za binafsi na kuhamisha mizigo iliyotoka porini kuingia katika ndege binafsi tayari kwa safari za nje.Huu ni mtandao ambao hujumuisha mpaka baadhi ya vyombo vya ulinzi kama polisi wanaotakiwa kukagua aina ya silaha za uwindaji na wale wanaopaswa kukagua pasi za kusafiria.Hii njia inatumika sana katika mapori ya Serengeti na Ngorongoro kupitia uwanja wa KIA.

Kule Loliondo,Mwarabu wa Loliondo amejitenezea uwanja wake binafsi wa ndege eneo la TISHWA,na umepewa "Location Indicator" ya ICAO kabisa ikifahamika kama HTSW,huyu ana uwezo wa kutua nq ndege zake moja kwa moja porini akitokea KIA,na baadae kurudi KIA akiwa na "mzigo" wake,anakamilisha taratibu za uhamiaji na kutimua zao kwao.Ujangili huu umefanyika sana katika maeneo ambapo kuna viwanja binafsi,vile vya TANAPA na vile vinavyomilikiwa na NCAA.

Kwa "report" hii ya Tume ya kina Profesa Manyele,Serikali itazame upya usalama na ulinzi wa viwanja vya ndege vilivyopo porini.Hakuna jangiri masikini,majangiri wote wana pesa na hutumia njia ya kitajiri kufanikisha ujangiri wao.Mambo ya kukimbizana na "vijangiri dagaa" vinavyowinda digidigi na nguruwe pori wa kitoweo hauna tija.Mapendekezo ya "Viwanja vya ndege na ujangiri" yaliyotolewa na Prof Manyele yazingatiwe.Ni mapendekezo yaliyochelewa lakini yamekuja muda muafaka.
 
toka 1961 mpk leo ndio wanagundua wanapigwa:mad::mad::mad: naona kakimbilia buzwagi leo kaacha faru john saga:D:D:D
 
Duu! hiyo ripoti ya prof. Manyere ikipitiwa kwa uangalifu,hakika mianya ya ujangiri itaminywa,ngoja tusubiri,lakini hata huu uzi tu ukipitiwa nakufanyiwa kazi ipasavyo,hakika majangiri wakubwa wanaweza kudhibitiwa kwa usahihi zaidi kuliko inavyofanyika sasa.
 
Back
Top Bottom