Jinsi unavyoweza kukubali kosa Polisi na kulikataa Mahakamani

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
JINSI UNAVYOWEZA KUKUBALI KOSA POLISI NA KULIKATAA MAHAKAMANI.

Unaweza kukubali kosa polisi au popote kama serikali za mitaa,sungusungu,nk na baadae kulikataa kosa hilo uwapo mahakamani. Kitu hiki sio jambo la kushangaza na tayari sheria ilishaweka mazingira ya jambo kama hili.

Makala haya hayalengi kuwaelekeza wahalifu mbinu bali kueleza sheria inavyosema. Wapo watu wengi ambao akiwa chini ya ulinzi wa polisi au wananchi wenye hasira hujikuta analazimika au analazimishwa kukiri kosa.

Na kwasababu ya mazingira mtu hujikuta amekiri hata kama hakutenda ili kunusuru maisha yake kwa wakati huo.Lakini pia wengine huwa wamepigwa sana hasa huko mahabusu za polisi.

Ni katika mazingira ya namna hii ambapo mtu anaweza kukiri lakini baadae mahakamani akakataa. Hata hivyo nitoe angalizo na msisitizo kuwa si vyema kukiri kama kweli hujatenda kosa, itokee tu katika mazingira magumu na ya kulazimishwa.

Hii ni kwasababu kunaweza kukawa na ugumu wa kujinasua katika kukiri huko mbeleni mahakamani.

Aidha, yapo maamuzi mengi ya mahakama kuu na ya rufaa yanayoongelea kukiri polisi na kukataa mahakamani ila tuangalie haya mapya katika kesi ya jinai namba 6/2017 kati ya JAMHURI dhidi ya MUHANGWA SIMON mahakama kuu ya Bukoba chini ya Jaji I.C. Mugeta iliyotolewa maamuzi hivi karibuni tarehe 25/9 /2019.

Katika kesi hii mtuhumiwa Muhangwa alikiri kosa la kuua mbele ya polisi huko Biharamulo na akaandikishwa maelezo ya kukiri mbele ya hakimu wa mahakama ya Mwanzo huko Biharamulo.

Alipoletwa mahakama kuu mjini Bukoba kwa ajili ya kusikilizwa kesi yake akakataa kuwa hajawahi kukiri.

Kawaida katika mazingira kama haya mahakama hujielekeza katika misingi mikuu mitatu ambayo hutakiwa kuthibitishwa na upande wa mashitaka ili kuonesha kuwa mtuhumiwa ameamua tu kubadilika lakini alikiri kweli.

Upande wa mashitaka ndio wenye wajibu wa kuitosheleza mahakama kupitia misingi hii kuwa mtuhumiwa alikiri japo sasa anakataa kuwa hakukiri.

Misingi hii ya mahakama nitaieleza ili ikusaidie ikiwa ikatokea ukalazimika kukiri na baadae kukataa, uweze kujua wanaokushitaki wanatakiwa kuthibitisha nini, au wewe uwahoji/uwaulize nini na katika lipi.

Misingi yenyewe ni kama ifuatavyo ; MOSI, wanaokushitaki wawe na ushahidi mwingine unaojitegemea unaoonesha kuwa kweli umetenda kosa(collaboration).

Wasitegemee ushahidi huu wa kukiri pekee kwasababu huo tayari umeishaukataa. Watafute ushahidi mwingine wa kuusaidia huu kuonesha kuwa hata kama umekataa kuwa ulikiri bado kuna hili na lile linakuingiza kwenye kutenda kosa.

Ni wajibu wako kuwahoji kuhusu uwepo wa ushahidi mwingine tofauti na huu wa kukiri. Wakikosa basi kukiri kwako kunakosa nguvu na hivyo kuleta uwezekano wa kuachiwa huru.

PILI, wanaokushitaki wathibitishe kuwa ulikiri bila kulazimishwa. Hii ni kasababu kukiri kwa kulazimisha au kushawishiwa ni sawa na kuwa hujakiri/hukukiri. Wathibitishe kuwa hakukuwa na kulazimishwa.

Hapa pia na wewe unayo kazi ya kufanya. Kazi yenyewe ni kujitahidi kuonesha mazingira ya kulazimishwa kukiri mfano alama za kipigo na mateso mwilini mwako, au mazingira ya hatari kama kuzingirwa na wananchi wenye hasira, au kundi, na mazingira mengine yanayofanana na hayo.

Ukifanikiwa katika hili basi umefanikiwa kufuta kukiri kwako na umekaribia kuachiwa huru.

TATU, wanaokushitaki wathibitishe kuwa ulichokiri ulikuwa ukimaanisha hicho na si vinginevyo. Kwa maana kuwa kukiri kwako hakukulenga kitu kingine chochote bali lile kosa uliloshitakiwa nalo.

Hii ni kwasababu waweza kuwa ulikiri lakini hukuwa umeelewa kile unachokiri. Ni kazi yao wanaokushitaki kuthibitisha kuwa ulichokiri ulilenga kosa husika, lakini pia ni wajibu wako kama ulikiri bila kuelewa kuonesha kuwa hukuwa umeelewa unakiri nini au mazingira hayakuwa rafiki kukupa nafasi ya kuelewa ulichokuwa unakiri.

Kwa ujumla wakishindwa kuthibitisha lolote katika haya matatu niliyoeleza basi ni shaka la msingi katika ushahidi wao hata kama ulikuwa umekiri yafaa mahakama ikubaliane na wewe kuwa hukukiri na uachiliwe huru.

Mwisho, kukiri nilikoongelea hapa kunajumuisha maelezo unayoandika polisi(cautioned statement),na yale yote unayoandika au kusaini popote nje ya mahakama kabla kesi yako kuanza(extra judicial statement).

Hivi ndivyo sheria inavyotaka.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.
 
Katika mazingira ya Jiwe leo, hizo point tatu hakuna ambayo DDP anayo! Na katika mazingira ya dictatorial regime ya Jiwe, basi hawa criminal record yao itafuta huko mbele baada ya jiwe
 
ukubali na ukili mbele ya polisi pamoja na ndugu zako wa karibu wawili kisha uruke futi 90 nasema haiwezekani .Kwa upande wa Sungusungu nakubaliana nawewe 200% polisi nakata kata kama ni sungusungu kwanza hawajasomea pili wanapokuwa wanampiga muhalifu wanapiga kama wanavyopiga nyoka aliyeingia ndani MWA mtu’
 
safi kabisa
 
Hata polisi nao ni vilaza tuu washeria usidanganyike.
 
Napenda kusikiliza kesi mahakamani.
Je naruhusiwa kusikikiza kesi mahakamani, nikiwa mimi sihusiki na chochote katika kesi hio?
 
Nadhani inaruhusiwa mana kuna kipindi tulikuwa tunaimizwa tukasikilize kesi mahakama za mwanzo
 
Napenda kusikiliza kesi mahakamani.
Je naruhusiwa kusikikiza kesi mahakamani, nikiwa mimi sihusiki na chochote katika kesi hio?
Yaani ...mimi niliwahi kwenda mahakamni nikaruka kesi ya ugoni .....japo maandishi ya kukiri yalikuwepo ila tulivyofika mahakamani nikayakataa kabisa

Na hiyo fidia nikaikataa kabisa
Nikawauliza kama walituchukua kutupeleka hospital kutupima km wana pf3...hakuwa nayo

Nikawauliza ule usiku mlikuwa wangapi kama mankumbuka wanajichanganya idadi yao...mashahidi wanajibu tofauti tofauti

Nikawauliza mlituona kbs tukiwa tunashiriki tendo wakadai tulihic tu lile jibu lilinipa nguvu

Nikawauliza mnaushahidi wa picha labda au wa kuninyanganya nguo km kielelezo kigine ili mahakama iniridhishe kuwa nilitenda kosa

Wao walijipanga sana kutegemea ushahidi wa maandishi zaidi .....peke yake

YAANI HAWAKUWA NA HAMNA TENA NA HUKUMU NILISHINDA ILE KESI MAHAKAMANI KABISA KIULAINI ...NA UJUAJI WAO WOTE UKAISHA NIKAJAFUNZA KITU KTK KESI....KUMBE KUPINDUA MEZA INAWEZEKANA !!! KWELI KBS KUKATAA STATEMENT NI JAMBO LA MSINGI
NA KATIKA KESI EPUKA MABUSH LOYER ...TAFUTA MTU ANAYEJUA SHERIA MWAMBIE UKWELI HALAFU ATAKUCHAMBULIA NA KUSHINDA
 
Hongera kwa kushinda kesi. Natumai umeshatubu dhambi ya ugoni/zinaa ili kufuta hiyo nuksi.

Kimsingi, kosa linafutwa na adhabu. Sio ujanja wa maneno. Usipoadhibiwa/jiadhibu kwa kosa ulilolitenda, utakuwa mfungwa nalo na pengine ukaendelea kutenda hilo kosa mpaka likakuangamiza.

Mamlaka zimejaa uonevu. Vema umezikwepa. Ila bado una jukumu la kuichoma hiyo ishu mkuu. Tafuta namna umalizane nayo mazima.
 
Nimalize nayo mazima kivip? Wakati nishaimaliza mahakamani na niko huru
 
Kwenye mahakama za kidunia upo huru, jamaa anauliza je mahakama ya nafsi umemalizana nayo?
Mahakama ya Nafsi iko huru kabisa najihic sina hatia yoyote na najiona ni mwema mwenye Nguvu inayotoka katika nafsi yangu

.....dhamri yangu inanishuhudia na Mungu ananishuhudia !!

Na ninaona Mungu tu alinisimamia kuna mahali nilitaka kujisahau sana ...akaruhusu litokee ili nipate cha kujifunza
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom