Jinsi unavyopata mikosi na laana bila kujijua

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
7,554
9,531
Kheri wapendwa wakubwa kwa wadogo
Leo ni siku nyingine tena tuutazame mzunguko wa maisha yetu ya kila siku

Nianze kwa kusema tu baadhi yetu tumekuwa na tabia au mazoea ya kufanya mambo kwa kujiona Wajanja kumbe ni kujitafutia mikosi na laana bure unakuta mtu miaka na miaka anafanya biashara hata Maendeleo hakuna kumbe anafanya vitu vya hovyo kabisa

1. Wauza maziwa hawa tabia zao ni kuweka maji kwenye maziwa hii laana tosha kabisa unafanya biashara isivyo

2. Mama ntilie hawa tabia zao zinajulikana kutuwekea hamira kwenye chakula haramu hiyo mafanikio utayasikia tu

3. Mdereva taxi mmekuwa mkitoza tozo kinyume na uhalali na mkifika vijiweni mnaanza kujisifia kuwa kuna abiria umempiga radi mkiwa na maana ya kuwa umemtoza bei kubwa kuliko

4. Wauza samaki dagaa mboga mboga baadhi yenu na nyie siyo waaminifu hata kidogo mnatulisha uchafu ili nyie mpate pesa

5. Makonda wa magari na nyie siyo waaminifu hata kidogo

Mko wengi sana ambao siyo waaminifu mtakalia hivyo hivyo mpaka kifo badilikeni laana zingine mnajitafutia tu
 
Mwenye uwezo wa kulaani ni mwanamke tu!
Nakupongeza sana kwa mada hii,umesema ukweli kabisa.Mimi hii kitu huwa naisema mara nyingi sana.
Juzi kati hapa kuna fundi seremala mmoja nilimpa kazi ya kukarabati meza yangu moja ya zamani kwa shughuli maalum.
Nikamlipa malipo ya awali sh 60000.baadae akaniambia nimuongeze sh 20000 kwa ajili ya kununua mbao moja mpya,nikampa akaweka mbao za zamani badala ya mpya.
 
Kuna kundi moja umelisahau hapa mkuu.. mafundi ujenzi. Wengi wao hawataenda mbinguni asilani. Tuseme mafundi wote tuu hii inawahusu.
 
Nakupongeza sana kwa mada hii,umesema ukweli kabisa.Mimi hii kitu huwa naisema mara nyingi sana.
Juzi kati hapa kuna fundi seremala mmoja nilimpa kazi ya kukarabati meza yangu moja ya zamani kwa shughuli maalum.
Nikamlipa malipo ya awali sh 60000.baadae akaniambia nimuongeze sh 20000 kwa ajili ya kununua mbao moja mpya,nikampa akaweka mbao za zamani badala ya mpya.
Huyo umaskini mpaka kiama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila kuwa mwaminifu kwenye kazi yoyote ni hatari sana.

Kazi yoyote inahitaji nidhamu pamoja na uaminifu.

Jaribu kufanya tathmini ndogo tu uangalie watu ambao hawana uaminifu uone hatua walizopiga ni zero.

Mtu hata akifanikiwa leo kwa njia ya udhulumaji huko aendako ni lazima mambo yaharibike tu.

Hata kama atafariki na kuacha mali nyingi lazima watoto wapigane kwanza au ikibidi wauane kwanza na mwisho watauza tu na kubaki na hali mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingsharon92 huu uzi wako umenifikirisha!
Juzi nilipiga mahali 10,000/= (sio kuiba kwa haswaa), nikanunua vocha ili nipate bando la kuchat humu JF, huwezi kuamini kilichotokea niliweka vocha halafu nikasahau kujiunga na kifurushi!!! Kesho yake nashangaa meseji huna salio la kutosha. hahahhah
Yaani kweli Mungu hataki dhihaka. hahahahahahahah
 
wanaokopesha kwa riba bila utaratibu maalum, hii ni dhuluma kubwa sana, jiulize jamaa kakupa 500,000/= umrudishie 1,000,000/=,

Mda huo unashida imekubana unaweka dhamana hata ya kiwanja, jamaa anakuja kuchukua kiwanja kisa hujamlipa m1 kavu..

wengine wanatumia mpaka dawa yaani hata kama deni ni dogo hutalipa mpaka anachukua dhamana uliyoiweka kama ni ya thamani kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom