ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,030
- 3,908
Ni ukweli usiopingika kwamba Magufuli amethibitisha kwamba yeye ni chuma.
Pamoja na jitihada zake nyingi za kujaribu kujenga Tanzania Mpya na mafanikio ambayo tunayaona kuna maeneo ambayo kwa hakika kabisa anaenda kukiua chama cha Mapinduzi CCM na kuimarisha chama cha Upinzani hasa Chadema.
Jambo la hatari zaidi ni kwamba kuna kitu kingine kinajengwa ambacho ni Movement ya wananchi wenyewe isiyokuwa na uhusiano na chama cha siasa ambayo wenzetu duniani wanatumiaga misemo kama(Citizens United)Maandamano ya Halaika,Popula Movements,Public activism na masuala kama hayo)
Ni ukweli usiopingika kwamba kadiri siku zinavyokwenda,Wananchi wananzidi kuwa na Nguvu sana dhidi ya watawala na wanasiasa na inakuwa ngumu kuwashawishi wananchi kwa propaganda na badala yake wnananchi wanatazama kwa macho na kuchambua kwa akili zao na kuamua kwa utashi wao ama kukubali au kukataa bila kujali ni nani mhusika.
Si ajabu kuona wananchi wakiwakosoa viongozi waziwazi,wakitoa maoni makali na kupinga masuala mbalimbali bila hofu.Tunapoelekea ndiko huko.
Sasa hivi hakuna siasa za Public sympath wala siasa za hongo na utapeli,watu ukiwapa pesa wnakula na bado wanakuwa na uhuru bila hofu.
Sasa nieleze ni kwa vipi ukiritimba wa Magufuli unaiua CCM.CCM ni Taasisi ambayo kimsingi ina mifumo na taratibu zake.Mheshimiwa Magufuli tangu ameingia madarakani katika serikali na katika chama amekuwa ni mtu wa maauzi yake tu na misimamo yake tu,yaani badala ya kuimarisha mifumo yeye anabomoa na kutumbua watu akiona wanatofautiana kimsimamo,kimaono na hata akiona hawaendani na mfumo wake wa kufanya maamuzi yake.Hali hii imejenga siasa za kujikomba,unafiki,uzandiki na chuki za chini kwa chini kati ya wana CCM wenyewe na hata ndani ya serikali.Lakini hili limezidi zaidi kuwafanya wananchi kutambua tabia halisi za viongozi wengi na hivyo kuwezesha watu kutambu kwa kina kile ambacho kinaendelea ndani ya chama na ndani ya serikali.Hili limepelekea CCM kutoungwa mkono na watu Makini na badala yake kimejaa Mamluki wanaojaribu kujikomba ili kupata vyeo na fursa
Pili Ukiritimba huu pia unapelekea Chadema kupata nguvu kwani kwa hakika wanatumia madhaifu haya kujifunza na kujijenga zaidi kama Taasisi.Kwa kawaida kabisa Taasisi kama Chadema ambayo inapingwa kwa nguvu sana inahitajika kujijenga kimifumo na hilo ndio ninaloliona kwani chama kimeweza kufanya SIASA pamoja na mazingira magumu nan kuendelea kuwa chama chenye nguvu pamoja na ushindani mkali.Ukifuatilia uchaguzi wa Chadema wa Mwaka huu utaona ni kwa kiasi gani chama kimeimarika kimfumo.Kura hazipigwi kwa rushwa au kuzingatia umaarufu bali zinapigwa kwa utashi na uhuru.
Ukifuatilia ziara za viongozi wa serikali utaona kabisa jinsi wananchi wanavouliza maswali magumu ya msingi bila hofu,Wananchi wnanafuatilia kwa karibu kila jambo na kama haliko sawa wanafuatilia kwa kina kupata Majibu na suluhu.Huu ni uthibitisho kwamba wananchi wameamua kwa sasa kuisimamia serikali baada ya Vyombo vyao kama Bunge kushindwa kutimiza wajibu huo kikamilifu
Mwaka 2020 utakuwa mwaka tofauti sana katika siasa za Tanzania.Kutakuwa na Mabdiliko Mengi sana.Ni muhimu sana JPM akaanza kujenga Mifumo thabiti ya Kichama na Kiserikali ili hata kama atapoteza Urais 2020 basi heshima yake aliyojijengea kwa awamu yake hii isifutwe kwa kuingia kiongozi ambaye atakuta mifumo dhaifu ya uongozi.
Wasalaam
PBK