Jinsi Ukiritimba wa Magufuli unavoiua CCM na Kuijenga Chadema na Popular Movement

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Messages
1,800
Points
2,000

ubongokid

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2017
1,800 2,000
Ni ukweli usiopingika kwamba Magufuli amethibitisha kwamba yeye ni chuma.

Pamoja na jitihada zake nyingi za kujaribu kujenga Tanzania Mpya na mafanikio ambayo tunayaona kuna maeneo ambayo kwa hakika kabisa anaenda kukiua chama cha Mapinduzi CCM na kuimarisha chama cha Upinzani hasa Chadema.

Jambo la hatari zaidi ni kwamba kuna kitu kingine kinajengwa ambacho ni Movement ya wananchi wenyewe isiyokuwa na uhusiano na chama cha siasa ambayo wenzetu duniani wanatumiaga misemo kama(Citizens United)Maandamano ya Halaika,Popula Movements,Public activism na masuala kama hayo)

Ni ukweli usiopingika kwamba kadiri siku zinavyokwenda,Wananchi wananzidi kuwa na Nguvu sana dhidi ya watawala na wanasiasa na inakuwa ngumu kuwashawishi wananchi kwa propaganda na badala yake wnananchi wanatazama kwa macho na kuchambua kwa akili zao na kuamua kwa utashi wao ama kukubali au kukataa bila kujali ni nani mhusika.

Si ajabu kuona wananchi wakiwakosoa viongozi waziwazi,wakitoa maoni makali na kupinga masuala mbalimbali bila hofu.Tunapoelekea ndiko huko.

Sasa hivi hakuna siasa za Public sympath wala siasa za hongo na utapeli,watu ukiwapa pesa wnakula na bado wanakuwa na uhuru bila hofu.

Sasa nieleze ni kwa vipi ukiritimba wa Magufuli unaiua CCM.CCM ni Taasisi ambayo kimsingi ina mifumo na taratibu zake.Mheshimiwa Magufuli tangu ameingia madarakani katika serikali na katika chama amekuwa ni mtu wa maauzi yake tu na misimamo yake tu,yaani badala ya kuimarisha mifumo yeye anabomoa na kutumbua watu akiona wanatofautiana kimsimamo,kimaono na hata akiona hawaendani na mfumo wake wa kufanya maamuzi yake.Hali hii imejenga siasa za kujikomba,unafiki,uzandiki na chuki za chini kwa chini kati ya wana CCM wenyewe na hata ndani ya serikali.Lakini hili limezidi zaidi kuwafanya wananchi kutambua tabia halisi za viongozi wengi na hivyo kuwezesha watu kutambu kwa kina kile ambacho kinaendelea ndani ya chama na ndani ya serikali.Hili limepelekea CCM kutoungwa mkono na watu Makini na badala yake kimejaa Mamluki wanaojaribu kujikomba ili kupata vyeo na fursa

Pili Ukiritimba huu pia unapelekea Chadema kupata nguvu kwani kwa hakika wanatumia madhaifu haya kujifunza na kujijenga zaidi kama Taasisi.Kwa kawaida kabisa Taasisi kama Chadema ambayo inapingwa kwa nguvu sana inahitajika kujijenga kimifumo na hilo ndio ninaloliona kwani chama kimeweza kufanya SIASA pamoja na mazingira magumu nan kuendelea kuwa chama chenye nguvu pamoja na ushindani mkali.Ukifuatilia uchaguzi wa Chadema wa Mwaka huu utaona ni kwa kiasi gani chama kimeimarika kimfumo.Kura hazipigwi kwa rushwa au kuzingatia umaarufu bali zinapigwa kwa utashi na uhuru.

Ukifuatilia ziara za viongozi wa serikali utaona kabisa jinsi wananchi wanavouliza maswali magumu ya msingi bila hofu,Wananchi wnanafuatilia kwa karibu kila jambo na kama haliko sawa wanafuatilia kwa kina kupata Majibu na suluhu.Huu ni uthibitisho kwamba wananchi wameamua kwa sasa kuisimamia serikali baada ya Vyombo vyao kama Bunge kushindwa kutimiza wajibu huo kikamilifu

Mwaka 2020 utakuwa mwaka tofauti sana katika siasa za Tanzania.Kutakuwa na Mabdiliko Mengi sana.Ni muhimu sana JPM akaanza kujenga Mifumo thabiti ya Kichama na Kiserikali ili hata kama atapoteza Urais 2020 basi heshima yake aliyojijengea kwa awamu yake hii isifutwe kwa kuingia kiongozi ambaye atakuta mifumo dhaifu ya uongozi.

Wasalaam

PBK
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
1,164
Points
2,000

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
1,164 2,000
Vikundi hivyo vya maandamano na migomo vilikuwa ni "projects" za UKAWA na washirika hasa CHADEMA ,Sasa vimekufa baada ya CHADEMA kusambaratika. Prove me wrong if am incorrect
 
ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Messages
1,800
Points
2,000

ubongokid

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2017
1,800 2,000
Vikundi hivyo vya maandamano na migomo vilikuwa ni "projects" za UKAWA na washirika hasa CHADEMA ,Sasa vimekufa baada ya CHADEMA kusambaratika. Prove me wrong if am incorrect
Kwanza hakukuwahi kuwa na vikundi kama hivo,Ila sasa hivi kuna force kubwa kuliko hivo vikundi.Nguvu ya vikundi hivi umeiona kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa n.k.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,588
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,588 2,000
Uwezi kuliona hilo kama uko sentimental.Na wala hutaelewa kwa sasa mpaka itakapokamilika
Hakuna na hakujawahi kutokea movement yoyote Dunia hii bila ya kuwa na Kiongozi au mtu anayeratibu, sasa nani huyo mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania dhidi ya Serikali? Kuna namna mbili tu hilo kuweza kufanikiwa TZ aidha kutumia Dini yaani atokee mtu awaaminishe Dini fulani kwamba maslahi yao ya kidini TZ yanaminywa hivyo ni lazima wayadai kwa kila hali au kundi la Kikabila kwa lengo hilo hilo kama la kidini, na lazima huyo anayeratibu awe na sapoti kubwa sana nje ya nchi kama ni peke yake hafiki popote kwani two shots and he is gone.
Ukiondoa hizo sababu 2 hakuna chochote kinachoweza kuwafanya watu watengeneze hiyo movement.

Kila movement Duniani ina sababu ambayo itamfanya mtu awe tayari kuifia na ni lazima hiyo movement ina Kiongozi na huyo Kiongozi ni lazima awe ametengeneza network kubwa nje ya nchi, sasa kwa Tanzania bado sana kufikia huko.
 
Nafikiri ilimu yako kuhusu movement iko limited,Unachopaswa ufahamu ni kwamba kabla hayo unayotaja hayajafanyika lazima kuwe na factors nyingine zinazowezesha hayo kufanyika.Hizo factors nyingine ziko sana na kila siku tunaona dalili zake kwenye media na mitaani.Wafadhili watatokea na viongozi watatokea mambo yakikamilika.Ila unaweza kufikiri tofauti
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,588
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,588 2,000
Nafikiri ilimu yako kuhusu movement iko limited,Unachopaswa ufahamu ni kwamba kabla hayo unayotaja hayajafanyika lazima kuwe na factors nyingine zinazowezesha hayo kufanyika.Hizo factors nyingine ziko sana na kila siku tunaona dalili zake kwenye media na mitaani.Wafadhili watatokea na viongozi watatokea mambo yakikamilika.Ila unaweza kufikiri tofauti

Hakuna kitu kama hicho, kama ingekuwa ni rahisi hivyo Dunia nzima kungekuwa na Mapinduzi kila siku, usidanganywe na mainstream media, hizo movements unazoona zinaangusha Serikali nchi nyingine ziko planned sema wanaopanga na kuratibu hauwaoni, kwanza unahitaji fedha nyingi sana kulipa watu, hakuna mtu atakubali kuumizwa au kufa hivi hivi tu kwa kuwa eti wewe haupendi Serikali yaani aandamane kwa ajili yako ? Wewe ni nani? Ila toa hela utapata watu wa kutengeneza anarchy, na hilo ni Dunia nzima.
 
herzegovina

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Messages
2,769
Points
2,000

herzegovina

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2015
2,769 2,000
Kupambana na MAGUFULI ni vigumu sana kwa sababu yeye hana aibu....Anaweza kukufanyia "UMAFIA" hata kama itaonekana dhahiri kuwa ni yeye kahusika, anaweza kukudhulumu hata kama itaonekana dhahiri kuwa kakudhulumu.

Pia MAGUFULI anajulikana kwa kupenda sifa/kusifiwa. Wateule wake wote wanalijua hili hivyo hata kama atapata kura mbili tu ambazo atajipigia yeye mwenyewe na Bashite bado watatangaza kuwa amepata kura 19,999,999 kati ya kura halali 20,000,000 na kura moja iliharibika.
 
ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Messages
1,800
Points
2,000

ubongokid

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2017
1,800 2,000
Hakuna kitu kama hicho, kama ingekuwa ni rahisi hivyo Dunia nzima kungekuwa na Mapinduzi kila siku, usidanganywe na mainstream media, hizo movements unazoona zinaangusha Serikali nchi nyingine ziko planned sema wanaopanga na kuratibu hauwaoni, kwanza unahitaji fedha nyingi sana kulipa watu, hakuna mtu atakubali kuumizwa au kufa hivi hivi tu kwa kuwa eti wewe haupendi Serikali yaani aandamane kwa ajili yako ? Wewe ni nani? Ila toa hela utapata watu wa kutengeneza anarchy, na hilo ni Dunia nzima.
Kwa hio haiwezekani kwa Tanzania sio?
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,588
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,588 2,000
Kwa hio haiwezekani kwa Tanzania sio?

Sijasema haliwezekani, kila kitu kinawezekana ila kwa sasa hakuna hayo mazingira ya kuunda hizo movements, TZ haina ugomvi na Big powers, Ushirikiano ni mzuri hivyo hakuna sababu kwa sasa kwa mtu yoyote kuunda na kusapoti hizo movements.
 
Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
276
Points
250

Poa 2

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2019
276 250
Hakuna na hakujawahi kutokea movement yoyote Dunia hii bila ya kuwa na Kiongozi au mtu anayeratibu, sasa nani huyo mwenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania dhidi ya Serikali? Kuna namna mbili tu hilo kuweza kufanikiwa TZ aidha kutumia Dini yaani atokee mtu awaaminishe Dini fulani kwamba maslahi yao ya kidini TZ yanaminywa hivyo ni lazima wayadai kwa kila hali au kundi la Kikabila kwa lengo hilo hilo kama la kidini, na lazima huyo anayeratibu awe na sapoti kubwa sana nje ya nchi kama ni peke yake hafiki popote kwani two shots and he is gone.
Ukiondoa hizo sababu 2 hakuna chochote kinachoweza kuwafanya watu watengeneze hiyo movement.

Kila movement Duniani ina sababu ambayo itamfanya mtu awe tayari kuifia na ni lazima hiyo movement ina Kiongozi na huyo Kiongozi ni lazima awe ametengeneza network kubwa nje ya nchi, sasa kwa Tanzania bado sana kufikia huko.
Kushibdwa kuheshimu na kuthamini utu wa mtu/watu huwa sababu kubwa sana ya hayo makundi unayoyaeleza ila udini ukabila ubaguzi ni matawi tu ccm endeleeni kuwadharau kuwaua kuwakejeli kuwatukana wapinzani na wananchi wenye mawazo tofauti na ninyi mliopomadaraka halafu tembeeni kifua mbele mkiimba mapambio ya amani baada ya mda wa miaka michache tutaona kama tanzania itakuwa salama
 
Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
276
Points
250

Poa 2

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2019
276 250
Hakuna kitu kama hicho, kama ingekuwa ni rahisi hivyo Dunia nzima kungekuwa na Mapinduzi kila siku, usidanganywe na mainstream media, hizo movements unazoona zinaangusha Serikali nchi nyingine ziko planned sema wanaopanga na kuratibu hauwaoni, kwanza unahitaji fedha nyingi sana kulipa watu, hakuna mtu atakubali kuumizwa au kufa hivi hivi tu kwa kuwa eti wewe haupendi Serikali yaani aandamane kwa ajili yako ? Wewe ni nani? Ila toa hela utapata watu wa kutengeneza anarchy, na hilo ni Dunia nzima.
Kwa wengine linawezekana kutokea ila kwa tanzania bado kwa sababu tz ni sayari nyingine nje ya dunia.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,588
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,588 2,000
Kushibdwa kuheshimu na kuthamini utu wa mtu/watu huwa sababu kubwa sana ya hayo makundi unayoyaeleza ila udini ukabila ubaguzi ni matawi tu ccm endeleeni kuwadharau kuwaua kuwakejeli kuwatukana wapinzani na wananchi wenye mawazo tofauti na ninyi mliopomadaraka halafu tembeeni kifua mbele mkiimba mapambio ya amani baada ya mda wa miaka michache tutaona kama tanzania itakuwa salama

Hakuna kitu kama hicho, hayo malalamiko yapo kila mahali na kila jamii lkn hayajawahi kuleta mapinduzi, kwanza Mapinduzi popote pale huletwa na foreigners na wao huwa na maslahi yao binafsi na haijawahi kuwa kwa maslahi ya Wananchi ingekuwa hivyo Libya, Irak, Misri, kote huko kungekuwa na neema leo hii lkn kilichotokea ni upande wa malalamishi kubadilia, na hali hata kuwa mbaya zaidi.
 
KYALOSANGI

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Messages
2,936
Points
2,000

KYALOSANGI

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2011
2,936 2,000
Wapiga mapambio hawewezi kuliona hili...wengine wanaona lakini wanantumikia kafiri.Mfano tu asilimia kubwa ya Watumishi wa Umma,hawakubalina na Mambo yanavyoenda ila majibu watafanya Nini wa wanauo mioyoni Mwao!
 
Forum statistics

Threads 1,380,347
Members 525,767
Posts 33,770,700
Top