Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Jinsi Ukawa ilivyoua demokrasia ndani ya vyama vishiriki na kuongeza udini,ukanda na ukabila miongoni mwa wananchi.
Kama ambavyo tunahitaji kuwe na fursa ya mgombea binafsi uamuzi wa muungano wa vyama (Ukawa) kusema jimbo au kata hii tunamwachia mgombea wa chama Fulani ni kurudi nyuma miaka 100 kulekea kwenye demokrasia ya vyama vingi.Yawapasa wananchi wawe na machaguo mengi iwezekanavyo ili wachague wanayemtaka. Ni upuuzi kusema eti majimbo ya Moshi na Arusha tuwaachie Chadema kwa sababu viongozi wajuu na waasisi wa chama hicho wanatokea huko kwa hiyo vyama vingine kama CUF kuonekama havitakiwi kusimamisha wagombea huko kwa kigezo wao (CUF) ‘wanakubalika kusini’. Madhara yake ni mengi kama ifuatavyo;
Kuna vyama vina hatimiliki ya kufanya siasa mahali Fulani na kujenga taswira ya udini,ukabila na ukanda..hili ni donda kubwa sana na hakika linatafuna demokrasia kwa wagombea katika vyama vya siasa.
Wengi, watasema mbona Kenya wanafanya…hakika hata Kenya wanakosea ndio maana muunganiko wa vyama vyao kabla ya uchaguzi huwa ni muunganiko wa makabila Fulani dhidi ya makabila Fulani, Kenya hakuna siasa za hoja bali ni siasa za chief mwenye wanachi wengi ndiye mtawala,nani anataka tufike huko. Kwa mfano Afrika kusini, vyama vyote husimamisha wagombea kila jimbo na baada ya uchaguzi kama hakuna chama chenye ‘majority’kuunda serikali ndipo hufanya makubaliano na vyama vingine kwa kugawana madaraka kuendesha serikali, jimbo au Manispaa…na hivi ndivyo ilivyo hata ulaya. Ndio maana mwaka 2010 David Camoroun ilimpasa kuungana na Nick Cleig wa Lib.Democrat kupata ‘majority’ ili kuunda serikali, lakini mwaka 2015 conservative ilipata viti vya kutosha kuunda serikali na walitengana na Lib Democrats ili kuendesha serikali kwa kuzingatia sera zao (Conservative) ambazo kimsingi ndizo chaguo la wananchi.
Ushahidi wa haya umeonekana tokea kipindi cha uchaguzi baadhi ya vyama kucheza rafu kwa kusimamisha wagombea, ni hulka ya mwanasiasa yeyote kutoa mchango wake kwa kuomba uongozi kama utasema wewe subiri muachie kwanza huyu halafu kesho itakuwa zamu yako. Huu ndio mwanzo wa chuki na kutokuaminiana. Mathalani, Je Mbatia atakubali kuacha kugombea ubunge 2020 ili kumpisha mgombea wa Chadema na kumuunga mkono? Hapa ndipo patakapochimbika, si Vunjo tu bali sehemu nyingi zitazua migogoro na kabla ya uchaguzi wa 2020 ni dhahiri hakutakuwa na makubaliano ya kuachiana majimbo,kata na hata uraisi miongozi mwa vyama shiriki Ukawa.
Kama wanasiasa wanafikiri ni muhimu kwa na sheria ya kuruhusu vyama vya siasa kuungana ili kupata wagombea ni vema wafikirie kuamua kuua vyama vyao na wakubaliane kutengeneza chama kimoja chenye nguvu ili kuleta mantiki ya hoja na itikadi