Jinsi Taliban wanavyoyazima maandamano hawana tofauti sana na Serikali yetu

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,712
11,688
Imeripotiwa kwamba leo baadhi ya wanawake wa Afghanistan waliandamana wakipinga kuundwa kwa serikali mpya chini ya Taliban ambayo haina waziri mwanamke hata mmoja.

Katika harakati za kuzia maandamano hayo Taliban wamewatembezea vipigo waandamanaji pamoja na waandishi wa habari walikuwa wanaripoti maandamano hayo. Wengine wamekamatwa na kuwekwa kizuizini.

Sambamba na hilo, Taliban wamedai kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria, kwani ni lazima uwe na kibali cha serikali ili uruhusiwe kuandamana. Pia ni marufuku watu kutumia lugha ya kuudhi dhidi ya serikali.

Matendo haya ya Taliban yamenikumbusha rafiki zangu wawili kutoka Kabul niliokutana nao Karachi nchini Pakistan miaka michache iliyopita, walinieleza kuwa wakati wa utawala wa Taliban kabla ya kung'olewa na Marekani kulikuwa na 'amani' 😀. Japo wezi walikatwa mikono, 'wasaliti' walinyongwa hadharani kwenye viwanja vya michezo, Taliban walikuwa juu ya sheria zote na ukatili mwingine mwingi chini ya bendera ya 'amani na utulivu'.

Nimetafakari, naona hata sisi hapa nchini tunayo 'Taliban' yetu, ambayo baada ya kuiba uchaguzi na kushika dola kwa njia haramu imepiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano ya vyama pinzani, inataka vyama vya pinzani viombe ruhusa ili kufanya mikutano ya ndani na vikao. Taliban hii inatumia ukatili na vitisho kuwatawala wananchi kwa kisingizio cha 'amani' na sasa 'kujenga uchumi'

Hata wakoloni hawakuwatendea ukatili huu watanganyika na wazanzibari, na ndio maana akina Kambona na Nyerere waliweza kuzunguka nchi nzima kuinadi TANU. Wakati wazee hawa wanadai uhuru wa kujitawala sijui kama wao na wananchi wenzao walikuwa wanatizamia aina hii ya 'uhuru' tuliyo nayo sasa, natilia shaka.
 
Taleban wako honest, hawana mpango na demokrasia tofauti na siye tunajifanya wana demokrasia wakati siyo!
Nadhani hiyo ni miongoni mwa tofauti zetu. 'Taliban' yetu ni wanafiki wakubwa, kwa kutaka fedha za mabeberu wanaigiza kuwa kuna demokrasia nchini wakati kiuhalisia tuko chini ya udikteta wa chama kimoja kwa miongo sita sasa.
 
Kwa ujumla, Tanzania ni kati ya nchi zinazoongozwa kidikteta na ukatili wa hali ya juu. Lakini udikteta na ukatii wake umetiwa manukato ili harufu ya mzoga isisikike kwa wapita njia.

Kwa sasa, angalao kidogo, mataifa na taasisi mbalimbali za kimataifa zinajua kuwa Tanzania inaongozwa kidikteta, tofauti na zamani.

Katika Afrika Mashariki, kwa sasa, Tanzania kwa vigezo vyote, ndiyo inayoongoza kwa udikteta, ikifuatiwa na Rwanda na Burundi. Uganda, Sudan Kusini na Kenya are much better kuliko Tanzania. Kenya, kwa vigezo vyote, ndiyo inayoongoza kwa demokrasia na utawala wa sheria katika Afrika Mashariki
 
Back
Top Bottom