Jinsi sogea tuishi ilivyoharibu thamani ya ndoa

gidlameck

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
604
500
Sasa hivi kumekuwa na wimbi kubwa sana la ndoa sogea tuishi hali iliopelekea kupoteza na kuondoa heshima na ladha ya ndoa kwa ujumla.

Unakuta binti jioni yupo kwao asubuhi mnaamka mnamwona kwa John ukiuliza utaambiwa kaolewa unajiuliza mbona ndoa zimekuwa rahisi hivi kumbe sogea tuishi.

Baada ya mwezi unamuona karudi kwao na hana shida kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea zamani japo sio mhenga lakini niliona baba zetu wakitaka kuoa garama zilihusika tena kubwa mtu anatoa ng'ombe 15

Hii ilichangia ndoa kuwa na heshima kwa kiwango kikubwa lakini leo maneno tu yanatosha kuanza maisha Mungu ibariki Tanzania hasa wakati huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
3,728
2,000
Utaratibu mbaya huu ila na mimi naufanya. UE inaisha navuta pisi kali nakula utawala wala haendi kwao. Sisi vijana wa sikuhizi tumeharibiwa na wazee wa sikuhizi, tushirikiane kulaumiana.

Sasa kama hela ya kusuka na ya mchezo nampa, kwa nini asiishi hapa. Mchawi friji, smart TV, ghetto kali, mzunguko wa pesa na mambo kama hayo. Ikitokea ukaongeza NETFLIX tiyari ushakuwa Michael Bloomberg wa bongo.

NB: Nimeandika kihuni kuelezea uhalisia
 
MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,823
2,000
Heshima ya ndoa iko pale pale kwa watu wanaojitambua bila kujali mlango walioingilia kwenye ndoa.

Suala la kuachana lipo pale pale bila kujali umetoa mahari ya ng'ombe 15, milioni 5, umefunga ndoa kanisani/msikitini au bomani kutegemeana na wahusika wenyewe.

Kwa kipindi hiki hasara za kufunga ndoa ni kubwa kuliko faida:
Mosi:Gharama kubwa sana kukamilisha harusi

Pili: Unafunga ndoa kwa gharama kubwa huku mke mwenyewe ni used/second hand. Nini hiki kama si ufala? Second hand wife unamtolea ng'ombe 15 au m3?
Ujanja hapa ni sogea tuishi-nawapongeza sana wanaosogeza tu.
 
Hapo kwenye used ndio anguko lilipoanzia hapo ndipo kipa alipoliacha lango wazi
 
the supporter

JF-Expert Member
Aug 18, 2013
708
1,000
Mkuu usisahau miaka ina kwenda, vumbuzi mbalimbali zaki sayansi zina toka kila siku, research pia zina fanyika kila siku, tathimini ya maswala mbalimbali pia zina fanywa na kupatikana basi na tabia za viumbe vile vile zimebadilika kutokana na mazingira na technlogy tulio nayo sasahivi. Watu hawa taki cheni ndefu za kufunguna kwa viapo vingiii simple una kuja tuna test mitambo kikieleweke fresh kikibuma bila kelele mingi 50/50.
 
MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,823
2,000
Hapo kwenye used ndio anguko lilipoanzia hapo ndipo kipa alipoliacha lango wazi
Hakika kabisa, wasichana wengi used kitu ambacho ni aibu kabisa kusimama mbele ya mchungaji/padre au shekh kufunga ndoa huku kuna boya mwingine aliyekuwa anakula mzigo anakucheki tu na kapewa kadi ya mwaliko na pengine kapiga mzigo wiki iyo hiyo ya ndoa.
 
gidlameck

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
604
500
Mkuu usisahau miaka ina kwenda, vumbuzi mbalimbali zaki sayansi zina toka kila siku, research pia zina fanyika kila siku, tathimini ya maswala mbalimbali pia zina fanywa na kupatikana basi na tabia za viumbe vile vile zimebadilika kutokana na mazingira na technlogy tulio nayo sasahivi. Watu hawa taki cheni ndefu za kufunguna kwa viapo vingiii simple una kuja tuna test mitambo kikieleweke fresh kikibuma bila kelele mingi 50/50.
kumbe
 
Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
746
1,000
Kuzuia uhamisho wa watumishi wa umma imesababisha hizo ndoa za sogea tuishi. Natumaini mama samia atalegeza masharti yaliopo na watumishi wenye ndoa watapata haki yao ya kuishi pamoja kama sheria ya ndoa inavyotaka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom