Jinsi simu yako inavyoweza kukusaidia kupaipata gari yako au pikipiki yako iliyo ibiwa.

mjapanimweusi

Member
Feb 11, 2019
26
11
Jinsi simu yako inavyoweza kukusaidia kuipata gari yako au boda boda iliyo ibiwa.

Kabla ya kufahamu jinsi simu inavyoweza kutusaidia kupata gari au boda boda iliyo ibiwa kwanza tufahamu vitu hivi muhimu GPS,GPRS,WiFi LOCATOR na CELL TOWER TRIANGULATION

GPS ni nini?

Ni mfumo wa kutambua sehemu ya eneo katika uso wa dunia kwa kutumia mistari ya longitudes na latidudes kwa msaada wa settellites.

Mfumo huu ili ukamilike,unahitaji vifaa viwili GPS SETTELITES na GPS RECEIVER.

Vifaa hivi viwili vinategemeana katika kukamilisha tendo la kutambua eneo katika uso wa dunia.

Kuna settellites zaidi ya 30,ambazo zinaizunguka dunia kuweza kufanikisha zoezi hilo.

GPS Receiver ndiyo inayosomwa na settellite mahali ilipo,Hivyo gps receiver ndiyo inayo tengeneza point ya utambuzi wa eneo.

Kwa maana hii ili uweze kujua kifaa (gari,pikipiki n.k)vipo wapi ni lazima gari au pikipiki kiwe kimefungwa GPS RECEIVER.

Hivyo setellites huwasiliana na kifaa hicho (gps receiver iliyofungwa ktk gari au bodaboda yako) moja kwa moja na kutambua eneo gari lako au bodaboda lilipo kwa kutumia longitudes na latitudes.

Baada ya kutambua wapi kifaa kilipo settellites hutuma taarifa hizo kwenye gps map ya ramani ya dunia na kueleza kifaa flani kipo longitudes na latitudes kadhaa katika uso wa dunia.

Fahamu kuwa kila kifaa cha GPS RECEIVER huwa na utambulisho binafsi yaani IMEI number,kupitia utambulisho huu ni rahisi settellites kuepuka kuchanganya taarifa za receiver moja na nyingine.

GPS RECEIVER haihitaji internet kuwasiliana na GPS SETTELLITES.

VIFAA AMBAVYO NI GPS RECEIVER

1. GPS RECEIVER STAND ALONE DEVICES. Hivi ni vifaa maalumu kwa ajili ya kupata taarifa za GPS pamoja na picha,sauti,vifaa hivi huwa na size tofauti tofauti,kuanzia saizi ya kiberiti na kuendelea.

Vifaa hivi ndivyo mara nyingi hupandikizwa katika vitu mbalimbali ili kifaa hicho kikiibiwa au kikipotea iwe rahisi kukipata. Mfano unaweza kukipandikiza kifaa hiki katika gari,pikipiki au kitu chochote ambacho unahisi kikipotea kitakupa kazi kukipata.

Kupitia gps receiver ndiyo utaweza kupata kitu ulicho poteza,kwa kutafuta taarifa za gps receiver uliyo ipandikiza kwenye kifaa chako,kwamba kifaa cha gps receiver chenye IMEI No.....,kipo eneo gani?,settellites zitakwambia kifaa hicho kipo eneo flani kwa kukupa longitudes na latitudes za pale kifaa kilipo.

Hata kama kifaa hicho kilichopandikizwa gps receiver kitakua kipo katika mwendo mfano kipo kwenye gari,au kuna mtu anatembea nacho bado settellites zitakwambia kifaa hicho kipo wapi,na kipo katika mwendo kiasi gani!

Hivyo itakua rahisi kwako kuipata gps receiver yako,maana yake pia utakua umepata kifaa ambacho kilipandikizwa gps hiyo,iwe gari,bodaboda n.k.

GPS receiver zinatumia battery,hivyo ni lazima battery iwe na chaji kuwezesha kifaa hiki kufanya kazi.

GPS receiver za kisasa nyingi zinatumia SIM card,na pia zinakuwa installed na Operating system mfano android OS au iOS,pia zimawekwa kamera,WiFi n.k.

Kuwekwa kwa SIM card na kutumia OS katika GPS device,kunaiongezea uwezo GPS device kutumia tekinolojia ya GPRS.

IFAHAMU GPRS NA JINSI INAVYO ONGEZA UFANISI WA KIFAA CHA GPS.

GPRS ni mawasiliano ya jumla ya radio na ya kidata ya mitandao ya simu,hii inajumuisha 2G,3G,4G na sasa 5G.

Kifaa cha GPS ili kiwe na uwezo wa GPRS,ni lazima kiwe kinatumia SIM card, GPRS inasaidia kutuma taarifa
za mawasiliano yaliopo kati ya GPS RECEIVER, na GPRS SETTELLITE kwenda katika saver (vifaa vinavyotunza kumbukumbu kwa ajili ya kusomwa na matumizi mengine) taarifa hizi hutumwa kwa tekinolojia ya GPRS (Data and Radio)

Pia GPRS inasaidia GPS RECEIVER oparators kuwasiliana na kifaa hicho mfano kutuma "commands" mbalimbali katika kifaa hicho,mfano kukiamrisha kifaa kupiga picha,kurekodi video au sauti sehemu kilipo n.k,oparator anaweza kutuma hizo command kwenda kwenye kifaa bila kujali umbali uliopo kati yake na kifaa hicho,anaweza kukiamrisha kifaa icho kufanya tendo flani hata kama oparator na kifaa wapo mabala mawili tofauti.

Ufanikishaji wa kutumwa,kupokelewa na kufanyiwa kazi kwa command zotezote,kunafanikishwa na mawasiliano ya GPRS na Operating system (OS) iliyokuwa installed katika GPS receiver.

GPS receiver za kisasa zimekuwa smart zaidi ambapo zinaweza kupiga picha,kurekodi video,kurekodi sauti,n.k.

2. VIFAA VYA GPS VILIVYO PANDIKIZWA KATIKA VIFAA VYA KIELECTRONICS

GPS device nyingine zimepandikiza katika vifaa mbalimbali vya kielectronics hapa nitazungumzia simu za kiganjani hasa smartphone.

Je?Wajua kama simu yako ya kisasa ya smartphone imepandikizwa kifaa cha gps receiver ndani yake?Na kwamba inaweza kufanya karibia matendo yote yanayoweza kufanywa na STAND ALONE GPS RECEIVER?

Jibu ni ndiyo!Simu nyingi za kisasa zimepandikiza gps receiver na zina uwezo sawa na maelezo ya stand alone gps device ya hapo juu,mtumiaji wa simu ana uwezo wa kuwasha au kuzima GPS ya kwenye simu yake kupitia menyu ya simu yake.

CELL TOWER TRIANGULATION

Hii ni teknolojia ambayo inasaidia kujua kifaa chenye GPRS teknoloji (mfano gps device au simu ya mkononi) kipo katika eneo gani kwa kutumia minala ya simu,minala ya simu huweza kutambua eneo na umbali ambao kifaa kipo kwa kupima nguvu ya mawimbi kutoka kwa mnala na kifaa hicho.

Kama kifaa ambacho kipo ktk target kitakuwa katika eneo lenye minala ya simu miwili uwezekano wa kujua kifaa kipo katika eneo gani huongezeka,ingawa uwezo huwa mkubwa wa kujua kifaa kilipo kama kitakua jirani ya minara 3 na zaidi.

WiFi LOCATOR
Hii husaidia kutambua kifaa chenye gps receiver kipo eneo gani kulingana na kifaa hicho kinavyozi tafuta na kuzipata WiFi za eneo husika kadri kinavyohama kutoka katika sehemu moja kwenda nyingine.

Mfano ukiwa na simu yamkononi yenye WiFi,na ukawasha WiFi yako kawaida simu itatafuta router zinazo rusha mawasiliano ya WiFi ya eneo husika,kwa kifaa cha GPS RECEIVER iwe simu au stand alone gps device hutuma taarifa hizo katika saver hivyo GPS oparators watajua kifaa kipo eneo gani ili mradi oparators wawe na mawasiliano na GPS device hyo.

JINSI NJIA HIZI NNE ZINAVYOTUMIKA KWA PAMOJA KUIPATA GARI AU PIKIPIKI VILIVYO IBIWA

Gari,au pikipiki ikiibiwa oparator ataanza kuwasiliana na kifaa cha gps kilichopandikizwa ktk gari,au bodaboda hiyo.

Maeneo ya wazi GPS teknoloji ndiyo hutumika kujua gari au pikipiki ipo wapi,inatembea au imesimama,na kama inatembea je ni speed kiasi gani?

Aliyeiba anaweza kwenda kupaki gari au bodaboda eneo ambalo limejificha mfano katika nyumba au jengo,maeneo kama haya GPS teknoloji hushindwa kufanya kazi sababu ili gps ifanye kazi inatakiwa kuwe na anga lililo huru kati ya gps receiver na gps settellites.

Oparator atajua hali hii kwamba mwizi kaingia na gari au pikipiki katika jengo kwa mafunzo waliyonayo atawasha mfumo wa pili wa WiFi LOCATOR.

Kifaa kilichopandikizwa katika gari au pikipiki hiyo iliyo ibiwa kita tafuta WiFi zote zinazopatikana eneo hilo ambapo mwizi amepaki gari au bodaboda aliyo iba.

Oparator atazisoma na kama kati ya hizo searched wifi ni za router znazo fahamika,oparator atajua eneo ambalo mwizi amepaki gari au pikipiki a,hivyo taarifa za mwanzo za gps,na hizi za wifi zitazidi kupata ushahidi gari au pikipiki ipo wapi.

Panapo ulazima oparator atawasiliana na polisi ili kuweza kupata kibali cha watu wa mitandao hasa ambao umeweka SIM card yao ili wafanye CELL TOWER TRIANGULATION.

Oparator wa mitandao ya simu kitengo cha uharifu atawasiliana na oparator wa kifaa cha gps kwa kumtaka oparator wa gps afanye command kadhaa zitakazo saidia kifaa kufanya data au radio (gprs) communication na tower zilizo jirani.

Baada ya command kadhaa,oparator wa mitandao ya simu atajua kifaa chenye IMEI namba flani kipo eneo gani na taarifa hizo zitakusanywa na zile za mwanzo.

Baada ya kujiridhisha oparator wa gps device,atawapa polisi ushirikiano kuwaelekeza sehemu ambapo ameona gari,au pikipiki ipo!

Polisi nao watajiridhisha kwa kutumia vifaa vyao na taarifa hizo,wakilidhka wataenda kuvamia eneo husika.

Kwa magari yaliyo ibiwa,ni rahisi kuepuka mhalifu kukimbia na gari umbali mrefu,GPRS hutumika kutuma command kwenye kifaa ambapo kifaa kitalizima gari na kulizuia kuwaka.

JINSI WEWE MWENYEWE UNAVYO WEZA KUFUNGA GPS SYSTEM KWENYE GARI AU PIKIPIKI YAKO.

1. Inatakiwa uwe na kifaa cha GPS (unaweza kununua stand alone gps device au ukatumia simu yako kama gps device).

2. Fahamu ktk kifaa chako lazima ufanye installation ya software ambayo itakusaidia kuwasiliana na kifaa hicho ukiwa mbali nacho

Kuna software nying za bure ambazo unaweza kuinstall katika kifaa chako cha gps mfano simu yenye gps au gps device yako kwa ajili ya kufanya tracking,ya gari yako au bodaboda,mfano software iitwayo "Traccar Client"

3. Ukisha install software hii,tafuta kampuni ambazo zinatoa huduma ya bure ya saver "free gps saver",ambao wanasaport traccar client au software yoyote uliyo weka.Kisha unganisha hiyo device yako na saver hiyo.

Kwa watakao tumia simu kama gps device,simu ambayo unataka kuitumia kama gps device haita tumika tena kwa matumiz mengine ichukue simu hiyo kisha kaifiche kwenye gari lako sehemu ambayo si rahisi kuonekana.

3. Hakikisha,umewasha GPS yake,WiFi,na data yaan GPRS, na pia hakikisha line uliyoweka ina internet bundle ya kutosha,hata GB 2 siyo mbaya.

4. Hakikisha simu hyo inawasiliana na saver vizuri hata kabla ya kuificha.

5. Baada ya hapo unahitaji simu nyingine au kompyuta ambayo inauwezo wa internet ambayo utaitumia kuingilia katika website ya saver uliyojisajili kupata taarifa za gps yako (simu ile uliyo ficha au gps device).

Kupitia website hii ndo utaweza kufanya commands,kuona gari au bodaboda yako iko wapi,route ilizofanya n.k

*kwa watakaotumia stand alone gps device hatua ndo hzo hzo.

FAIDA ZA KUFUNGA TRACKING KATIKA GARI AU BODA BODA.
*Mfumo utasaidia kukipata chombo chako kikiibiwa.

*Mfumo utakusaidia kujua mizunguko yote ambayo chombo chako kimefanya kwa siku au mwezi.

*Utaweza kukizima chombo chako hata ukiwa mbali nacho na mtu mwingne hataweza kuwasha.

*Utaweza kufatilia safari zote za chombo chako.

*Utajua chombo chako kipo wapi,speed kinayotembea

*Unaweza kurekodi sauti,video au ukapiga picha eneo ambalo chombo chako kipo hata kama wewe ukiwa mbali,hvyo utajua nn kinaendelea.

*Na mambo mengine mengi.

Unaweza kupata huduma hii bila gharama na ukaisimamia wewe mwenyewe kama nilivyo eleza hapo juu.

lakini kwa ufanisi mzuri zaidi wa huduma hii unaweza kujiunga na kampuni zinazofanya kazi hii kwa malipo,kwasababu

1. Taarifa za tracking huhitaji saver kubwa yenye speed ya kutosha,ambayo huwezi kuipata katika huduma ya bure.

2. Tracking hufanywa na mtaalamu wa kusimamia na kuviongoza vifaa hivi,wakati wa kawaida na wakati wa dharula,ambae anajua atumie command gani na kwa wakati gani.

3.Japo simu yenye gps au kifaa cha Gps kinaweza kufungwa na kukupa taarifa,mfumo huu kuwa thabiti hufungwa na vifaa vingne,kama vile power supply,charging system,power bank,sensor controls n.k,ambavyo humuhitaji mtaalamu

4.Mifumo ya kimawasiliano huhitaji wataalamu ambao wanaweza kurahisisha utendekaji wa jambo flani kwa wakati.

Kwa mtu atakaye hitaji huduma ya tracking kwa ajili ya gari,bodaboda n.k

Wasiliana nasi 0629068815

Au fika ktk ofisi zetu zilizopo machinga complex

Pia unaweza kusoma kuhusu gharama zetu Hapa.fahamu "route" za gari yako ya biashara - JamiiForums
 
Nashukuru sana kwa elimu hii. Mie nimenunua gari (used from Beforward) kuna makorokoro mengi sana ndani yake nahisi na hayo ma-GPRS Receiver yapo pia ngoja nikacheki vizuri nione kama itaweza kuwa na msaada siku gari ikiibiwa.
 
... thanks a lot! Ila ni vizuri pia ku-acknowledge kwamba hayo masatelaiti zaidi ya 30 yako huko angani kwa teknolojia ya Kimarekani na Jews. Kila mtu anafaidika nayo bure kabisa kuanzia Iran kule hadi Mchambawima. Hii ni katika kuweka tu rekodi sawasawa maana habari ilivyokaa wengine wanaweza kudhani yalikuwemo huko tangu uumbaji! Hapana, ni brains zimetumika! Itutie hamasa na sisi kufikia level hizo.
Cc: kimsboy
 
Back
Top Bottom