Jinsi Serikali inavyotakiwa kudhibiti mfumuko wa bei

msigazi

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
456
330
JF nawasalimia kupitia jina la jamhuri,

Nachukua nafasi hii kuleta nasaha zangu kwenu ikiwezekana serikali izipate.

Kuna jambo ambalo nimewaza ni kwanini vitu huwa vinapanda bei bila mpangilio nikagundua kuwa kuna shida kwenye wasimamizi wa bishara.

Kwenye wizara ya viwanda inatakiwa ipitie upya ufuatiliaji wa bidhaa kama wanavyofanya kwenye bidhaa bandia wanatakiwa waangalie hasa masoko.

Natoa mfano
Sukari ya kagera sugar inazalishwa Kagera ajabu ni kuwa bei ya sukari kwa mikoa ya kanda ya ziwa ni bei juu sababu inayosababisha ni kusafirishwa mara mbili. Kupelekwa Dar kwa ajili ya uchapishaji wa TBS nk.

Kwanini wasije moja kwa moja kiwandani wakaweka hizo TBS zao? Na kitu kingine vifaa vya ujenzi viko bei juu mno. Dar unaweza kukuta mfuko wa siment Tsh. 15,000/= lakini huku mikoani tunalia bei ziko juu mno nondo siment na vifaa vyote vya ujenzi.

Kama kuna kitu ambacho serikali wanajisahau ni kuwaachia wawekezaji kupanga bei za vitu. Bila serikali kuweka bei elekezi hasa upande wa vifaa vya ujenzi, mafuta ya kula, sukari nk.

Naiomba serikali iliangalie suala hili kwa jicho la tatu.

Asante.
 
Tupo katika mfumonwa kibepari bei huamuliwa na soko sio serikali, Tukianza kuleta bei elekezi hapa ndo tutaporudi kufunga mpaka ili mahindi yasiende nch nyingine ili hio bei elekezi itimie
 
Tupo katika mfumonwa kibepari bei huamuliwa na soko sio serikali, Tukianza kuleta bei elekezi hapa ndo tutaporudi kufunga mpaka ili mahindi yasiende nch nyingine ili hio bei elekezi itimie
Kwa hiyo mkuu ni halali mahindi yauzwe debe Tsh 5,000/=
Ilihali mfuko mmoja wa siment Tsh 22,000/=?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo mkuu ni halali mahindi yauzwe debe Tsh 5,000/=
Ilihali mfuko mmoja wa siment Tsh 22,000/=?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa mkuu mahindi na cement vinaingilianaje ?
Mana kila kitu kina bussness model yake na cost of production pia zinatofautiana ko its possible and fair mahind yakauzwa buku debe na cement ikauzwa laki mfuko
 
Pamoja Na hayo petroli imepanda, bila shaka vitu vitazidi kupanda maana hatukai viwandani lazima visafirishwe.
 
Back
Top Bottom