Jinsi serikali inavyochangia kuzidisha umasikini wetu watanzania

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,000
Nimependa uchambuzi huu uliofanywa na Mkuu Ngongo


a. Tanzania ina export kwa wingi dhahabu lakini utashangaa hakuna uhusiano naustawi wa taifa kwa ujumla hii inasababishwa na aina ya mikataba ambayo taifaliliingia na makampuni ya nje kwaajili ya uchimbaji wa dhahabu.Nimewahi kusikiataifa linafaidika na kodi kama PAYE,SDL, Corporate Tax na Royality 3%tu.Ukienda kwa wenzetu Botswana utakuta serekali yao ni wabia wa migodi kituambacho Tanzania inakikosa.Sasa we fikiria mgodi xyz umeuza tons 150 za dhahabukwa mwaka unaambulia 3% mwekezaji anatafuna 97% !!!!!!.Kibaya zaidi mwekazajini mgeni faida anayoipata anawekeza kwao wakija wataalamu wa uchumi wanakokotoahesabu pamoja na za mgeni tunaambiwa Tanzania tumeuza dhahabu tons 150 halafuunashangaa kwanini wananchi wengi hawana access ya maji,madawa,elimu....Naambiwa Mwl Nyerere alianzisha STAMICO pengine hawa wangekuwa wabia wa migodiyote ya dhahabu hata kwa 30% tu tungeshuhudia mabadiliko makubwa na mapatokatika sekta ya madini yangekuwa na mchango mkubwa.Unapotegemea SDL,PAYE kamamchango wa sekta ya madini tegemea matatizo makubwa.

b. Serekali inakosa nidhamu ya matumizi ya fedha na sera mahususi zinazolengakupunguza au kumaliza umasikini badala yake mara nyingi imejikuta ikianzishaprograms mbali mbali (MKURABITA.MKUKUTA....) ambayo zinatumia fedha nyingikatika utawala na kuwaacha walengwa wakuu (wanavijiji) bila msaada wamaana.Mfano unaweza kukuta mradi xyx ujenzi wa bwala la kuogesha mifugoumetengewa 500 milioni wataalamu wetu wananyofoa 300 milioni kwaajili yaununuzi wa gari la msimamizi wa mradi Land Cruiser VDJ,posho za safari,ukaguziwa mradi 50 milioni,semina elekezi 70 milioni,matengenezo ya magari 50 milionihapa bado sijaweka wizi mdogo mdogo utajakuta fedha zinazomfikia mlengwa nichini ya 15%.

c.Tanzania imekosa dira ya maendeleo ya muda mrefu na muda wa kati nchiinajiendeea yenyewe kusikojulikana.Najua watakuja watu na vitabu vilivyojaavumbi toka wizara mbali mbali.Ukweli ni kwamba sera nyingi zinatengenezwa nawataalamu wetu lakini zinabaki katika mawizara badala ya kupelekwa kwa wahusikaambao ni wananchi kwaajili ya utekelezaji.Uandaaji wa sera lazima ushirikishewananchi ngazi ya kaya kabla ya kutekelezwa.Matokeo yake ni huu umasikiniusiokwisha kila uchao.

d.Tanzania inapata fedha nyingi kutokana na mauzo ya bidhaa za nje lakini fedhahizo hazipelekwi katika maeneo yanayoweza kuondoa au kupunguza umasikini laukama zinapelekwa basi zinapelekwa kidogo sana.Fedha nyingi zinaelekezwa kamamatumizi ya kawaida ya uendeshaji wa serekali.Tunaweza kuongeza bidii kuuzamazao mbali nje ya nchi lakini serekali nayo inaongeza matumizi ambayoyangeweza kuepukwa.Mfano leo hakuna tofauti ya gari anayotumia Rais na mkuu wawilaya,RPC au wakurugenzi wa mashirika ya umma.Ebu fikiria Tanzania ina wilayangapi ?.Serekali imekuwa ikizalisha wilaya na mikoa kwa jinsi inavyotaka kwakisingizio eti inasogeza maendeleo kwa wananchi !.Wananchi masikini hawana hajana wakuu wa mikoa au wilaya wananchi wangependa kusogezewa huduma za afyakaribu na maeneo yao,wangependa kuhakikishiwa soko la uhakika la mazaoyao,wangependa kupata huduma ya maji karibu na maeneo yao na si madoido ya mkuuwa wilaya na L/C VDJ.


Mwisho nadhani
"outwardlooking strategies" ni nzuri lakini mapato yetu lazima yaelekezwe katika maeneoyenye kupunguza umasikini.Lazima taifa liwe na tafsiri moja ya umasikini na sikuwa na mipango mingiiiii progarms nyingi majina mengiiiiii.Tuwe na vipaumbelevichache tunavyoweza kuvisimamia na matokeo yake yakaonekana wazi pasipoghilipa za statistics za kuunga unga.Serekali ipunguze matumizi ya kawaidabadala yake ipeleke fedha nyingi katika matumizi ya maendeleo.

Uchambuzi huu ulikuwa nI majibu kwa thread hii hapa chini

https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/546729-uchumi-wa-tanzania-je-ni-kitendawili-au-ni-mazingaombwe-kwa-maskini.html
 

mwahaja

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
387
225
Kama leo sijala,na ni degree holder mtarajiwa,mbaya zaidi ni siku ya uhuru.Nini maana ya uhuru?kuna haja gani ya kujivunia uhuru? kama mie hivi vipi wengine wa chini zaidi yangu?NITAIPIGANIA CHADEMA DAIMA,KWA AKILI TIMAMU.Mungu nisaidie.
 

Misa

JF-Expert Member
Jul 5, 2013
839
195
Kama leo sijala,na ni degree holder mtarajiwa,mbaya zaidi ni siku ya uhuru.Nini maana ya uhuru?kuna haja gani ya kujivunia uhuru? kama mie hivi vipi wengine wa chini zaidi yangu?NITAIPIGANIA CHADEMA DAIMA,KWA AKILI TIMAMU.Mungu nisaidie.
Duh Pole sana mkuu hii nchi ni ya wachache tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom