Jinsi Rais Samia alivyowapiga chenga ya mwili wapiga kelele wa mitandaoni kwenye teuzi

Nafikiri kwa sasa ile mihemuko yako ya kutaka kutafuta mabadiliko nje ya chama tawala itakuwa imetulia kidogo. Kwa sababu huchelewi kuja na uzi mwingine tena hapa jukwaani na kuanza kumlalamikia tena.

Atakuwa kafarijika na uwepo bado wa Chalamila.
 
Naomba kutofautishiwa kwa nafasi ya mkuu wa mkoa wanaposama "amestaafu na mwingine muda wake umeisha"
 
Kufa kwa Covid tena kizembe ni ushujaa? Hakuna jizi lolote la kura linakufa kishujaa.

Wenzako kila siku wanaanzisha uzi kuwa mama anafanya maamuzi kufuata maoni ya mitandaoni. Kila anapogusa waovu wenzake na Magu, kilio ni kuwa mama anamsaliti dhalimu.
Huyu Veronica France ndo bingwa wa hizo nyuzi za kijinga jinga!
 
JINSI MAMA ALIVYOWAPIGA CHENGA YA MWILI WAPIGA KELELE WA MITANDAONI....

Baada ya Mama kutangaza kuwa angeteua hata wa upinzani kuitumikia serikali...vijana wa Chadema na ACT humu mitandaoni wakaanza kuota Ndoto za mchana..!!

Waliamini kuwa hao watakaoteuliwa toka upinzani basi watatoka vyama hivi vikubwa...Chadema na ACT Wazalendo..!!

Wakawa wanausubiria kwa hamu uteuzi huu wa Wakuu wa mikoa....na leo mama kalipua bomu...!!kamteua Mama Queen Sendiga kutoka chama kidogo sana cha ADC kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa

Ni habari mbaya sana kwa wapinzani wetu hawa wa mitandaoni..ambao jana tu walikua wakishangilia kutenguliwa kwa DC Sabaya

Kwanza Walianza kumshinikiza Mama avunje baraza mawaziri ili awateme mawaziri wote walioteuliwa na JPM.Mama hakuwasikiliza..!!

Wakahamia kwa Wakuu wa Mikoa...wakaanza kumshinikiza tena Mama awapige chini Wakuu wa mikoa wote walioteuliwa na JPM..wakidai walikua wakiendesha hiyo mikoa kwa mihemko na mashinikizo kutoka kwa JPM

Mama leo kawaonesha wapinzani wetu kuwa Yeye na JPM ni kitu kimoja...kaamua kufanya kazi na wakuu wa mikoa karibia wengi wa JPM.

Ali Happi na Chalamila ndio wakuu wa mikoa wakiosubiriwa kwa hamu na wapinzani watenguliwe...haijawa hivyo,Mama kawahamisha mikoa waendelee kuwatumikia wananchi...

Huyu ndiye Mama tunayemfahamu...anang'ata huku akipuliza..!!!
Heeeeee... Imeshaanza tena kumsifia mtu uliyeshinda week nzima ukimwanzishia nyuzi za kumponda
 
Kufa kwa Covid tena kizembe ni ushujaa? Hakuna jizi lolote la kura linakufa kishujaa.

Wenzako kila siku wanaanzisha uzi kuwa mama anafanya maamuzi kufuata maoni ya mitandaoni. Kila anapogusa waovu wenzake na Magu, kilio ni kuwa mama anamsaliti dhalimu.
Una uhakika ni Covid? Au unahara prapraaaaaaa
 
Back
Top Bottom