Jinsi pombe inavyoathiri chembe chembe za DNA yako na kukupa hamu ya kunywa zaidi

Feb 18, 2019
8
45
Utafiti umeonyesha kuwa imani za zamani kwamba glasi moja ya mvinyo wakati wa chakula ni muhimu ni potofu.

Unywaji wa pombe kupitia kiasi sio mzuri kwa afya yako kitu kilichothibitishwa kisayansi miaka kadhaa iliopita.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni , utafiti umeonyesha kuwa imani za zamani kwamba glasi moja ya mvinyo wakati wa chakula ni muhimu ni potofu.

Tukiongezea athari za unyawaji wa pombe zinazidi kujulikana.

Na sasa kundi moja la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani pamoja na watafiti kutoka chuo cha Yale nchini Marekani wamegundua kwamba unywaji wa pombe unaweza kuathiri chembechembe zetu za DNA na kutufanya tuhisi kutaka kubugia pombe zaidi.

Wengi pia wanahoji kwamba kinywaji kimoja kina athari mbaya kwa afya yetu.

Ukinywa unazidi kuwa na hamu ya kuendelea.

Kufikia hapo kundi hilo la watafiti liliamua kuangazia uchanganuzi wake katika jeni mbili zinazohusiana na kudhibiti tabia wakati tunapokuwa chini ya shinikizo la pombe.

Moja ni ile ya PER2 inayoshawishi maisha ya miili yetu na nyengine ya POMC, ambayo inadhibiti utaratibu wetu wa kukabiliana na dhiki.

Ukilinganisha wanywaji wa kadri na wale wanaobugia pombe kwa wingi, wanasayansi wamegundua kwamba jeni za watu wanaokunywa pombe kwa wingi hubadilika.

Kwa wale wanaobugia kwa wingi, jeni zao hutoa protini polepole na hupata hamu ya kunywa wakati wanapokumbwa na matatizo

Kwa nini watu hupendelea kunywa ili kukabiliana na matatizo?

Mabadiliko ya jeni huongezeka kutokana na vinywaji zaidi.

Unapobugia pombe zaidi unazidi kuharibu jeni hatua inayotufanya kuwa na hamu ya kunywa pombe zaidi na zaidi.

"Tumegudua kwamba watu wanaokunywa pombe nyingi wanabadilisha chembechembe zao za DNA katika njia inayowafanya kutaka kunywa zaidi'', alisema Profesa Dipak K Sarkar, mwanzilishi wa utafiti huo unoaongozwa na chuo kikuu cha Rutgers.

"Hii inaweza kusaidia kuthibitisha kwa nini pombe ina mvuto mkubwa'', aliongezea

Watafiti wanatumai kwamba ugunduzi wao utawaruhusu kutambua viashiria vinavyoweza kupimwa kama vile protini au jeni zilizobadilishwa kutabiri hatari ya mtu anayekuwa na unyawaji wa kiwango cha juu mna vile atavyolindwa asiweze kunywa zaidi.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
49,077
2,000
Hata chakula ululate sana ni hatari kwa afya yako, we should do things in moderation other wise life will be boring.
 

King Ngwaba

JF-Expert Member
May 15, 2016
15,955
2,000
Pombe sio Gamma-rays haiathiri wala kubadilisha DNA ya mtu tuache kudanganya.

Tukubali tu kuwa pombe sio nzuri kwa Mwanadamu kama ukinywa kidogo au kupita kiasi itabakia kuwa ni mbaya tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom