Jinsi picha la kurudia chaguzi Tanzania linavyochezwa

Dive

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
868
1,424
Watanzania tutazame picha linalolechezwa la kuumalizia mbali upinzani. Ukiangalia wafuatao wamejiuzulu uanachama wao bila sababu mujarabu na chaguzi za wabunge na madiwani zimerudiwa. Akina Mwita Waitara wa jimbo la Ukonga, mbunge wa Monduli, mbunge wa Kinondoni, mbunge wa Liwale.

Hii inatupa picha kuwa hili picha limetengenezwa kwani hata mkuu wa nchi mwenyewe baba Jiwe hakemei chochote anaruhusu mamilioni ya pesa za walipa kodi yatumike kurudia chaguzi ili kukipa nguvu chama tawala.

Alitakiwa akemee ili mambo yaishe, lakini kwa kuwa ni upinzani anachekelea ingekuwa CCM wanahama huu mchezo ungeisha mara moja!! Tujiulize sote lengo hasa ni nini? Kwanini inakuwa hivi na haikuwa hivi kipindi cha nyuma?

Hii inafanyika ili kukiua chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Wale wanachama na viongozi waaminifu ndiyo wamebakia mifano akina Mwenyekiti Freeman Mbowe, Mchungaji Peter Msigwa, mbunge Joseph Mbilinyi, Mbunge Peter Lijuakali, mbunge Joseph Haule, mbunge Halima Mdee, mbunge Esther Bulaya, Mbunge Esther Matiko, mbunge John Heche, mbunge Tundu Antipas Lissu, mbunge John Mnyika na mbunge Saed Kubenea na wengine ambao sijawataja hapa.

Inafanyikaje? Njia kuu zinazotumika katika nyingi ni Mapandikizi na Kompromati. Kwa mapandikizi ni wanachama hawa kuingizwa katika vyama hivi vya upinzani mapema na kujenga kuaminika hadi kuweza kuingia kwenye vikao muhimu na kukusanya siri muhimu za vyama vya upinzani hasa CHADEMA. Halafu ndiyo sasa na muda unavyoenda wanarudi na kupewa madonge nono ya fedha.

Kompromati ni neno la kirusi (Russian) katika intelijensia ambapo mtu huhujumiwa (black mailing) na kupewa masharti kuwa usipofanya hivi tutaweka mambo yako wazi na tutakuchafua au tutafanya vile. Hapo hauna namna lazima usalimu amri na kuyasikiliza matakwa ya wanaokuhujumu.

Picha hili litavimaliza vyama vikuu vya upinzani kwani CUF tayari chali na CHADEMA ndiyo hivyo. Picha linaweza kwenda hadi kuundwa kwa vyama vingine vya ajabu ili kuonekana kuna upinzani. Kumbuka kikija chama chenye nguvu au upinzani wa kweli huwa vinahujumiwa si mnakumbuka Chama cha Jamii (CCJ) cha marehemu Samwel Sitta na Dr. Harrison Mwakyembe kilivyomalizwa kwenye hatua za usajili.

Hawa walijaribu kwa kumtoa kafara mbunge Fred Mpendazoe na viongozi akina Kiyabo. Ndiyo maana hao akina Kiyabo hatuwasikii tena kwenye siasa wapo kimyaa.

Vyama vinavyoongeza upinzani zaidi kama ACT Wazalendo hivyo vimepeta kwenye usajili ila vimekuja kumalizwa kwa kuwachukua viongozi wake na kupewa nyadhifa serikalini kama tulivyoona kwa Profesa Kitila Mkumbo na Mama Anna Mughwira.

Na katika chaguzi zote ndogo za kurudia ambazo wapinzani wanajirudisha CCM ni mwiko upinzani kushinda na Mkurugenzi na viongozi wengine ole wao washinde wapinzani. Kwa kweli demokrasia inaisha na wananchi wengi ambao hawajui chochote hasa vijijini wakiwa na uelewa mdogo hawana nafasi ya kuchagua viongozi kwa ubora wao hiyo 2020 bali watachagua chama.

Na tunaamini ili nchi iendelee tofauti ya mawazo au changamoto ndiyo inaendeleza nchi zetu hizi ambazo ustaarabu wetu bado. Serikali ikiwa haina upinzani wa kweli na wa nguvu inalala tu na kuzisababisha nchi zizidi kutopea kwenye umasikini uliokithiri. Hapo hakuna mawazo mbadala, hakuna kujiuliza, hakuna uoga wowote.

Sitegemei mtu aje abishe kwa kuleta mifano ya China sijui Korea na kwingine bila kujua wale walishapitia kwenye ustaarabu miaka mingi na hatua waliyofikia ni ya juu sana. Tena wameweka mifumo mizuri sana ambapo mafisadi wanashughulikiwa na utendaji bora wa kazi ndiyo utamaduni wa nchi zao.

Naamini demokrasia ikisimama ndipo tutaweza kusogea bila hivyo tutaendelea kujuta na vizazi vyetu vitabakia pale pale huku wenzetu wakisogea Mbele kwenye nyanja za kisiasa , kiuchumi, kiutamaduni na kisayansi.

Sasa wewe na mimi tutafanyaje? Viongozi wa vyama vyote CCM na upinzani wafanyaje? Hapo ndipo tujiongeze na kufikiria tutasogea vipi?

Sisimamii kwenye chama chochote cha kisiasa nasimama kwa Tanzania nzuri, bora, yenye mafanikio na yenye future inayopendeza kwani hiyo kesho hatutakuwepo ila wajukuu, vitukuu, vilembwe ,vilembwekeza na vining’ina wetu ndiyo wataikuta Tanzania hii ikiwa mbaya au nzuri.

TUTAFAKARI
 
Kuna ule msemo unaosema kama maisha magumu achana nayo ufanye mchongo mwingine. Leo ndio naelewa maana yake. Karibu ulimwenguni mkuu, kwenye nchi ya watu tusio jali.
 
Lakini na wapinzani wajiulize kwa sasa wana sera gani za kuvutia masikio ya wananchi?
Zamani walikuja na sera nzuri sana sijui kwa sasa wamekuaje?
Kwa mbano uliopo hizo sera za kuvutia masikio ya wananchi utazisikia wapi? Hakuna mikutano ya hadhara, vyombo vya habari vinadhibitiwa, mitandao inatungiwa sheria kali, kubambikiwa kesi kwa viongozi n.k. n.k. Kifupi tumerudi nyuma kwa hiyo maendeleo tutayasikia kwa wengine.
 
Uongozi wa kinafiki na undumilakuwili hauwezi kuleta maendeleo kamwe!..linalofuata ni anguko kubwa la kiuchumi lakini watakaoumia ni wananchi wa kipato cha chini!
 
Ninachokiona hapa kwa mara ya kwanza Magufuli kama Mwenyekiti anabomoa msingi mzuri uliowekwa na wenyeviti waliopita. Same story waliyoitumia CCM kipindi cha kampeni kuelezea mchakato wa upatikanaji wa Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya ukawa kuwa haukuzingatia katiba ndio ikasababisha wapiganaji wa ukweli kwenye siasa za upinzani kujiondoa (Slaa na Lipumba) ndivyo itakavyokuwa hatima ya CCM anayojenga Magufuli na wasaidizi wake. Wanapokewa watu toka upinzani ambao hawana utashi wa kweli zaidi ya maslahi ya matumbo yao na kuwaacha wanachama wao wa siku nyingi. Mchakato wa kuteua wagombea haufuati katiba yao ambayo inaeleza wanachama kupiga kura kumpata mgombea.

Cha kujiuliza hawa wapinzani wanaobomoa upinzani, je watakauwa na nafsi ya kuteuliwa tena mwaka 2020 kwenye chaguzi mkuu au watarudishwa kwa wanachama asili matawini wasurubiwe na watu wenye vinyongo? Inshort naona baadhi yao kupotea kwenye ulingo wa siasa mapema mno. Wengi watatumika kama Bazoka/Big G kisha watatupwa.
 
Back
Top Bottom