Jinsi Ole Sabaya atavyochomoka kwenye mikono dhalimu iliyombambikia kesi

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Kwanza mpaka sasa tuhuma alizopewa zina msukumo wa kisiasa zaidi na ni kisasi baada ya kupambana na wanasiasa dhalimu na wapiga madili'

Ushahidi dhidi ya tuhuma zake ni wa kutengeneza au kwa kimombo unaitwa fabricated. Mfano anadai kuporwa mil 90 atathibitisha vipi kirahisi mahakamani kuwa alipigwa biti ili amapatie Sabaya mil 90. Ilikuwa ni mazingira gani mpaka analazimishwa kwa nini hakufungua malalamiko polisi mpaka wanaharakati wa twita ndio wakaweka mbinyo?

Pia wanaodai kuwa waliteswa na kupigwa na Sabaya walikuwa wapi kufungua malalamiko polisi? Hakuna ushahidi wa wazi kuwa walimuona kwa macho yao akwatembezea mateso na kichapo zaidi ya Ansbert Ngurumo anayetumiwa na Chadema kupakaza hizi tuhuma.

Unyag'anyi wa kutumia siraha ni moja ya makosa makubwa kabisa. Jeshi la polisi lilikuwa wapi kumkamata mtuhumiwa maana alikuwa akihatarisha maisha ya watu.

My take: Chadema ni chama cha wakora na mafisadi ukipambana nao wakishindwa kukuua kama Chacha Wangwe wanakufanyia njama mbaya
 
Hakuna kitu kibaya kama kupambana na mtu asiye adui yako. CHADEMA inaingiaje katika ishu ya Sabaya?

Aliyeagiza uchunguzi ni Mwenyekiti wa CCM, aliyemsimamisha kazi ni mwenyekiti wa CCM, aliyemuhoji ni TAKUKURU, organ ya Serikali inayoongozwa na CCM, aliyemshtaki ni DPP aliyechaguliwa na mwenyekiti wa CCM sasa CHADEMA inaingia wapi hapa we jamaa.

Kipindi hiki mngetumia sala zenu na nguvu zenu kujisafisha kuliko kupambana na CHADEMA.
 
Watu kutokwenda Polisi kuripoti haina maana kwamba Sabaya hana kosa, hayo yote uliyoandika ni upuuzi tu, unatakiwa ujue watu walimuogopa kwasababu alikuwa analindwa na Magufuli, now Magufuli is gone, Sabaya is finished, kama unataka ushahidi usioacha shaka nenda Mahakamani kasikilize hiyo kesi kuanzia tarehe 18.06.
 
Ndio itajulikana sasa wapi alipotoa hizo silaha smg,pingu na bastola alizokuwa akitembea nazo,kama alipewa na OCD kisha wanagawana ndo atataja.

Uovu atende mwenyewe wanasiasa wanahusikaje sasa.Hizo kesi sita zote ngumu kuzipangua.We kama unamdai samehe tu huyo atoki kesho wala leo
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom