Chief asantee

Nisaidie hapa ...


Kwanza nilimpata mtu wa kunitengenezea website ambaye nilimlipa ila huwa ananichaji pesa kila mwaka akinidai ni hosting fee je ni kweli ?

Domain huwa inaexpire ?

Je naweza kuibadilisha domain ?
 
Chief asantee

Nisaidie hapa ...


Kwanza nilimpata mtu wa kunitengenezea website ambaye nilimlipa ila huwa ananichaji pesa kila mwaka akinidai ni hosting fee je ni kweli ?

Domain huwa inaexpire ?

Je naweza kuibadilisha domain ?
Ndio. Domain mara nyingi zinahitaji renewal kila mwaka.
Hosting pia inalipiwa every month or year.

Inategemea jamaa anakucharge bei gan maana kurenew domain sio bei kubwa (18,000 mpk 30,000 hvi)

Hosting ndio ina cost kidogo kulingana na space na features ulizochukua.
 
Chief asantee

Nisaidie hapa ...


Kwanza nilimpata mtu wa kunitengenezea website ambaye nilimlipa ila huwa ananichaji pesa kila mwaka akinidai ni hosting fee je ni kweli ?

Domain huwa inaexpire ?

Je naweza kuibadilisha domain ?

Uyo brother hapo juu racka98 amejibu vizuri kabisa swali lako.

Ila kuhusu kubadili Domain its Possible 100% .
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Ndio. Domain mara nyingi zinahitaji renewal kila mwaka.
Hosting pia inalipiwa every month or year.

Inategemea jamaa anakucharge bei gan maana kurenew domain sio bei kubwa (18,000 mpk 30,000 hvi)

Hosting ndio ina cost kidogo kulingana na space na features ulizochukua.
Shukran mkuu ...
 
Mkuu nina shida hapa, hv mm napenda kuwa na website ila sasa sijui nifanye nn ili niwez kuimilik
Njia yako nimeipend
Ila mm shida kuindesh site n changamoto kubwa kwangu
Sina base ya vitu vya kuwek
Je siwez pata auto site inajipost kwa mtindo huo
 
Mkuu nina shida hapa, hv mm napenda kuwa na website ila sasa sijui nifanye nn ili niwez kuimilik
Njia yako nimeipend
Ila mm shida kuindesh site n changamoto kubwa kwangu
Sina base ya vitu vya kuwek
Je siwez pata auto site inajipost kwa mtindo huo

Naomba untumie email hapa ( erickngimba@yahoo.com ) tafadhali. Tutaongea fresh.
 
Kwenye hii nakala nitakuonesha kwa ukamilifu kabisa jinsi ninavyoweza kutengeneza websites zenye mvuto (kama hiyo apo chini) bila ujuzi wowote wa lugha za kompuyta (programming languages) na pia ndani ya muda mfupi ( hata dk 10 ).

iNtMzzuwVGwmvmkjX6x22DuKGRueDoKmjQGhk3XIUAN0bhiqwUNAT6ziPFWfpbYojPHUMMSGuC6ReCa0L7j9Hm9d-8EaOSn4wE8iuV6x84CUf4HrgZkPd0RIsl8F6BrrBkVxACA7


Unaweza ukawa unajiuliza CODING NI NINI??... Kwa Ufupi Coding ni kitendo cha kutumia Lugha za Kompyuta ili kuunda kitu kitakachoifanya kompyuta iweze kukisoma, kuelewa na kutoa majibu… Naamini umepata picha kidogo.

Nmeamua kutoa nakala hii ili kuwasaidia watu ambao wanatamani kutengeneza website kwa ajili ya biashara zao lakini hawana bajeti ya kutosha ya kumlipa mtu awatengenezee na vile vle hawana ujuzi wa kutengeneza, lakini muda wanao.

Natumaini kabisa mpaka mwisho wa haya mafunzo utapata kitu hata kidogo.


Ngoja kwanza nikuandikie kwa ufupi hatua tutakazopitia kwenye hii nakala.
  1. Kununua Domain na Hosting
  2. Ku-install Wordpress
  3. Ku-install Plugins na Themes
  4. Ku-install Template
  5. Ku-upload taarifa zako
  6. Hitimisho


  1. KUNUNUA DOMAIN NA HOSTING
    1. DOMAIN
  • Kwa ufupi domain ni address ya website yako, inamaana kuwa watu wakitumia hiyo address (anwani) wataweza kuipata website yako moja kwa moja mtandaoni.
  • Nadhani unazifahamu domain sema tu, inawezekana labda ulikuwa hujajua kuwa zinaitwa domain, mfano wa domain ni kama; facebook.com, itv.co.tz, company.com, n.k unaweza ukachagua jina lolote lile kwa ajili ya domain yako na watu watakupata hapo.
  1. HOSTING
  • Ni mfumo unaowezesha domain yako iweze kuonekana mtandaoni na pia kuhakikisha kuwa hiyo domain imeunganika na website utakayoitengeneza.
  • Bila hosting website yako haitaweza kuonekana mtandaoni na bila domain pia hautaweza kupatwa na mtu yeyote mtandaoni. Hivyo basi domain na hosting ndiyo mihimili ya website na vyote 2 vinategemeana.
  1. JINSI YA KUNUNUA DOMAIN NA HOSTING
  • Kuna namna nyingi za kununua domain na hosting, kuna njia rahisi, ngumu, za gharama, za bei chee… Lakini zote zinautofauti kwenye utendaji kazi hasa hosting.
  • Hosting nyingi sana zinazouzwa na makampuni zinatofautiana viwango na ubora. Ila leo ntatumia hosting ambayo mimi mwenyewe naitumia na ninaikubali za sana.
  • Kwasababu, inafanya kazi vizuri yani ina kasi na usalama, gharama yake ni nafuu mno, na pia rahisi kuitumia, inaitwa INTERSERVER.


  1. Anza kwa kutembelea Website yao hapa Interserver.net na ubonyeze BUY NOW.

View attachment 1537641

  1. Andika Jina la Domain unalotaka, mfano “ Biashara.com” au “kampuniyangu.com”. Bonyeza Yes na Kisha bonyeza “Continue”
  • Kama wamekuletea ujumbe unaoonesha jina ulilolitumia limeshachukuliwa, basi jaribu jina lingine linaloendana na kile unachotaka.
3cGsjSrMWJjf-r5YExFcaYblsZbMgxxG53-1Q2itvQ4uCw8FZzSY37lSw8B028DEixFSVfa8mCnE3e3JL45qfpaf2fZL0DPrzhb10ZtZrwVJFGmhWzy7aci7BSRpW9WxkrDUFg0-


  1. Jaza Email na Password yako unayotaka.. Hakikisha unaikumbuka kwa sababu ndiyo utakayoitumia kuingia kwenye Ukumbi wako wa kutengenezea Website.
  • Bonyeza Kiboksi kukubali na Kisha bonyeza “Create Account and Continue”.

_ugXm-Wdx_Z222SsqUa8falDv2LAZ2iBJjm8pXCfH9TF9gKVGZ64iK8OfX1CiYfuXlhndNM0fXrZY6LC_nZpBT-uov-03dbaWAJcDVhWtJE3TWJ4Y_SH5BxaQk9iZel4Zsb3s67f


  1. Jaza Taarifa Kama Fomu ilivyouliza kisha Bonyeza “ Continue ”
pOe5IWmZkDxh7Tv09HMhEA4fwKBCCb4TiAmY_DmvOtYycJdI2rd2UaBvI6VsADDDxsqUnUhNmbzo15B0Y1TlHHcX_IXa6ZnCs0Hdq6CmCpr7YjFcEU0_Ugnec66YjFCftcfvtHH3


  1. Nenda kwenye “Billing Interval” hapo kama utahitaji Kupata Hosting kwa Mwaka Mzima na Uchague Miezi 12 (Watakupa Punguzo Zaidi).
  • Kisha Jaza Taarifa za Mastercard au Visa Card yako… Unaweza Ukatumia Airtel Mastercard au hata Vodacom Mastercard zinafanya kazi vema kabisa.
  • Bonyeza Hicho Kiboksi hapo chini kukubali, na kisha Bonyeza”Place Order”.
f4y-MIGotk5zAn_AizFWNghCdZ_upM8b9ZjgbJ52PKStfgsaI-qdwzcChkadiO2SbOW0oqC1eUWZbGPzUnWrKNHZwcoGIkBPmpWd5mlUby0uVS1jiMQniAPh8xPAfd6xpeblz0pw


  1. Mpaka Hapo Utakuwa umemaliza kabisa suala la Kupata Domain na Hosting. Utaletwa Moja kwa Moja kwenye Dashboard yako ya Interserver.
  • Kama hautapelekwa moja kwa moja kwenye Dashboard ya Interserve, tumia link hii kwenda moja kwa moja na uweke email na password yako uliyojisajilia.. “ my.intersever.net
MmsTv7l0Z_B3MY4Wo_rqz8uMlrS06-b1EgaV2DcH7Y8zECtBCxhuKZu_cyYhLXsQ0tKK43vVCF2O3oZQcVBwwoq0wyF14hUy7OF-qBXJtbmp0IkhzFnNPXQ-0M74h7hsjoN6BgmQ


2. KU-INSTALL WORDPRESS.
  • Wordpress ni Kampuni Kubwa inayotoa uwanja wa kutengeneza websites kwa watu wote, uwe unajua au hujui, maana wameitengeneza hii wordpress kwa mfumo ambao ni rahisi kutumika kutengeneza websites bila kutumia lugha za kompyuta.
  • Kwa hiyo kwa watu kama mimi na wewe itakuwa rahisi kwetu kufanya ubunifu wetu bila kufungwa na ujuzi wowote mgumu.
  • So, tunahitaji ku-install hii application ya wordpress ili kuanza kazi.

  1. Kwenye Dashboard yako ya Interserver hapo bonyeza Link ya website yako hapo chini ya Hosting.

7DswTKZbBdEvbnBfP8I9578H1Qd0BoyUFNuSUCzcj3WgJt3_juQp7Zhw2-rw_H9ZRQd4QtYkUh4yNqeDKjCqd5QEPDva-EO_Nulbwl1Vbng_tL-DniWRa1wZyZKipwmO73gb-sy8


  1. Bonyeza “Login to Cpanel”
n8E8bWHbTBab7jumwrhC0Wxxw7rwRm_GYO6tLpvtkA0UQAmc4Ge8UvmxL2P-P5zMM0bUGtn9kgdGEsDAIi9cGb9UWkOdwuHWmnJ79QzuRo-30GyLnn-GC1MaemX9RJK_sbM--jAo

  1. Ukishafika kwenye CPanel, andika kwenye hiyo nafasi hapo juu neno “ Soft”, kisha angalia chini na Ubonyeze ilipo “Wordpress” hapo.
VF0ZrRhiFwB5A_r9KtbAV60T81Vzv_0cKDIlFGhcbnbB1Iy0uc3BtbDNOBRQGPyx36HaC0MJKHL2T_MotvMLP091ejyFTzssj-KkRhygnDEI66HaBK2VR-TSN4ldpLj1bkTIOOvz


  1. Kisha Bonyeza “Install Now”


pOFmGuqwouDxcQ833yRXWc3a47JDoLxHBtGtis8NVRFuKd0MJ5OJX_vckFPaAeEYU0iKRcSJxvuXZMSrfWAONl5flw538BbHFwtwuBCJI8p2t3NwJ2BdLbiDX5tTBku4tdHnojFH


  1. Jaza Taarifa vile utakavyo kisha Bonyeza “ Install “
  • Hakikisha!! Unafuta hapo palipoandikwa WP, juu hapo mbele ya Domain yako kwenye huu ukurasa.
fQrCeseK99Rxj2tksQFhIfaJhTE0OtOho5oYuMorRMoVYmctHp7QmyVaD-3WctQupcZCYpVKx_dWETJwZn9NFOCeMDah1OyyW5vr3sZLKdyDRwrfzQ7Qiopr3kwuYjkxzGQkwGXx


  1. Ikimaliza ku-istall, itakuleta kwenye ukurasa ambao, utapewa maelekezo ya kuingia kwenye app ya wordpress,
  • Tumia hiyo iloandikwa “ adminstrative Url ” ili kuingia kwenye Dashboard yako ya Wordpress. Yangu ni hiyo… yako itakuwa tofauti, ila lazima iishie na maneno “ wp-admin” na ianze na Domain yako.

2cjzHJKrb5OicRTdVW6IeM7hDT7Bo9Xs8lY6RveWssZNAQIyDJz1YPPq_8du_j0geNy8ObE5jfpARyaV-ZDDk_g9pZR-cij5apd4zMbDDKi_KYIeZnjn3PTk2ci4PhjxEDbIHHNb


  1. Mpaka Hapo utakuwa umemaliza Ku-install Wordpress kwenye Account yako.
  • HAKIKISHA: Umeandika Pembeni Taarifa za “ USername na Password” unazopewa katika ukurasa utakaotokea baada ya hatua ilopita.
  • Kisha Bonyeza “ Login to Wordpress” ili kuanza ujenzi na utatumia hiyo “Username na Password” Kuingia kwenye account yako ya Wordpress.

  1. Utakapo ingia kwenye account yako ya wordpress Utaletwa Kwenye Dashboard yako ya Wordpress.

GpHI_KWyAtPmlBMW0m_tAMEHNH7-AbQDKKrcxm9l5x-mK2ewVTuaLA4G1zpRS62HuMaPYeyTi1UYF-4w8VM1d_ybh1-k-hVB6NY0Ked3Woiw1Ijts_KcPnZGeCuHu3E6iNScZwVi







3. KU-INSTALL PLUGINS NA THEME.
  • Plugins ni application ndogo ndogo zinazosaidia kuboresha shughuli unazozifanya kwenye website yako.
  • Theme ni application inayosaidia kuweka Muonekano wa ujumla wa website yako.
  • So, Tuta-install plugins Mbili (2) na Theme (1). Ambazo zitafanya Muonekano wa website yetu uwe mzuri na wa kuvutia.

  1. Ku-install Theme:
  • Kwenye Dashboard yako ya wordpress bonyeza sehemu iliyoandikwa “Appearance”
  • Kisha Bonyeza “Add New”

JkambO62rtJXvMgDguWyFHqPcEhVHZvg47lFenKiz9sdGb4X9ztwrpQaQjLXCgg3WKmdTJcMrgm5RQubm-G6-9ZwXKzrdxBQH3G-Vf4MMIl-41J6VMRcAvV1Z4FBlJWouoz7YsoT


  • Nenda Sehemu iliyoandikwa “ Search Themes…” na uandike “ Astra “ .. Utaona zimetokea “Themes” kadhaa kwa Chini, Ila Bonyeza “ Install” kwenye Iyo ambayo imeandikwa “ Astra” na siyo “ Astral “.
  • Subiri mpaka litokee neno limeandikwa “ Activate” na kisha Bonyeza tena hapo hapo na utakuwa umemaliza kuistall theme.

pFiOvN_KntFHtNnlDZ2oQlm3UwUPg3ZOr1ZCfvRkpSvCIO2OmRmRhPSMr0o3Uly076Pql4elqTO1Bm24ZBu4292pOnxcxzarmmTvZSB1uSQvC0Xm24iZZTGs5qtPvOZp1XvJPTvD


  1. Ku-install Plugins.
  • Utaratibu wake ni kama tu ule ule unapo install theme, ila hapa tuta-install zaidi ya kitu kimoja, yani Plugins.
  • Tuta-install plugins Mbili tu.
  • Tutanza hivii… Kwenye Dashboard yako ya wordpress bonyeza sehemu iliyoandikwa “Plugins”
  • Kisha Bonyeza “Add New”

Kg0K_3wYPn8csxEaQhw7uCs8Adqq84jhkWz1-4NC86lnWj1bq3sTWXfqbELZR4KOzj1Itqb7XjNvP5z7XRDd6SPhJENiE2DJCc--f5ue1oL6ESWl8WUzvmAcjVhzhCQcejHn7Ih6



  • Nenda Sehemu iliyoandikwa “ Search Plugins…” na uandike “ Elementor“ .. Utaona zimetokea “Plugins” kadhaa kwa Chini, Ila Bonyeza “ Install” kwenye Iyo ambayo imeandikwa “ Elementor ” tu.
  • Subiri mpaka litokee neno limeandikwa “ Activate” na kisha Bonyeza tena hapo hapo na utakuwa umemaliza kuistall Plugin.

VwrwiNbVv9Qp1RTPPUABBaEGgBumHCCO_jXe59maOSXyB4wMzGBUseHQYwgxPygxJROPlo6s665HK6tkUvrVfDaJR9RMT5udsG49ZztSykBvaqnp1oxyfu9eq2vVVEHzzEWb8_Hk



  • Nilikuambia kuwa tunatakiwa ku-install Plugins Mbili sasa Utarudia tena Kwa Kuanza kwenda kwenye Plugins => Add New => Search Plugins.. Kama kawaida na safari hii utaandika “ Starter Templates”. Kisha Chagua iyo ambayo imeandikwa “ Starter Templates” tu. Mara nyingi inakuwaga ya kwanza kabisa.
  • Tutakuwa Tumemaliza Kazi ya Ku-install plugins zetu mbili.

kgRVfxv5V8TnzHA7qLuSdbxBKFCEVrN20ef2eN5hVSKcDYj6evxj1uxtE5FETB8HV9EupQkNMhZat6PliQhtNT3Deds7DmhJ8-LzqS4KyZdRaSkyTwqQcRHCISzjhWO_9TaORTIe



SAMAHANI: Kwasababu JF wanaruhusu kuweka mwisho picha 20 kwenye Post moja na mimi nimetumia zaidi ya picha 35, kwa hiyo post imeshindwa kukamilika hapa ...

Nilivyoona hilo tatizo nikaamua niiweke Nakala hii kwenye Website ili kila mtu aweze kupata kitu kilichokamilika. Website ambayo nimeiweka hiyo Post yote Mwanzo - Mwisho , ni Hii: Jinsi ya Kutengeneza Websites

Naamini Utaelewa vema kabisa, ila kama utakuwa na Swali Lolote au unahitaji msaada zaidi.

MAWASILIANO YANGU:
Email: hello@erickngimba.tech
Simu: 0777 906 987
Website: www.erickngimba.tech
Yote Mema.
Well quoted
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom