Jinsi ninavyobaguliwa na Watanzania wenzangu Tanzania

Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
6,677
9,035
Wandungu mambo vipi civilians wenzangu?

Jana kuna jambo lilinitokea nkachukulia kawaida. I did not think it through, lakini baada ya kutulia na kuwasha flashback nikapata picha halisi.

In short jana nilienda pale Rock Garden Mwanza kuulizia bei ya boti kwenda Sanane island, sasa pale kuingia kwenye kigarden wameweka bango kiingilio ni Tsh1000/= ingawa hakuna uzio.

Lakini ile nafika kabla ya kuingia nikaona wazungu wawili wa kike wakiingia nao pia walikuwa wanaulizia boat, waliingia pale na kuanza kaongea direct na wahusika kwa muda wa kama dakika 15. Mimi nikawa nimesimama pale nje ya garden nasubiria wamalize wazungu na mimi niulizie.

Walipomaliza wazungu wakaondoka na mimi nikaingia kuulizia, ile naingia nikawaita wahusika na kuanza kuelezea shida kuwa sijaja kujivinjari hapa garden bali nina shida ya kukodi boat, waliniangalia juu chini halafu wakasema tafadhali tunakuomba usimame kwa nje kwakuwa hujalipia kiingilio, bila hiyana nikatoka nje na kumuita tuongelee kwa nje.

Tukaongea na kisha nikaondoka. Kwa kweli ile situation nilichukulia kawaida lakini leo nimekaa nikawaza na kukumbuka wale wazungu hawakulipa lakini waliingia direct na kuulizia mle ndani kama dakika 15 nzima bila kulipishwa.

Nikagundua na kuunganisha matukio ya zamani kuwa hizi sehemu za starehe, utalii, mabenki au mahotel makubwa huwa kuna ubaguzi wa chini chini na wabongo walioajiriwa pale.

Unakuta ukiingia hotelini au sehem ya Starehe kama ni mbongo walinzi wanakufuata na kukuuliza mara mbili mbili kama vile umepotea lakini wazungu wakija wanapokelewa kwa karibu nyingi kama kwao vile.

Inaniuma sana hapa Tanzania wote weusi tunadharauliana na kubaguana na kuendelea kuwaabudu Wazungu.
 
Pole sana,ungewapiga makofi mawili ingependeza zaidi maana kazi yao ni sehemu ya hizi kazi za hospitalituy,yani haiitaji mchezo hata kidogo.
Siku nyingine wachane baada ya hapo nenda kwa bosi wao,kitakachotokea watakuja kuhadithia wenyewe.
 
Wabongo hawatoi tips ndio maaana sehemu wakiwa wanakuja wabongo na wazungu lazma uone unabaguliwa sababu wabongo hawatoi pesa..mzungu anapendewa pesa sio rangi yake ile.
 
Bado sisi ni watumwa mkuu
Bora wangekua wanatutumikisha ila sio sisi kujitumikisha...inauma sana mzungu akiulizia hata directions mtaani kila mtu anataka kumuelekeza,ila we mbongo unaweza ukaulizia watu wakawa bize na time zao
 
Kuna mtu pia alishaandika kuwa ukivaa malapa na ndala na kuingia benki kuna uwezekano wa kutohudumiwa au kuonekana wa ajabu lakini Mzungu akivaa hivyo atahudumiwa na kuthaminiwa.

Watu weusi ni Watumwa kwa watu wenye ngozi nyeupe.

Ni kielimu, kisiasa, kijamii na zaidi kiuchumi.

We are inferior to the white race,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilienda bank moja crdb kile kidada cha mapokezi kikaniletea nyodo nikampigia boss wake akaja nikamwambia mpelekeni training huyu bibie. Nikazama kwa manager. Sijawahi kumkuta yule dada pale bank. Ukweli si hurka ya taasisi kubagua ila ni vyenyewe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kavae ndala na Mzungu avae ndala muongozane hotel kubwa ye atapita we utapigwa mkwara.

Ay- Inategemea na mtu.
 
Ndio wabongo tulivyo, mi nikiingia sehemu nakunja sura kwanza, naongeza makonfidensi mara 100 utaona wahusika wenyewe wanaanza kukunyenyekea. Ukienda kiupole pole dharau zao wana onesha waziwazi.
 
Wandungu mambo vipi civilians wenzangu?

Jana kuna jambo lilinitokea nkachukulia kawaida. I did not think it through, lakini baada ya kutulia na kuwasha flashback nikapata picha halisi.

In short jana nilienda pale Rock Garden Mwanza kuulizia bei ya boti kwenda Sanane island, sasa pale kuingia kwenye kigarden wameweka bango kiingilio ni Tsh1000/= ingawa hakuna uzio.

Lakini ile nafika kabla ya kuingia nikaona wazungu wawili wa kike wakiingia nao pia walikuwa wanaulizia boat, waliingia pale na kuanza kaongea direct na wahusika kwa muda wa kama dakika 15. Mimi nikawa nimesimama pale nje ya garden nasubiria wamalize wazungu na mimi niulizie.

Walipomaliza wazungu wakaondoka na mimi nikaingia kuulizia, ile naingia nikawaita wahusika na kuanza kuelezea shida kuwa sijaja kujivinjari hapa garden bali nina shida ya kukodi boat, waliniangalia juu chini halafu wakasema tafadhali tunakuomba usimame kwa nje kwakuwa hujalipia kiingilio, bila hiyana nikatoka nje na kumuita tuongelee kwa nje.

Tukaongea na kisha nikaondoka. Kwa kweli ile situation nilichukulia kawaida lakini leo nimekaa nikawaza na kukumbuka wale wazungu hawakulipa lakini waliingia direct na kuulizia mle ndani kama dakika 15 nzima bila kulipishwa.

Nikagundua na kuunganisha matukio ya zamani kuwa hizi sehemu za starehe, utalii, mabenki au mahotel makubwa huwa kuna ubaguzi wa chini chini na wabongo walioajiriwa pale.

Unakuta ukiingia hotelini au sehem ya Starehe kama ni mbongo walinzi wanakufuata na kukuuliza mara mbili mbili kama vile umepotea lakini wazungu wakija wanapokelewa kwa karibu nyingi kama kwao vile.

Inaniuma sana hapa Tanzania wote weusi tunadharauliana na kubaguana na kuendelea kuwaabudu Wazungu.
Mkuu kabla sijacomment cha maana, ngoja nikuulize: personal appearence yako ya siku hiyo ilikuwaje na ulivaaje labda?

Hilo kwa baadhi ya wanaume huwa hatulijali wala kulipatia uzito na tunajisahau sana!

Akina mama hawashuki thamani kwa sababu ni wajanja sana na wanalidhibiti sana hilo.

Unapotoka nyumbani kwako kwenda kwa watu jikague kama upo jeshi, kuwa umevaaje?

Siyo kiatu tu, je ni kiatu chenye thamani gani?

Siyo shati tu ama suruali tu, je vina thamani gani?

Umefunga mkanda wenye thamani gani, umepauka au una mabaka ya kuchakaa?

Shati umechomekea? Umeenda salon kushevu nywele?

Ndevu zako umezispray zinameremeta?

Maswali yote hayo niliyokuuliza uyajibu kwa ukweli uliokuwepo!

Utu wa mtu manjiani hubebwa na yeye mwenyewe alivyojiseti kwa kujistiri.

Siyo unavaa shati la sagurasagura wala halijapigwa pasi, eti unaenda kukodi boti!

Utaangaliwa juu chini hadi utajidharau!

Asikwambie mtu, vazi ndiyo humuweka mtu kwenye kundi analopaswa kuhesabiwa, bila kujali ana ukwasi kiasi gani mfukoni mwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhindi ana principal mona moja ya pesa, anasema vijicent huleta shilingi. Hata uwe na muonekano wa ajabu anaangalia ile senti yako ajalizie.
Dah basi hawa jamaa ni Wa kuwaiga sana kwenye customer care although wanavyowa'treat wafanyakaz wao nyuma ya pazia ndiyo wanazingua sana
 
Back
Top Bottom