Mndali ndanyelakakomu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2016
- 13,992
- 31,695
habar
Hii ni ya kweli nitaondoa baadhi ya vitu ili iwe fupi kidogo
Mwaka 2005 niliajiliwa kampuni X kama kibarua mwaka 2007 niacha kazi kampuni X na kuenda kampuni N
Hii yote nikutafuta maslahi bora lakini nilipata matokeo tofauti na matarajio yangu
Mwaka 2009 niliamua kutafuta njia ya kuiongezea kipato hapa ndio nilianza kufanya utafiti wa biashara gani nifanye
Kulikuwa na biashara nyingi zilizo nivutia
Duka la mahitaji majumbani
Duka la urembo
Duka la vifaa vya simu
Duka la nguo za mtumba
Duka la viatu vya mtumba
katika kufanya kwangu tafiti toka 2009 nilikuja kugundua zote zinahitaji mtaji mkubwa tofauti na matarajio yangu na hela niliyo kuwa nayo kwa wakati huo
Mwaka 2010 nilichagua biashara ya vifaa vya simu maana hii niliona inafaida kubwa na nirahisi kuiendesha hata nikiwa kazini
Nianza kutafuta frem kwaajili ya biashara yangu nilibahatika kupata frem maeneo mazuri na yanayo faa kwa biashara yangu
katika fremu niliyo panga ilihitaji marekebisho makubwa kidogo hapa paliongezea kukomba kamtaji kangu
Mpaka namaliza kukarabati chumba nilikuwa nimebakiwa na laki na nusu na hii ndio ilikuwa mtaji wangu wa kwaanza nao biashara
na niliamua kuchukua vifaa vya hela hiyo hiyo na hapo ndio mwanzo wa biashara yangu
Na hapo ndipo nilipo weka malengo ya kila mwezi kutoa kiasi cha sh. 30,000/ (elfu thelathini ) kila mwezi ili kuipa nguvu biashara yangu
mwaka 2011 mwanzoni niliamua kuajiri mtu kwaajili ya kuuza hapa sikuajiri ili nipate faida bali niliajiri ili watu waone kuwa mahali pale panapatikana bidhaa fulani
Mwaka huo huo nilipata pigo la kuibiwa karibu robo tatu ya duka lote na mzigo ulio baki ulikuwa ni kidogo sana
Hapa nilijikuta nimekata tamaa ya kiwango cha juu Asikwambie mtu kuwa na kitu gafla huna hapa unaweza kujikuta unatamani kufa
Nilikaa kama miezi mitatu nikajikusanya kusanya kidogo nikaanza tena upya maana niliona kukubali kushindwa ni kuogopa sanamu ya kuchongwa
baada ya miezi minne niliacha kazi kampuni N na kwenda kutafuta kazi kampuni D yenye fani tofauti na niliyo kuwepo
Kampuni D nilienda kwa malengo mawili kwanza ni kujifunza fani mpya
Pili ni kusafiri mikoa tofauti tofauti na kujifunza mazingira na fursa mpya za huko mikoa mingne
Hii kampuni ilinifanya nizunguke karibu tanzania nzima na nje ya nchi na kujifunza zaidi biashara niliyo kuwa nayo
huko nilifanya kazi kwa miezi kumi na nane(18) hapa niliamua kuacha kazi na kwenda kujiajiri rasmi na kufanya shughuli zangu
Nilikuwa tayari kidogo ninacho kipata nawekeza kwenye biashara yangu
Kwa kipindi nafanya kazi nilikuwa bado nimeajiri mtu ninavyo acha kazi Tuliendelea kuwa pamoja na mfanya kazi wangu ila tu kuna kazi nilimpa ambayo nilimwambia ni kama yake ila ilikuwa ndani ya ofisi yangu
baada ya hapo nilitafuta badhii ya baishara shirikishi ndani ya ofisi yangu
Niliweka MPESA hii iliniongezea katika kukuza mtaji
toka nimejiajiri sijawahi kujuta na wala kujilaumu
Ila tambua unapo amua kujiajiri unapaswa kujituma zaidi ya ulipo kuwa umeajiriwa
Fursa zipo nyingi chagua moja tembea nayo
Baada ya kuacha kazi yapo mengi niliyo fanya ili kuongeza kipato Changu na kujipa uhakika wa ajira yangu
Yapo niliyo yaacha ili kuweka fupi kidogo
Manyanyaso ya waajiri pamoja na mishahara ya kukatwa bila ridhaa ya mfanya kazi
Mungu awabariki wote