Jinsi nilivyougua miaka mingi na kunusurika kifo baada ya kurogewa uchawi wa bundi

Wewe endelea na stori yako mkuu...

Lakini sasa kwa wale wanaoifahamu Dar es Salaam miaka nenda rudi, hiyo mikanganyiko inakuwa inavuruga uhalisia...

Rekebisha hilo basi
Dar ya ss tofauti sana na zamani unaongelea Regency ya 2000 hii story ni 1975-1990's
Zamani hakukuwapo na Regence ilikuwapo Hindu Mandal na Zanaki ambazo ndio unaweza fanya kama rejea yako walikuwa wanatembea kutoka Zanaki mpaka Hindu Mandal kwa mwendo kama wa 2Km kama sijakosea.

Unabisha uwapo wa mtaa ulioitwa Kariakoo au Kariakoo ndogo ndani ya mtaa wa Keko Magurumbasi labda utakuwa haujawai kuishi Dar maana huo ni mtaa maarufu kwa kuuza pombe zote za kienyeji kwa kipindi hicho sijuhi kwa ss km bado upo.
 
Dar ya ss tofauti sana na zamani unaongelea Regency ya 2000 hii story ni 1975-1990's
Zamani hakukuwapo na Regence ilikuwapo Hindu Mandal na Zanaki ambazo ndio unaweza fanya kama rejea yako walikuwa wanatembea kutoka Zanaki mpaka Hindu Mandal kwa mwendo kama wa 2Km kama sijakosea.

Unabisha uwapo wa mtaa ulioitwa Kariakoo au Kariakoo ndogo ndani ya mtaa wa Keko Magurumbasi labda utakuwa haujawai kuishi Dar maana huo ni mtaa maarufu kwa kuuza pombe zote za kienyeji kwa kipindi hicho sijuhi kwa ss km bado upo.
Mkuu achana na hao watoto! Turudi kwenye story! Anayeona ni uongo akate pua aunge wajihi.
 
Dar ya ss tofauti sana na zamani unaongelea Regency ya 2000 hii story ni 1975-1990's
Zamani hakukuwapo na Regence ilikuwapo Hindu Mandal na Zanaki ambazo ndio unaweza fanya kama rejea yako walikuwa wanatembea kutoka Zanaki mpaka Hindu Mandal kwa mwendo kama wa 2Km kama sijakosea.

Unabisha uwapo wa mtaa ulioitwa Kariakoo au Kariakoo ndogo ndani ya mtaa wa Keko Magurumbasi labda utakuwa haujawai kuishi Dar maana huo ni mtaa maarufu kwa kuuza pombe zote za kienyeji kwa kipindi hicho sijuhi kwa ss km bado upo.
Endelea kushusha visa mhenga, nilitamani tu kuwekana kumbukumbu sawa hapo...
 
Endelea...
Niliondolewa hospitalini pale Hindu Mandal na kupelekwa nyumbani baada ya matibabu kushindikana,nilichoambulia ni dawa tu za kutibu malaria na sindano za kuchoma (yaani dozi ya sindano) .

Kuna mama alikuwa anakuja nyumbani ni jirani yetu ila ni nesi alikuwa anakuja kunipatia dozi ya sindano kutwa mara tatu mpaka nilipomaliza ,ilipita wiki mbili lakini hakukuwa na mabadiliko yeyote.

Hapo ndipo ukurasa rasmi wa kuanza kuangaika huku na huku kutafuta waganga wa kienyeji zilipoanza rasmi.

Zamani watu walikuwa wakarimu sana naadithiwa kuna mama wa jirani alikuja kunitembelea nyumbani.

Yeye ni Mzigua mwenyeji wa sehemu moja inaitwa kwa Chagga huko Handeni ndani ndani ,alivyoiona hali yangu na story alizozisikia zilimfanya kuja kuniona babla hajaondoka akasema kuna mganga ambaye ni ndugu yake ila anaishi maeneo ya Lushoto huko milimani kuna sehemu inaitwa Soni karibu karibu na Bumbuli.


Endelea......
 
Endelea...
Yule jirani aliamini kabisa kama tungeweza kukutana na huyo ndugu yake mganga basi angetusaidia na mm hali yangu ingerudi kama kawaida sababu watu wwnye matatizo kama yangu ya kurogewa uchawi wa bundi wengi tu alishawatibu na wakapona.

Hivyo basi tumaini la kupona likaibuka tukamuomba yule mama afanye mpango wa kuwasiliana na huyo mganga aje Dar Es Salaam sisi tutagharamika nauli yake ya kuja na kurudi.

Msomaji naomba ufahamu kuna waganga wengine masharti waliyopewa na mizimu yao ni kutotibu kwenye miji ya watu ,yaani waganga hao hawaruhusiwi na mizimu au kiti kutoka nje ya nyumba yake kwenda kumfuata mgonjwa.

Na hivi ndivyo ilivyo kwa mganga huyo ,hivyo yule mama akatufahamisha kwamba hilo swala la mganga kuja Dar alitowezekana hata nikimshawishi vipi maana kwa uzoefu anavyo mjua ndugu yake ajawahi kwenda kutibia nje ya mji wake na huo ndio mwiko wa uganga wake.

Hapo hatukuwa na jinsi zaidi ya kuandaa safari ya kwenda Tanga maeneo ya Soni milimani kwenda kumfuata mganga .

Endelea....
 
Endelea...
Tulianza safari ya kuelekea Tanga nikiwa nimebebwa sijitambui ,na tulipofika tulipokelewa vizuri kule Soni,Lushoto milimani.Hivyo tulikula chakula na tukalala kwanza ili kupumzika kwa ajiri ya uchovu maana mganga wenyewe hatukumkuta kwake kwa siku hile,tuliambiwa mganga ana wake wa nne na sisi tulifikia kwa mke mkubwa alikuwa anaitwa Bi Khadja bila shaka kwa siku hile alienda kuzungukia wale wake
wengine watatu.

Asubuhi na mapema mganja alikuja kutuona maana alishapewa taarifa kuna wageni wako walikuja jana wamefikia kwa Bi mkubwa .Si unajua bwana vijijini wageni wakija tu wanajulikana kama kuna watu wageni wamekuja na watu lazima wajue wale wageni wa nani.

Na jinsi ya mji wa Soni pale Lushoto ulivyokaa ni kama mlima yaani ni mlima stand ipo kwa chini ukiwa unapandisha watu wanakuona.

Endelea...
 
Endelea...
Basi baada ya kufika kijiji cha Soni huko Lushoto milimani asubuhi yake tulikutana na mwenyeji wetu tukaongea naye,akasema swala letu ni zito kidogo.

Hivyo akaagiza tumtafutie mbuzi,ubani maka ,ubani mashitaka, unga wa sulfur ambao mara nyingi unakuwa wa njano na vitu vingine kaza wa kaza.

Zoezi liliitajika kufanyika juu ya mlima ambapo ndio kuna mzimu wake,yaani ukitoka pale Soni unapandisha juu kidogo mlimani huko ndipo zoezi la kufanya kafara lilitakiwa kufanyika mida ya usiku.

Endelea....
 
Endelea...
Kwa mujibu wa mazungumzo ya mganga baada ya kupiga ramli yake aliona kabisa kwamba siku kabla ya tatizo kutokea kulikuwa na mtu alikuja kufukia vitu uwanjani,uwanja ambao ulipaswa kufanya shughuri au sherehe..

Hapo ndipo watu walipoamini kweli yule bwana alikuwa nguli wa kuona ramli yaani alijauaje kama miaka kadhaa kulikuwa na shughuri kijijini kwetu anasisistiza kuna mtu alifukia vitu au majini ndio yanayoleta shida.

Hivyo hivyo vitu inabidi vifukuliwe haraka sana na kutolewa baadaye vichomwe moto au vikatupe kwenye maji yanayotembea kwenye uelekeo tofauti na kilipo kijiji chetu.


Endelea...
 
Endelea...
Kiukweli hapo mganga aliwachanganya watu yaani watu wapo Tanga huko Lushoto vitu vimefukiwa Morogoro ss itawezekanaje vifukuliwe au itatubidi tupewe dawa twende tukavifukue na kuvichoma moto bwana mmoja aliuliza swali kama hilo.


Mganga akamjibu hapa mmefika swala dogo sana mm nitasafiri usiku na kwenda Morogoro kimazingara na kurudi kimazingara harafu nitarudi na vitu hivyo na tutavichoma wote hapa mkiona ,mradi mlete vitu au vifaa nilivyowaagiza mnunue mniletee nifanye kazi.Kamwe msiwe na wasiwasi mtu wenu atapona mganga alisisitiza.

Endelea....
 
Bila ajizi mganga alipatiwa mbuzi wake wa kafara na vitu vingine alivyoagiza teyari kwa kuanza kazi.

Ilipofika usiku mganga aliaandaa dawa zake watu wakabeba na mbuzi mpaka mlimani wakiwa wamebeba na vyakula na mahitaji mengine muhimu maana alibidi wa keshe mlimani.


Mganga alimwaga dawa kumzunguka mbuzi akaweka na majani ya kula mbuzi yaani kama mtego ambao unangoja atokee mnyama anayekula nyama mfano simba amvamie yule mbuzi na sisi tumuue huyo mnyama.Lakini mtego hule haukuwa kwa ajiri ya mnyama mla nyama bali kwa ajiri ya jini linalokunywa damu ya binadamu na viumbe ambalo lilichimbiwa kijijini Morogoro sasa linaitwa kwa jina lake litoke lilipochimbiwa lije kunywa damu ya mbuzi na pindi litakapofika tu mganga atalikamata kwa kutumia ungo ,ni ungo kama ungo lakini umezungushiwa na shanga shanga sio ungo wa mchezo mchezo yaani inavyoonekana ndio ungo wanaotumia wachawi kupaa angani usiku japo sina uhakika kama dada anavyosimulia.

Endelea....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom