Jinsi nilivyoteswa na mama mkwe, alichoma vyeti vyangu vyote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi nilivyoteswa na mama mkwe, alichoma vyeti vyangu vyote

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, Aug 12, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  Baada ya kusimamishwa kazi mambo mengi yalikwama kiasi cha kutimuliwa kwenye nyumba nliyokuwa naishi anga za Sinza.
  Mama mkwe alinibembeleza sana nikakae nyumbani kwake Tegeta ambako ana nyumba kubwa na anaishi peke yake.

  Nilienda ili nikae kwa wiki moja then niondoke ili nirudi kijijini kwetu Nassa Jeneri ili nikauze ng'ombe na nije kuanza maisha upya.
  Siku ya tatu ya ukaaji wangu ukweni nikiwa busy na JF mara sms ikaingia. Ile msg inaingia tu waif akaidaka simu na kukimbia nayo.

  Akampelekea mama yake, ambaye akaja akiwa amekasirika sana. Mke wangu akaanza kunitukana kuwa mimi ni malaya na mama mkwe akaanza kuchana chana nguo zangu huku akinisimanga kuwa sina mbele wala nyuma na matusi mengine mengi mazito yasiyoelezeka.

  Nguo zangu zikachanwa kiasi cha kuniacha mtupu kabisa, nikamwagiwa maji na kutolewa nje ya geti mchana kweupe.
  Simu yangu, vyeti, laptop na vitu vyangu vyote vikabaki kwa mama mkwe wangu.Niliondoka hadi mitaa ya jirani ambako kuna rafiki zangu walionisitiri.

  Baada ya siku chache nikaenda Mwanza kuuza ng'ombe wangu, sikuwa na simu wala namna yoyote ya mawasiliano.
  Nikiwa Mwanza niliuza ng'ombe nikanunua simu na kumpigia mama watoto.

  Akaniambia kuwa yale yote yalitokana na hasira, ndipo nikamuuliza kwani ile msg iliyoleta songombingo ilikuwa inasemaje?
  Akaniambia ilitumwa na sekretari wangu na aliiandika Dear boss, hali ya ofisini ni mbaya sana amna amani, i m praying for you. Dah.. Nlivyo ambiwa hivyo nkatamani kucheka na kulia kwa wakati mmoja.

  Nikauliza vyeti vyangu, nikaambiwa mama mkwe kachoma moto vyeti vyangu vyote vya sekondari hadi chuo.
  Nliposikia hivyo niliumia sana.

  Sasa nina mtaji wa milioni saba, wana jamvi anaombeni ushauri wenu je nifanye biashara gani kwa mtaji nilionao? Maana sina tena vyeti, biashara ndio maisha yangu yajayo.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Muwe mnaandika kwa kutumia aya.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  lm sorry ngabu, natumia mobile device, ila nilikuwa paragraphs
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nimesoma post yako... huku deep down hoping kua isiwe kweli..... Dah! Sad. Hata hivo naona kama the way umesimulia ni kana kwamba there is something missing na the story not complete... kuenda hizo extremes kwa mama mkwe hata kama kichaa kweli it has to be more than message ya kuambiwa dear Boss; Mara nyingi mtu unapokua ugenini hasa kwa wakwe inatakiwa u-minimize kabisa use of vitu kama mobiles maybe kama kweli za ki kazi ambazo ziko busy saana - which in your case hata haikuwa for ulihifadhiwa hapo kwa mda....

  Hata hivo pole na matatizo yamekupata... na naamini kabisa kua una mtihani mkubwa saana. Upande wa Biashara naona wataalam watapita hapa na kukushauri - ila tu la muhimu ni kua ni vizuri ukafanya biashara yenyewe una ujuzi nayo.... Na as much as vyeti vyako vimechomwa...next time docs za mhimu scana na serve hata kwenye email address yako kama drafts, in case of emergency...
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  inachekesha kwa kweli.....................
  sasa tukushauri biashara au tukushauri kuhusu mke na mama mkwe?

  unge save hiyo stori yote for yourself ,ukaja na la biashara...hapa

  otherwise utashauriwa zaidi ya mama mkwe na mkeo....
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,135
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Mikela naomba Mungu isiwe kweli bana kha!!!
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwani mkuu vyeti kuchanwa na mama mkwe ni kwamba huwezi kupata vingine, Nenda karipoti polisi kuwa vyeti vyako vimechanwa na utapata barua kutoka polisi ambayo utaenda nayo kuanzia shule yako ya msingi then nenda baraza la Mtihani na Chuo ulichosoma ambapo watakutolea Certified Copies za vyeti vyako vyote.

  Na utakakoomba kazi kokote unaambatanisha na ile barua ya polisi kuwa uliwahi kureport polisi juu ya uharibifu wa vyeti vyako na ndo maana una Cerified Copy. Mbona wengi wanapoteza vyeti au kuungua kwa moto au kuibiwa ila wanapata kazi

  Inaonekana kuchanwa kwa vyeti vyako ndo umeona mwisho wa maisha yako, kuhusu biashara ngoja waje wataalam kukupa ushauri
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hivyo vyeti ulivipatia wapi? Na huko ulikovipatia hawana/ hawatunzi nakala ambazo unaweza kwenda wakakupatia vivuli vyake kwa kulipa ada ndogo?
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  The Boss;

  Mambo ya mke na mama mkwe sio ya muhimu kwangu, kwasasa cha muhimu ni future yangu. Walisema sina mbele wala nyuma... Ngoja nitafute mbele na nyuma
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  ni kweli yametokea
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  UDSM na vyeti vingine ni vya baraza la mitihani
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Aug 12, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Sasa si uende tu hapo UDSM ukachukue vivuli vyake. Au hawana?
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,143
  Trophy Points: 280
  kamshtaki kuwa amechana nyaraka za serikali, ila Mpwa hii story ni kweli? na hizo 7M umezipataje fasta hivyo jamani?? haya pole bana, nenda Dubai kanunue nguo ufungue Boutique au wanavyofanya wenzio wenye mtaji kama wako wametafuta chumba cha biashara Mwenge na kununua Ngua kariakoo na kuja kuziuza kwa bei mbaya akijifanya ndio ametoka kuchukua Dubai au china, ila kama utafungua biashara ya ngu basi ziwe ni za watoto, nakwambia zinalipa sana...all da best
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu angalia ushauri hapo juu
   
 15. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  pole sana na matatzo yaliyokukumba ... naamini kuna mambo mengi ya kujifunza .. katika suala la biashara ni vyema ukatoa mawazo ya aina ya biashara utakayotaka kuifanya ili watu tuweze kukushauri kwani hatuwezi kukuambia aina ya biashara bila kupata mwelekeo wako
   
 16. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu,mwanaume kuvumilia,mwanaume kupambana,never give up,mpaka kieleweke.Hayo ni maisha ya mapito tu ambayo kimsingi ni ya muda,unatakiwa kuchukua nakala za vyeti vyako kwenye shule na chuo ulichosoma baada ya kutoa maelezo polisi,unatakiwa kumshitaki huyo mama mkwe na mwanaye,hawana maana.Ni unyama huo!!!!!!!Kuwa makini na mradi utakao uanzisha maana m7 ni kidogo,kuwa na msimamo!!!!Pambanaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Watakosaje? Yeye ahakikishe ameripoti polisi na amepata loss report!!!

  Pole mkuu!!
   
 18. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mamkwe kakuzabua vibao!??? Mi na izi hasira sijui tungefikishana wapi! naona kesi ingegeukia kwangu tu. Kuhusu biashara mi sina cha kukushauri, ila endelea kufuga hao ng'ombe tu, ila kwa milioni saba sijui umeuza ng'ombe wangapi shehe?
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,397
  Trophy Points: 280
  Mbona mi naona kama ameandika kwa paragraphs vile... au macho wangu ndio yanahitaji msaada wa yule mganga wa bungeni PROFESA MAJI MAREFU?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 12, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  That's just unnecessary bureaucratic red tape, IMHO. But I understand that, that could just be how they do things over there.
   
Loading...