Jinsi nilivyotapeliwa na mtu niliyedhani ni mhitaji kumbe ni tapeli

Kuna siku moja alinisimamisha mzee mmoja, akaniambia mwanangu nimetoka hospitali naomba nauli nipande bajaji kwa hali yangu siwezi kutembea nikampa. Wakati anaondoka nikajilaumu kwanini nimempa hela ya bajaji wakati obvious hela ya kula atakuwa hana naye ni mgonjwa.

Namfata chap kumuongezea fedha ya chakula, kwa mbali namuona bajaji anazipita bila kupanda mpaka akazimaliza. Mbele akamsimamisha mtu mwingine anamuomba, niliumia.
Afu huyo mzee namkumbuka, ana bichwa kubwa kama ndugai
 
Umenikumbusha miezi miwili iliyopita nikiwa pale studio nasubiri daladala niende kariakoo akaja kaka mmoja mdogo mdgo umri kati ya miaka 17-19. Akaniambia dada samahani mimi naulizia machinga complex ipo wapi, mimi nikasahau ilipo nikamwambia mh hata sikumbuki ipo wapil akasema yeye ametoka singida huku amekumbatia begi lake kama wa bush haswa aliepewa story dar kuna matapeli, akaniambia ni wachimbaji wadogo wa madinj hivyo wamepata na yeye ameambia aje huku auze maana wananunua kwa bei nzuri huko machinga complex,
Ikabidi nianze kumshauri.kwanza nikamwambia mimi machinga complex sipakumbuki ipo wapi ila ukiwa unamuuliza mtu usipende kumueleza shida yako yote sababu hujui yupi atakua mwema kwako na yupi mbaya. Basi ikabidi nimpigie mume wangu kumuuliza hivi machanga complex ipo wapi, huku napiga kuna baba yupo pembeni yangu mtu mzima yule kijana akaanza kumuuliza tena yule baba machinga xomplex ni wapi na akaanza kumuelezea habari ya yeye kuja kuuza haya madini, ikabidi nimvute yule kaka nimkumbushe awe makini asubiri mme wangu apokee sim anielekeze ni wapi na asirudie tena kuwaambia watu kila kitu kuhusu yeye. Bas yule baba akaamuelekeza machinga ni wapi, huku bado nasubiri daladala yule kaka akaanza kuniambia dada nisaidie nisije nkatapeliwa na bla bla nyingi, kilichokuja nitokea hata sielewi nilijikuta science sina simu wala pesa , ikabidi niombe msaada wa nauli nirudi nyumban.
Mpak leo naomba Mungu amuongoze yule kaka, unajitoa kumsaidia mtu kwa moyo kumbe ni tapeli.
Niliapa sitosaidia tena wapita njia lkn bado najiuliza kila mtu akila hiki kiapo tutaishi vipi maana na mimi nilisaidiwa nauli ya kurudi kwangu.
Kubwa ni kuwa makini matapeli ni wengi sana na sijui wengine wanatumia dawa gani maana niliumwa almost wiki nzima na nikawa napoteza kumbukumbu
Duuh pole Sana
 
Huu mkasa umenikumbusha mzee mmoja nilikutana naye kule mwanza yupo smart tu kimtindo akanijia kashika 200 mkonini akaniambia mtoto wangu nimepungukiwa Mia 200 nauli nataka nirudi nyumbani national igoma Basi nikatoa buku nikampa ,tukaachana nikajua kapanda daladala ile napiga misele nikamkuta yupo kasimama na dada mmoja anampanga Kama alivyonipanga Mimi na Mia mbili yake mkononi ....daa mjini shule
 
Habari ndugu wapendwa na natumaini sote tu wazima wa afya na walio na mitihani ya maradhi au changamoto mbali mbali Mungu awapiganie ili sote tuishi kwa raha na kukiri utukufu wa Mungu.

Nimeamua kuileta habari hii ambayo ilinitokea mimi mwenyewe ili iwe kama funzo kwa wengine wenye mioyo ya kusaidia wanadamu wenzao wenye uhitaji lakini badala yake wanakutana na matapeli.

Nakumbuka siku fulani miezi kadhaa nyuma nilipanda dala dala kituo cha Mwembechai nikiwa naelekea Sinza, pembeni yangu alikuwa ameketi kijana mmoja wa makamo hivi huku mkono wake wa kulia akiwa ameushikilia huku akigugumia kwa maumivu makali.

Kilio chake kilivuta hisia zangu kama mwanadamu na kutaka kujua zaidi alipatwa na jambo gani, basi katika maelezo yake machache na alinifunulia kile kiganja kilichokuwa kimevimba kwa kutunga usaha mzito huku akisema kuwa hana msaada wowote nikadhamiria kumsaidia.

Alisema kuwa alikuwa anahitaji kiasi kama 15,000/= ili akapasuliwe ule uvimbe na kusafishwa kidonda. Yeye alisema ni dereva wa magari madogo ya mizigo na maskani yake ni pale Manzese Bakhresa kwa hali hiyo anashindwa kufanya shughuli zake za udereva hivyo kukosa kipato na kupelekea kudhoofu kutokana na lishe duni, pale nilimpatia kiasi kama 20,000/= ili akajitibie na nikampatia mawasiliano yangu ili awe ananipa maendeleo ya kidonda chake na kwa msaada zaidi.

Baada ya pale tukawa tunawasiliana na yule kijana kuhusu maendeleo ya kidonda chake na nikawa kila siku namtumia 7,000/= kwa ajili ya kujikimu huku akijiuguza kidonda chake, baada ya masiku kadhaa nikamuuliza wewe unatokea mkoa gani akaniambia anatokea mkoa wa Tanga. Nikamwambia kwanini nisimpe nauli arudi Tanga kwa wazazi kupumzika akijiuguza taratibu mpaka atakapotengemaa ndipo arejee mjini maana kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba hata pakulala hana maana alifukuzwa baada ya kushindwa kulipia pango, basi tukakubaliana kesho yake ajiandae ili nimtumie nauli ili aende nyumbani kupumzika, kesho yake nikamtumia 50,000/= nikiamini itamtosha nauli ya Tanga na hela kidogo ya kujikimu.

Baada ya masaa kama 7 nikiamini ameshaondoka mjini kwenda Tanga, akanipigia Simu kwa namba ya mtu mwingine maana yeye hakuwa na simu, aliniambia kuwa ameshafika Stendi Kange lakini amepungukiwa na nauli maana amebakiwa na 5,000/= hivyo mpaka afike kwao hiyo hela haitoshi. Kuanzia hapo akili yangu ikawa na mashaka kwa kuwa Tanga napafahamu inawezekana vipi kutoka Dar mpaka Tanga atumie 45,000/= ? Sikumtumia hela nilimwambia nipo bize kidogo.

Baada kama dakika 10 nikatumia namba nyingine kumpigia yule aliyenipigia nilimpa msichana aongee naye ili nijue yupo wapi, ikagundua kuwa yule alikuwa Manzese darajani na hakuwa Tanga, nikawapigia watu waliokuwa wanampa simu niongee naye na nilipokuwa nawatumia kumtumia hela, wote wakanithibitishia kuwa yule jamaa yupo Pale pale Dar na alikuwa ni muokota makopo ya plastiki maarufu na pia mtumiaji mkubwa dawa za kulevya hata wakati namtumia fedha walijua mimi ni ndugu yake na mara nyingi anautumia mkono wake uliojaa usaha kujipatia kipato huo ndio ukawa mwisho wa mimi na yeye, na yote niliyomsaidia nikamwachia Mungu.

Nb;
Tuwe macho na tunaodhania wanahitaji misaada.
Pole sna lakini hongera kwa kuonesha huruma na utu.Jina lako Sasa litahifadhiwa katika makabati yote ya Africa na litaandikwa kwa wino wa dhahabu.
 
Pole sana mimi pia niliwahi kutapeliwa na mtu aliyejifanya mhitaji na mimi huruma ikanijaa basi nikatapeliwa,kitendo hicho kimenifanya niwe mzito sana kusaidia mtu nisiyemfahamu,niliumia mno,nawachukia matapeli na majambazi hata nikimkuta anachomwa moto naongezea kuni
Weee!! huku poteza yaani kwanza natamaniga niwe na Moyo km huo!! sijui kwa nini siupati!! km ulitoa kwa Moyo wako wote yaani Mungu ninae mjua atakubariki mpaka ushangae!!! endelea wala usiangalie nyuma na kujiuliza maswali meengi!
 
Pole kwake, hongera kwako mkuu.

Miaka ya nyuma nilikuwa ninafanya kazi sehemu fulani kipato cha chini mnooooo, ila sikuacha kutoa chochote kila Ijumaa kwa wazee waliopita kuomba msaada.

Kati yao alikuwepo Bibi mmoja ambaye nilikuwa namuandalia ya kwake hata nisipokuwa nayo akiba yangu ila yeye nilijitahidi kumpa.

Siku moja akaja nikampa. Akasema anaomba apumzike kidogo baadae akajifunika(akiamini amejificha) akaanza kuhesabu pesa. Ukweli ni kwamba alikuwa na kiasi kinachozidi hata mshahara wangu wa mwezi mzima.

Tangu pale nimejifunza kutoa zaidi kwenye vituo vya mayatima au mitaani ambapo naona kabisa maisha halisi ya mtu. Na nimeegemea kwa watoto zaidi.
Lkn sasa hivi unajionaje?? si una kipato kizuri weee endelea tu!! watu wengi humu hawajui siri ya kutoa angalia Donor Countries zinavo neemeka!!! siku nikiwa Rais nitaishangaza USA kwa kuipa misaada wallah!
 
61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom