Jinsi nilivyotapeliwa na mtu niliyedhani ni mhitaji kumbe ni tapeli

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,049
32,459
Habari ndugu wapendwa na natumaini sote tu wazima wa afya na walio na mitihani ya maradhi au changamoto mbali mbali Mungu awapiganie ili sote tuishi kwa raha na kukiri utukufu wa Mungu.

Nimeamua kuileta habari hii ambayo ilinitokea mimi mwenyewe ili iwe kama funzo kwa wengine wenye mioyo ya kusaidia wanadamu wenzao wenye uhitaji lakini badala yake wanakutana na matapeli.

Nakumbuka siku fulani miezi kadhaa nyuma nilipanda dala dala kituo cha Mwembechai nikiwa naelekea Sinza, pembeni yangu alikuwa ameketi kijana mmoja wa makamo hivi huku mkono wake wa kulia akiwa ameushikilia huku akigugumia kwa maumivu makali.

Kilio chake kilivuta hisia zangu kama mwanadamu na kutaka kujua zaidi alipatwa na jambo gani, basi katika maelezo yake machache na alinifunulia kile kiganja kilichokuwa kimevimba kwa kutunga usaha mzito huku akisema kuwa hana msaada wowote nikadhamiria kumsaidia.

Alisema kuwa alikuwa anahitaji kiasi kama 15,000/= ili akapasuliwe ule uvimbe na kusafishwa kidonda. Yeye alisema ni dereva wa magari madogo ya mizigo na maskani yake ni pale Manzese Bakhresa kwa hali hiyo anashindwa kufanya shughuli zake za udereva hivyo kukosa kipato na kupelekea kudhoofu kutokana na lishe duni, pale nilimpatia kiasi kama 20,000/= ili akajitibie na nikampatia mawasiliano yangu ili awe ananipa maendeleo ya kidonda chake na kwa msaada zaidi.

Baada ya pale tukawa tunawasiliana na yule kijana kuhusu maendeleo ya kidonda chake na nikawa kila siku namtumia 7,000/= kwa ajili ya kujikimu huku akijiuguza kidonda chake, baada ya masiku kadhaa nikamuuliza wewe unatokea mkoa gani akaniambia anatokea mkoa wa Tanga. Nikamwambia kwanini nisimpe nauli arudi Tanga kwa wazazi kupumzika akijiuguza taratibu mpaka atakapotengemaa ndipo arejee mjini maana kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba hata pakulala hana maana alifukuzwa baada ya kushindwa kulipia pango, basi tukakubaliana kesho yake ajiandae ili nimtumie nauli ili aende nyumbani kupumzika, kesho yake nikamtumia 50,000/= nikiamini itamtosha nauli ya Tanga na hela kidogo ya kujikimu.

Baada ya masaa kama 7 nikiamini ameshaondoka mjini kwenda Tanga, akanipigia Simu kwa namba ya mtu mwingine maana yeye hakuwa na simu, aliniambia kuwa ameshafika Stendi Kange lakini amepungukiwa na nauli maana amebakiwa na 5,000/= hivyo mpaka afike kwao hiyo hela haitoshi. Kuanzia hapo akili yangu ikawa na mashaka kwa kuwa Tanga napafahamu inawezekana vipi kutoka Dar mpaka Tanga atumie 45,000/= ? Sikumtumia hela nilimwambia nipo bize kidogo.

Baada kama dakika 10 nikatumia namba nyingine kumpigia yule aliyenipigia nilimpa msichana aongee naye ili nijue yupo wapi, ikagundua kuwa yule alikuwa Manzese darajani na hakuwa Tanga, nikawapigia watu waliokuwa wanampa simu niongee naye na nilipokuwa nawatumia kumtumia hela, wote wakanithibitishia kuwa yule jamaa yupo Pale pale Dar na alikuwa ni muokota makopo ya plastiki maarufu na pia mtumiaji mkubwa dawa za kulevya hata wakati namtumia fedha walijua mimi ni ndugu yake na mara nyingi anautumia mkono wake uliojaa usaha kujipatia kipato huo ndio ukawa mwisho wa mimi na yeye, na yote niliyomsaidia nikamwachia Mungu.

Nb;
Tuwe macho na tunaodhania wanahitaji misaada.
 
Wala usiumie

Katika kila tendo atendalo binadamu kwa mwenzake Mungu huwa anaangalia moyo wake,ni nini haswa kusudi la mtu kutenda jambo fulani kwa mwenzake na kama kusudi lako lilikua jema basi hakika hujapoteza!

Utavuna tu huo wema siku moja na wema huo utaenda adi kwa watoto wako, watafadhiliwa na wasiowajua!
 
Kuna siku moja alinisimamisha mzee mmoja, akaniambia mwanangu nimetoka hospitali naomba nauli nipande bajaji kwa hali yangu siwezi kutembea nikampa. Wakati anaondoka nikajilaumu kwanini nimempa hela ya bajaji wakati obvious hela ya kula atakuwa hana naye ni mgonjwa.

Namfata chap kumuongezea fedha ya chakula, kwa mbali namuona bajaji anazipita bila kupanda mpaka akazimaliza. Mbele akamsimamisha mtu mwingine anamuomba, niliumia.
 
Kuna siku moja alinisimamisha mzee mmoja, akaniambia mwanangu nimetoka hospitali naomba nauli nipande bajaji kwa hali yangu siwezi kutembea.. nikampa. Wakati anaondoka nikajilaumu kwanini nimempa hela ya bajaji wakati obvious hela ya kula atakuwa hana naye ni mgonjwa.

Namfata chap kumuongezea fedha ya chakula, kwa mbali namuona bajaji anazipita bila kupanda mpaka akazimaliza. Mbele akamsimamisha mtu mwingine anamuomba.. niliumia.
Wahenga wanasema usione ukadhani, pole ndugu kwa hilo tukio.
 
Mtu anaweza kuwa anakuomba pesa ya kula na kutibiwa kila siku kumbe ana pesa yake kwenye account hataki kuitumia sababu ina malengo.

Kuna wakati inahitaji kumshirikisha Mungu kabla hujatoa msaada.
Malipo ya wema hutoka kwa Mungu na sio mwanadamu kwa kuwa ni vigumu kujua dhamira ya anayeomba msaada lakini rahisi kujua dhamira ya anaye toa msaada.
 
Pole kwake, hongera kwako mkuu.

Miaka ya nyuma nilikuwa ninafanya kazi sehemu fulani kipato cha chini mnooooo, ila sikuacha kutoa chochote kila Ijumaa kwa wazee waliopita kuomba msaada.

Kati yao alikuwepo Bibi mmoja ambaye nilikuwa namuandalia ya kwake hata nisipokuwa nayo akiba yangu ila yeye nilijitahidi kumpa.

Siku moja akaja nikampa. Akasema anaomba apumzike kidogo baadae akajifunika(akiamini amejificha) akaanza kuhesabu pesa. Ukweli ni kwamba alikuwa na kiasi kinachozidi hata mshahara wangu wa mwezi mzima.

Tangu pale nimejifunza kutoa zaidi kwenye vituo vya mayatima au mitaani ambapo naona kabisa maisha halisi ya mtu. Na nimeegemea kwa watoto zaidi.
 
Pole sana mimi pia niliwahi kutapeliwa na mtu aliyejifanya mhitaji na mimi huruma ikanijaa basi nikatapeliwa,kitendo hicho kimenifanya niwe mzito sana kusaidia mtu nisiyemfahamu,niliumia mno,nawachukia matapeli na majambazi hata nikimkuta anachomwa moto naongezea kuni
 
Kuna siku niko pale jengo la CCM mkoa Mwanza alinisimamisha mama mmoja hivi kwa muonekano ni kama ana mimba sasa sijui ni mimba kweli au lah! mpaka leo sijui ile ilikuwa mimba! Basi akaniomba pesa ya nauli ya daladala alidai anaishi Kisesa kama kumbumbuku zangu ziko sawa maana ni miaka 4 imepita sasa.

Nikampa akaenda uelekeo ule wa daladala zizonasimama pale Kembondo kwa wenyeji wanapajua, nilivyompa sijui ni nini kiliniambia nigeuke kumuangalia yule mama bwana weee

Yule mama hakupanda daladala wala nini alizipita zile daladala kama hana akili nikamuangali anapandisha na ile barabara ya mataa huku akiendelea kusimamisha watu wengine niliumia sana.
 
Pole kwake, hongera kwako mkuu.

Miaka ya nyuma nilikuwa ninafanya kazi sehemu fulani kipato cha chini mnooooo, ila sikuacha kutoa chochote kila Ijumaa kwa wazee waliopita kuomba msaada.

Kati yao alikuwepo Bibi mmoja ambaye nilikuwa namuandalia ya kwake hata nisipokuwa nayo akiba yangu ila yeye nilijitahidi kumpa.

Siku moja akaja nikampa. Akasema anaomba apumzike kidogo baadae akajifunika(akiamini amejificha) akaanza kuhesabu pesa. Ukweli ni kwamba alikuwa na kiasi kinachozidi hata mshahara wangu wa mwezi mzima.

Tangu pale nimejifunza kutoa zaidi kwenye vituo vya mayatima au mitaani ambapo naona kabisa maisha halisi ya mtu. Na nimeegemea kwa watoto zaidi.
Pole sana ndugu.....ndio ulimwengu ulipofikia sasa.....watu wema wanatumika na watu wabaya badala ya kuenziwa.....so sad.....
 
Back
Top Bottom