Jinsi nilivyotapeliwa na mtu niliyedhani ni mhitaji kumbe ni tapeli

Kuna siku moja alinisimamisha mzee mmoja, akaniambia mwanangu nimetoka hospitali naomba nauli nipande bajaji kwa hali yangu siwezi kutembea nikampa. Wakati anaondoka nikajilaumu kwanini nimempa hela ya bajaji wakati obvious hela ya kula atakuwa hana naye ni mgonjwa.

Namfata chap kumuongezea fedha ya chakula, kwa mbali namuona bajaji anazipita bila kupanda mpaka akazimaliza. Mbele akamsimamisha mtu mwingine anamuomba, niliumia.
Mimi nilikutana na mzee maeneo ya kanisani magomeni na yeye akainiomba nauli..wakati narudi namwona kajibanza sehemu anahesabu hela nyingi🤣
 
Tunatakiwa tufkirie Mara mbili mbili kabla hatujasaidia watu

Inatakiwa ukae chini ufkirie Kama unachoambiwa na muomba msaada Kina ukweli
 
Umenikumbusha mbali sana!!mwaka jana kama mwez wa pili hv!!Mafuriko yalipiga sana pande zetu!!ikatokea mkulima mmoja mhamiaji tena ngosha ana wake wawili na amebomokewa nyumba hz za udongo !!akawa amepata hifadhi kwa mtu tena chumba kimoja akadai hakitoshi ana wake wawili na watoto karibu sita!nikaamua kumpa akae nyumba yangu ya vyumba viwili na sebule!!!sasa akanipigisha stori za biashara za samaki tukafikia mwafaka tufanye kazi sasa nikatoa mtaji na yeye akawa anabanika samaki!!samaki walipokauka tu!akasema soko zuri lipo kahama !akaenda kuwauza!!alipopata hela akaitumia hela familia yke kimya kimya na wakatoroka hadi leo sijawaona tena!!!!LAKINI CHA AJABU MAISHA YANGU YA KIFEDHA YALIBADILIKA SANA KUANZIA PALE!YAANI HADI LEO FAMILIA YANGU INAINGIZA PESA NYINGI AMBAZO HATA MWANZO NILIKUWA ZISIPATI!!HADI NASHANGAA HADI LEO AISEEH!!!
JAMAA ALIKUWA ANATIA HURUMA HUKU AKIWA NA WATOTO WADOGO CHINI YA MIAKA MIWILI NA WALIKUWA WANALALA CHINI TENA KUMELOWA MAJI!!LAKINI NILIWA NYUMBA YENYE KITANDA NA KILA KITU!!!
NADHANI MUNGU ALITUBARIKI KWASABB YA WALE WATOTO!!!
UKITAKA KUWA TAJIRI JIFUNZE KUTOA TU HASA PALE UNAPOKUWA NA AMANI MOYON.I MWAKO!HUWEZ JUA KWANN ANAKUDANGANYA UJUE ANA SHIDA KUBWA!!!
NIKUTIE MOYO SANA MAN!!WE ENDELEA TU!!!
 
Wewe utalipwa kwa kumsaidia na yeye atalipwa kwa kukutapeli
 
kuna kibabu huwa kila ijumaa anapita ofisini kwangu kuomba nampa jero au buku!!
siku hiyo sikumuona kama kawaida yake ya kupita mchana siku ya ijumaa!
badala yake akapitia jioni na akanikuta ofisini!!
nikamwambia leo sina kitu mzee umechelewa nimewapa wenzio...
akaanza kulalamika leo hali mbali toka asubuhi hadi jioni hajapata vile amezoea kupata!!
nikamuuliza kiutani kwani mzee umepata sh ngapi leo??!!
elfu 48 mwanangu yaani leo ni nuksi tupu!hadi leo omba omba pita hivi usinisogelee.

mwingine huwa anatembea kwenye mahospitali na hotpot na chupa ya chai..
anasema mtoto wake kalazwa amekataa kula hvyo anaomba ela kdgo ajaribu kumnunulia mtori au supu
 
kuna kibabu huwa kila ijumaa anapita ofisini kwangu kuomba nampa jero au buku!!
siku hiyo sikumuona kama kawaida yake ya kupita mchana siku ya ijumaa!
badala yake akapitia jioni na akanikuta ofisini!!
nikamwambia leo sina kitu mzee umechelewa nimewapa wenzio...
akaanza kulalamika leo hali mbali toka asubuhi hadi jioni hajapata vile amezoea kupata!!
nikamuuliza kiutani kwani mzee umepata sh ngapi leo??!!
elfu 48 mwanangu yaani leo ni nuksi tupu!hadi leo omba omba pita hivi usinisogelee.

mwingine huwa anatembea kwenye mahospitali na hotpot na chupa ya chai..
anasema mtoto wake kalazwa amekataa kula hvyo anaomba ela kdgo ajaribu kumnunulia mtori au supu
Mkuu kama una amani nafsini uwe unatoa tu!nafsi ndio mwalimu mzuri wa kila jambo!!!we fanya kile nafsi ina kwambia tu!!
 
Umenikumbusha miezi miwili iliyopita nikiwa pale studio nasubiri daladala niende kariakoo akaja kaka mmoja mdogo mdgo umri kati ya miaka 17-19. Akaniambia dada samahani mimi naulizia machinga complex ipo wapi, mimi nikasahau ilipo nikamwambia mh hata sikumbuki ipo wapil akasema yeye ametoka singida huku amekumbatia begi lake kama wa bush haswa aliepewa story dar kuna matapeli, akaniambia ni wachimbaji wadogo wa madinj hivyo wamepata na yeye ameambia aje huku auze maana wananunua kwa bei nzuri huko machinga complex,
Ikabidi nianze kumshauri.kwanza nikamwambia mimi machinga complex sipakumbuki ipo wapi ila ukiwa unamuuliza mtu usipende kumueleza shida yako yote sababu hujui yupi atakua mwema kwako na yupi mbaya. Basi ikabidi nimpigie mume wangu kumuuliza hivi machanga complex ipo wapi, huku napiga kuna baba yupo pembeni yangu mtu mzima yule kijana akaanza kumuuliza tena yule baba machinga xomplex ni wapi na akaanza kumuelezea habari ya yeye kuja kuuza haya madini, ikabidi nimvute yule kaka nimkumbushe awe makini asubiri mme wangu apokee sim anielekeze ni wapi na asirudie tena kuwaambia watu kila kitu kuhusu yeye. Bas yule baba akaamuelekeza machinga ni wapi, huku bado nasubiri daladala yule kaka akaanza kuniambia dada nisaidie nisije nkatapeliwa na bla bla nyingi, kilichokuja nitokea hata sielewi nilijikuta science sina simu wala pesa , ikabidi niombe msaada wa nauli nirudi nyumban.
Mpak leo naomba Mungu amuongoze yule kaka, unajitoa kumsaidia mtu kwa moyo kumbe ni tapeli.
Niliapa sitosaidia tena wapita njia lkn bado najiuliza kila mtu akila hiki kiapo tutaishi vipi maana na mimi nilisaidiwa nauli ya kurudi kwangu.
Kubwa ni kuwa makini matapeli ni wengi sana na sijui wengine wanatumia dawa gani maana niliumwa almost wiki nzima na nikawa napoteza kumbukumbu

Huyu nilikutana nae Manzese kwenye Zebra pale machale yakanicheza nikamkata jicho nikapanda bajaji nikaondoka zangu
Ila hadithi ni Kama hii hii
 
mimi hawa wanaotembezwa wameshikwa mikono,sio vipofu bali ni mbibi wa 70 na mdada kama wa 25 hivi.

ninaposhinda kuna vibanda vya jamaa wakala mwingine anaingiza nyimbo,vimegawanywa na barabara kimoja huko kingine huku,wakaja nimekaa na mshikaji wakaniomba nikawapa 2000,baadae nikahamia upande wa pili kwa yule wakala,wakanikuta wakiwa wanarudi wakaniomba tenaa.nikajua kumbe akikugeuzia mgongo tu na habari yako imeisha,hata akikukuta sehemu unapigwa mawe hatakumbuka.
 
mimi sikupi pole, ila nakupa hongera kwa kujali na kuwajibika ipasavyo; kimsingi binadamu tunapaswa kusaidiana kama hivyo kwa sababu ni kweli kuna wenye uhitaji huko mtaani......ni hawa waharifu wachache ndiyo wanaharibu na kuwaharibia wenzao wenye uhitaji wa kweli. kwa upande wako we umeshinda, tena sana tu. kinachopatikana hapo ni zaidi ya kile ambacho kingepatikana kwa aliye na shida kweli kweli. kitakachokosekana kwa tapeli huyo ni kikubwa sana hapo baadae.
 
Huyu nilikutana nae Manzese kwenye Zebra pale machale yakanicheza nikamkata jicho nikapanda bajaji nikaondoka zangu
Ila hadithi ni Kama hii hii
Nilikuja kuammbiwa wapo wengi wa design hii
 
Wala usiumie

Katika kila tendo atendalo binadamu kwa mwenzake Mungu huwa anaangalia moyo wake,ni nini haswa kusudi la mtu kutenda jambo fulani kwa mwenzake na kama kusudi lako lilikua jema basi hakika hujapoteza!

Utavuna tu huo wema siku moja na wema huo utaenda adi kwa watoto wako, watafadhiliwa na wasiowajua!
📌📌📌📌📌📌📌📌
 
Mtoa mada tegemea baraka zaidi kurudi kwako....endelea kutoa hata kama ni kibaka ww toa...ni hazina hiyo
 
Aisee kwa hiyo jamaa ameamua kutembea na mkono wenye usaha ili apige pesa tu, akicheza huo usaha utamuozesha mkono mwishowe utakatwa.
 
Mimi nilikutana na Mtu kipindi kile cha mfungo wa Ramadhani akanisimamisha akaniambia hajala tangu jana ivi basi yeye anatumia ARV akasema nimpe ata elfu moja akapate chai anywe zile dawa. Nikampa buku tano kwa vile alinionesha kile kichupa cha Dawa nimekaaa kama masaa ma3 hivi namuona yule jamaa amelewa yupo chakali yupo na wenzie niliumia sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Aiseee.
 
Back
Top Bottom