Jinsi nilivyotaka kutapeliwa kwenye Crypto-Currency: Chukua Tahadhari, itakusaidia

Sasa hapo ulikuwa unadeal na crypto currency kivipi mkuu mbona maelezo yote harafu ni pumba ....


Mimi nikajua labda umenunua Bitcoin ukakuta ni fake ,labda umenunua Tron ,Shiba Inu ,etherium ,ukakuta ni fake ....

Nikajua labda umefungua account binance ukaweka hela ikapotea ,nikajua labda umenunua coin badae ukakuta haina thamani ......


Mbona sijaona ulipo nunua coin (digital currency)?????


Hapo mbona sijaona sehemu ulipojikita kwenye crypto currency ....

Unajua mkuu wewe ni mweupe kichwani kabisa kuhusu crypto currency ....


Mtu anayejua crypto ,hawezi andika maneno yote hayo bila kutaja ,trust wallet ,binance ,hotbit ,na wallet mbalimbali zinazotumika kutunza hizo coin na kufanya exchange ....


Kiufupi wewe jamaa hujui kitu kuhusu crypto currency ,ni mweupe kabisa ....

Mada yako sijui imejikita wapi ,kwa sababu sijaona sehemu uliyonunua coin ,sijui ulitaka kuwatumia hao wazungu hela ili iweje ,sijui uwape $200 then watakupa $500 hivi kweli kwa mtu anayejua crypto anaweza andika huo uharo .....someni someni jamani ,acheni mihemko


......N.B ..Kwenye crypto currency kama utataka kufanya trade upate pesa za haraka ,kaa ukijua upo mbioni kupoteza mtaji wako ....kama utaamua kununua coin na kuhold ,kwa zaidi ya miaka 3 kaa ukijua unaenda kuwa millionea hio ndio Siri ya crypto currency....
Umeanza vizuri mwishoni mbwembwe zimezidi hadi umeharibu!
Kama unafahamu kutrade crypto on daily basis aka ku-scalp utatengeneza pesa, kama hujuhi kutrade basi invest kwa muda mrefu yaani hold hiyo position yako ulipie commission ya broker, interest...na bado coin ishuke thamani na upigwe! Wakati anayetrade ikishuka anauza, ikipanda ananua....kila siku analaza faida!

Tuache uvivu, tusome na tuwe na angalau na basics za macroeconomics!
 
Ujinga wako tu usisingizie cryptocurrency mbona hata kwenye vitunguu na viwanja mnapigwa ko vitunguu ni scarm ,acha ujinga kiongozi
Daa mkuu kuanzia wiki hii sijacheka zaidi Kama leo.
Tena usiku.
Watu wanauziwa Sana viwanja na tapeli.
Kuna rafiki yangu aliuziwa kiwanja 13M Tena wakauziwa wengi.
Akaenda court akapata tu Kama 6M akaamua kusamehe.
Tena aliyewakamatisha ni kiongozi wa mtaa mwenyekiti.
Utapeli upo kila Kona.
Hata demu hata demu anakupiga hela ya kutolea mimba afu 50K so Kama mko kumi hesabu.
Sema wanadhani mtandaoni sio Hawa Hawa watu matapeli wako huko pia.
 
Wakuu,

Kwanza kabisa, ieleweke wazi kuwa sipo hapa kupinga kuhusu Crypto-Currency trading, Forex Trading na jamii zote za mambo kama haya. Mie mwenyewe naendelea kujifunza ili nijue kwa undani na huenda siku moja nikawa expert wa hizi mambo. Lengo kubwa ni ku-share utapeli niliokumbana nao kwa baadhi ya matapeli wanaotaka pesa kirahisi ili kuokoa hata mtu mmoja asije akatapeliwa.

Sasa buana, mimi ni member wa Clubhouse, kama ujuavyo Clubhouse unaweza ku-connect na Dunia kwa haraka zaidi, nadhani ni kuliko Social media yoyote ile. Ni suala tu la wewe kuchagua Club (room) ya nchi gani unataka kuwa member na ukawa connected huko kufuatilia kinachojiri.

Sasa moja ya malengo ya mwaka huu niliyojiwekea ni kujifunza kwa undani ili nijue vizuri haya masuala ya crypto et al. Maana nimekuwa nikisikia stories nyingi sana na kwakuwa katika majukumu yangu nabakiwa na muda, nimeona si vibaya ikawa ni moja ya jambo naloweza kujifunza kupata knowldge. Ili nisiwe mwepesi wa kupinga pinga kila jambo kumbe sina taarifa za kutosha. Kwahiyo ili kutimiza lengo, nikawa nimejiunga Clubhouse kwenye groups (rooms) zinazoelezea masuala hayo kutoka nchi za Marekani na Uingereza. Nilikuwa nimeshafuatilia kidogo Youtube na Twitter kwenye space kutoka kwa wanaofahamu na kufanya mambo hayo kwa wadau wa Bongo land. Nikaona si vibaya kupanua wigo wa kujifunza zaidi ndio maana nikajiunga na hizo rooms za Uingereza na Marekani.

Kwahiyo kwenye profile yangu nikaandika mbwembwe za hapa na pale kama ilivyo profiles/bio za wengine. Members wa Clubhouse watakuwa wameelewa nachomaanisha. Miomngoni mwa niliyoandika kwenye profile/bio ni interests zangu za kujiunga Clubhouse ambapo, pamoja na mambo mengine, nikawa nimeandika kuwa nataka kujifunza zaidi kuhusu Digital business and E-Commerce et al. Ebwana eeeh, kilichojiri sasa... Endelea kufuatilia...

Tangu nimejiunga ni kama wiki 2 hivi, mwanzoni nilikuwa natumia anonymous account ila badae nikaona ngoja niweke real account maana niliona inaweza kuwa fursa ya kukutana na watu potential huku Duniania.

Sakata linaanzia hapa
Kumbe kila nikiingia kusikiliza hayo madini ya Crypto huko kwenye rooms ambazo nipo huwa kuna matapeli wanafanya inspection ya kila member, wanakuwa wanachungulia na kujua wewe una interests gani. Yaani kwa wastani hizo DMs sijui mnaita Backchannels ama kwa lugha rahisi inbox, huwa napokea zisizopungua 3 za hao matapeli kila siku. Imagine nimejiunga rooms za US na UK tu, ingekuwaje ningejiunga na Nchi nyingine wanazozungumza Kiingereza?

SIFA ZAO.
1. Wanakuwa hawana followers wengi na account zao ni mpya.
2. Majina yao yana utata na kwa kiasi kikubwa wanaanadika majina Fake
3. Instagram pages zao zina followers wengi ila ukiangalia posts hazizidi 10. Hii ina maanisha wana-hack accounts za watu kisha wanazitumia kufanya utapeli.
4. Wana lugha flani hivi za kukushawishi tena very professional. Yaani usipokuwa makini unaliwa.

Tuendelee sasa.
Kwahiyo mie mwanzo sikujua kinachoendelea maana sina muda mwingi sana tangu nijiunge. Na kwakuwa nina muda kidogo huku kwa Mabeberu nimeanza ku-adapt hali ya kumuamini mtu kwa haraka na kujaribu kuwa postive. Japo simaamishi kuwa namwamini kila mtu. Kwa mazingira niliyopo kuwaamini watu kwenye hii community nilipo ni kama culture tu. Ni jambo la kawaida. Sijawa exposed sana huko nje kwenye mambo mengi mengi sana kiasi cha kukumbana na kadhia nyingi kiviile. (Najua kuna watakao sema najifanya nimebadilika ama najaribu kuonesha kuwa sie Wabongo siyo waaminifu na siyo positive, ila nia yangu siyo hiyo na hii ni mada nyingine tutaijadili siku nyingine ikihitajika). Kwahiyo mwanzoni sikuwa nime-notice kabisa. Nikawa na-reponds positively.

Naendelea na kisa.

Sasa nikawa nimepokea hizo DMs buana, akaniambia crypto trading inavyokuwa na akasema ana-make pesa nyingi na kwamba watu wengi hawa-make pesa kutokana na sababu kuwa hawana experience yakutosha. Ila yeye anaweza kuniasaidia kufanya trading na nitakuwa nampa commission yake kama 10% hivi ya faida. Nikasema ngoja niendelee kumfuatilia nione wakati huo nikiwa sijamgundua kama ni tapeli. Akasema tubadilishane namba ili tuwasiliane kwa karibu zaidi. Nikawa nimempa buana, si unajua sisi wabongo tulivyo wepesi kuwaamini wazungu. Akawa amenipa namba na nikaona ni ya US. Nilivyocheki instragram profile yake nikakuta amepost mambo hayo ya crypto posts kama 10 hivi na account ina followers wasiopungua 3000.

Kilichoendelea.
Akazungumza swagga nyingi kisha akanambia nifungue account kwenye website flani hivi nilivyoicheki nikaona kweli inahusika na hizo mamboz. Nikafungua kweli. Akanambia kinachofuatia sasa ni ku-fund account yangu kwa USD 500. Nikamwambia sina, akasema naweza kuanza na USD 200. Mwingine alinimbia ataniazima USD 100 mie niweke 200. Duh.! Hapo kwenye kutuma pesa ndio huwa sipo mrahisi kiviiiile. Nikasema ngoja nifanye ka-research kafupi kwanza. Nikaingia Youtube kujua namna gani Scammers wanafanya Scamming kwenye crypto et al. Nikapata hints nyingi nyingi nikaona kuna mojawapo inataka kufanana na kisa changu japo ni tofauti kidogo. Nikavuta pumzi kidogo. Nikatulia makalio kwanza. Nikasema hebu nijipe muda kidogo. Japo alikuwa kama ashafanikiwa kunishawishi maana niliona pesa mbona naweka kwenye profile yangu na situmi mahala? Natapeliwaje sasa.?

Naendelea usichoke.
Sijakaa sawa nikapokea DM kwa tapeli mwingine kwa maelezo hayo hayo. Nikajifanya sijui kinachoendelea na akaaendelea kufunguka na akanipa namba ya simu nikaicheki nikajua ni ya state nyingine huko huko US. Nikapokea DMs tena na tena, yaani kwa wiki nzima mpaka sasa nimepokea DMs kama 15 hivi. Walipofikia watu watatu ndio nikagundua huu ni utapeli tayari. Nikacheeka, nikasema sawa nimejifunza jambo na mie, si mbaya kujua mambo yanayoendelea huku Duniani.

Sifa zao (Nyongeza)
1. Ukimwambia umpigie mzungumze live anakataa, atakwambia sijui yupo tight ofsin na braabraa nyiiingiiiii.
2. Wengine wakishajua unatoka nchi gani, ili uweze kumwamini, anajiunga CLUB (rooms) za nchi yako kabisa. Nilichungulia mmoja wapo nikakuta amejiunga Club za chama kimoja sitakitaja, yaani kajiunga kama rooms 3 hivi za chama hicho. Tena kawa-follow watu prominent kabisa nawajua kama wawili. Tapeli mmoja nimeona yaani kuna a prominet person na yeye kam-follow huyo tapeli. Sasa usipokuwa makini unaliwa kabisa maana unaweza kumwamini kidogo. Nilivyojaribu kumuuliza kama anafahamu kiswahili akasema hapana. Nikamuuliza mbona umejiunga kwenye rooms za Tanzania? Akanambia stori ndeefu, kiufupi akasema eti alikuwa anataka kuja bongo kufanya research kwahiyo akaona aanze ku-connect na wabongo. Duh. Utapeli professional.
3. Utasikia wanakwambia kuwa ukiweka USD 500 ndani ya wiki unapata USD 2500. Ukiweka USD 1000 unapata USD 10,000 kwa wiki. Aisee, yaani simple like that? Kama ingekuwa simple basi kila mtu angekuwa tajiri na watu wasingefanya kazi za kutoa jasho. Sikatai kuwa cypto ama Forex hupati faida, ila siyo kirahisi kihivyo.
4. Mwingine nilivyomwambia kuwa hakuna mtu anaweza kupata faida za namna hiyo, akaja na gear kuwa wao unapata faida ya 30%. Utapeli mtupu.
5. Mwingine anakung'ang'aniza umtumie adress yako, namba za simu. Hapo unaenda kupigwa kuwa makini. Maana huku kwa Mabeberu address ni kitu mojawapo sensitive sana.

Mwisho.
Tapeli mwingine akanambia nifungue wallet kwenye Bitcoin.com, mwingine kwenye Crypto.com. kisha wanakwambia Ku-fund account yako. Baada ya hapo wanasema watakuunganisha na hizo website zao ambazo ni kama brokers, hapo nadhani ndipo wanaenda kukupiga sasa. Kwakuwa sikufikia mwisho, sijui wanakupiga kwa style gani, ila hutumi pesa japo unafanya malipo kwenye account yako uliyofungua kisha baada ya hapo naona wanakuunganisha na links zao ambapo ndio unapigwa sasa.

Wakuu, maelezo yamekuwa mengi sana na sijasema yote ila ili kukatisha maneno nimeona niweza kushea hapa ili kuokoa watu wasije wakatapeliwa. Kuwa makini.
😂😂Polee ndugu. Ila hakuna mentor duniani atakayekufata wewe duniani while he make alot of money kingine hawa wanaokupa namba zinazoonyesha Ni states wengi Ni wanigeria na huenda wapo states au wasiwepo u.s.a hakuna nchi ina scammers wengi Kama Nigeria japo kila sehemu wapo. But keep grinding and don't stop to learn.
 
Mkuu Mimi nakwambia 2030 utakuja kujuta kwanini ulipuuzia crypto currency .....
Siwezi kujutia kwa sababu life goes on kwa miradi yangu

Hata 2008-2010 wadau wa bitcoin wakati inaanza anza waliniambia maneno unayoniambia nikapuuzia na sasa hivi maisha yanaendelea and i don't care nafanya yangu, sitegemei hela za miujiza

Kwanza kwa maisha gani nianze kuweka hela nianze kuisikilizia leo inapanda kesho inashuka, maisha niliyonayo yanatosha ilimradi naingiza kipato halali na familia yangu hailali njaa na miradi inaendelea

Financial freedom niliyo nayo inanitosha chief kwa hiyo siwezi kujutia kwa hela za kubeti na za kudownload!
 
Siwezi kujutia kwa sababu life goes on kwa miradi yangu

Hata 2008-2010 wadau wa bitcoin wakati inaanza anza waliniambia maneno unayoniambia nikapuuzia na sasa hivi maisha yanaendelea and i don't care nafanya yangu, sitegemei hela za miujiza

Kwanza kwa maisha gani nianze kuweka hela nianze kuisikilizia leo inapanda kesho inashuka, maisha niliyonayo yanatosha ilimradi naingiza kipato halali na familia yangu hailali njaa na miradi inaendelea

Financial freedom niliyo nayo inanitosha chief kwa hiyo siwezi kujutia kwa hela za kubeti na za kudownload!
Pointless
 
Wanaijeria kiakiri wapo kama wachina, wanambinu nyingi sana za wizi. Na niwatu wenye akili kinoma
 
Siwezi kujutia kwa sababu life goes on kwa miradi yangu

Hata 2008-2010 wadau wa bitcoin wakati inaanza anza waliniambia maneno unayoniambia nikapuuzia na sasa hivi maisha yanaendelea and i don't care nafanya yangu, sitegemei hela za miujiza

Kwanza kwa maisha gani nianze kuweka hela nianze kuisikilizia leo inapanda kesho inashuka, maisha niliyonayo yanatosha ilimradi naingiza kipato halali na familia yangu hailali njaa na miradi inaendelea

Financial freedom niliyo nayo inanitosha chief kwa hiyo siwezi kujutia kwa hela za kubeti na za kudownload!
Yaaani kumbe 2009 wakati Bitcoin inawekwa sokoni ulikaza kichwa hivi hivi na Bado hujutii ...

Mkuu Mimi sitaki kusema mengi ila wewe ni maskini jeuri tu ....

Kwa taarifa yako ungenunua hata BTC 7 enzi hizoo ungekuwa na hela ya kula wewe na familia yako mpaka unakufa bila kufanya kazi ....

ila kwa vile una umaskini wa kiburi na jeuri ,endelea hivo hivo
 
Yaaani kumbe 2009 wakati Bitcoin inawekwa sokoni ulikaza kichwa hivi hivi na Bado hujutii ...

Mkuu Mimi sitaki kusema mengi ila wewe ni maskini jeuri tu ....

Kwa taarifa yako ungenunua hata BTC 7 enzi hizoo ungekuwa na hela ya kula wewe na familia yako mpaka unakufa bila kufanya kazi ....

ila kwa vile una umaskini wa kiburi na jeuri ,endelea hivo hivo
HAYA WEWE KAMA UNA HELA YA KULA YA BITCOIN NA CRYPTO NA FAMILIA YAKO MPAKA UNAKUFA BILA KUFANYA KAZI UNATAFUTA NINI HUKU JF SASA? KAMA SIO KUJA KUCHOTA RAIA TU

UMASIKINI JEURI NA KIBURI MY FRIEND SIPO HUKO
 
Back
Top Bottom