Jinsi nilivyonusurika kuuawa baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Urais 1995

Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
14,430
Likes
37,848
Points
280
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
14,430 37,848 280
Wapendwa habari, ni matumaini yangu mko vyema mkiendelea vizuri na majukumu ya ujenzi wa taifa kwa ustawi wa taifa letu na familia zetu. Kuanzia sasa na kuendelea kila nipatapo nafasi nitakuwa nikisimulia huu mkasa uliotokea miaka 21 iliyopita ambapo M/Mungu alininusuru, na laiti kama nisingenusurika basi leo hii nisingekuwepo kwenye hii dunia. Nisiwachoshe kwa huu utangulizi, karibuni sana.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa uchaguzi ulioshirikisha vyama vingi vya siasa kufanyika, hivyo mvutano ulikuwa ni mkubwa kwa wagombea wa nafasi mbali mbali mbali za uongozi pamoja na wanachama wao. Kipindi cha kampeni kilipita na sasa ikawa kinachosubiriwa ni siku ya kwenda kupiga kura, siku ikawadia ambapo watu wengi walijitokeza kwenda kupiga kura na baada ya hapo kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ilikuwa ni kutangazwa kwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi huo uliofanyika.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumanne ya tarehe 31Oktoba majira ya saa 10 jioni ambapo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa kipindi hicho alipokuwa akisika kupitia STZ alikuwa akitangazia matokeo ya uchaguzi huo, baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye alimtangaza Dr. Salmin Amour kuwa ndie mshindi wa kiti hicho hivyo nderemo, vifijo na shamra shamra zikalipuka kwenye mitaa, watu wakafurahia na wengine kupita mitaani huku wakicheza beni na ngoma nyingine wanazozijua wao. Hapo ndipo siku ikageuka chungu kwangu kwani kwenye ukuta wa mbele nyumbani kwetu kulikuwa na picha ya aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama cha upinzani kipindi hicho, kwa vile nilikuwa bado ni mdogo na sielewi uchungu/hasira za mtu alieshindwa kwenye uchaguzi basi nilikwenda hadi ilipo ile picha na kuichana, kipindi naichana picha ile baba yangu alikuwa ndani amelala huku akiwa na hasira sana baada ya chama chake kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Wakati naendelea kuichana picha ile nikasikia mlango unafunguliwa, nikiwa naangalia vizuri ili nimjue aliefungua mlango nikakutana uso kwa uso na baba huku akiwa ameshika silaha mkononi na mimi nikiwa nimeshika vile vipande vya ile picha... Hapo sikutaka hata kujiuliza mara mbili, kwani kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu baba na kwa ile sura yake nilivyoiona kwa muda ule {sura yake ilikuwa imesawijika kama mtu aliekuwa analia} na akiwa na silaha mkononi, kengele ya hatari iligonga kichwani kwangu hivyo nikaanza kukimbia. Kwa vile nilikuwa bado mdogo nilikuwa na uwezo wa kukimbia ndani ya sekunde chache nilitoweka machoni mwake na asiweze kuniona tena. Wakati hayo yakitokea mama yangu alikuwa yuko jikoni akiosha vyombo na hivyo hakuwa akijua kinachoendelea.
Nitaendelea...
 
mjukuum

mjukuum

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2014
Messages
5,101
Likes
2,010
Points
280
mjukuum

mjukuum

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2014
5,101 2,010 280
Wapendwa habari, ni matumaini yangu mko vyema mkiendelea vizuri na majukumu ya ujenzi wa taifa kwa ustawi wa taifa letu na familia. Kuanzia sasa na kuendelea kila nipatapo nafasi nitakuwa nikisimulia huu mkasa uliotokea miaka 21 iliyopita ambapo M/Mungu alininusuru, na laiti kama nisingenusurika basi leo hii nisingekuwepo kwenye hii dunia. Nisiwachoshe kwa huu utangulizi, karibuni sana.
Umemaliza au ndio unaandika
 
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
14,430
Likes
37,848
Points
280
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
14,430 37,848 280
Itakuwia ngumu kueleweka mkuu ungeandika zima *ndio*
Upost sasa hapo utapotezwabna comment
Mkuu ni mkasa mrefu, nikiandika yote kwa pamoja itanichukua muda sana na itawachosha kusoma, hivyo najaribu kutulia ili niweze kufupisha na pia iweze kueleweka. Ahsante.
 
mjukuum

mjukuum

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2014
Messages
5,101
Likes
2,010
Points
280
mjukuum

mjukuum

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2014
5,101 2,010 280
Mkuu ni mkasa mrefu, nikiandika yote kwa pamoja itanichukua muda sana na itawachosha kusoma, hivyo najaribu kutulia ili niweze kufupisha na pia iweze kueleweka. Ahsante.
Kama ilikutokea ww na nikweli ungeiandika tu bora ndefu inayoeleweka kuliko fupi ya kuunga unga ambayo itakuwa ngumu kueleweka
 
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
14,430
Likes
37,848
Points
280
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
14,430 37,848 280
Kama ilikutokea ww na nikweli ungeiandika tu bora ndefu inayoeleweka kuliko fupi ya kuunga unga ambayo itakuwa ngumu kueleweka
Mkuu na jua una shauku ya kujua ilivyokuwa lakini sisi wengine hatushindi humu, tuna majukumu mengine ya kutafuta kwa ajili ya familia zetu
 
Tunzo

Tunzo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
2,692
Likes
863
Points
280
Tunzo

Tunzo

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
2,692 863 280
Wapendwa habari, ni matumaini yangu mko vyema mkiendelea vizuri na majukumu ya ujenzi wa taifa kwa ustawi wa taifa letu na familia zetu. Kuanzia sasa na kuendelea kila nipatapo nafasi nitakuwa nikisimulia huu mkasa uliotokea miaka 21 iliyopita ambapo M/Mungu alininusuru, na laiti kama nisingenusurika basi leo hii nisingekuwepo kwenye hii dunia. Nisiwachoshe kwa huu utangulizi, karibuni sana.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa uchaguzi ulioshirikisha vyama vingi vya siasa kufanyika, hivyo mvutano ulikuwa ni mkubwa kwa wagombea wa nafasi mbali mbali mbali za uongozi pamoja na wanachama wao. Kipindi cha kampeni kilipita na sasa ikawa kinachosubiriwa ni siku ya kwenda kupiga kura, siku ikawadia ambapo watu wengi walijitokeza kwenda kupiga kura na baada ya hapo kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ilikuwa ni kutangazwa kwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi huo uliofanyika.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumanne ya tarehe 31Oktoba majira ya saa 10 jioni ambapo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa kipindi hicho alipokuwa akisika kupitia STZ alikuwa akitangazia matokeo ya uchaguzi huo, baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye alimtangaza Dr. Salmin Amour kuwa ndie mshindi wa kiti hicho hivyo nderemo, vifijo na shamra shamra zikalipuka kwenye mitaa, watu wakafurahia na wengine kupita mitaani huku wakicheza beni na ngoma nyingine wanazozijua wao. Hapo ndipo siku ikageuka chungu kwangu kwani kwenye ukuta wa mbele nyumbani kwetu kulikuwa na picha ya aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama cha upinzani kipindi hicho, kwa vile nilikuwa bado ni mdogo na sielewi uchungu/hasira za mtu alieshindwa kwenye uchaguzi basi nilikwenda hadi ilipo ile picha na kuichana, kipindi naichana picha ile baba yangu alikuwa ndani amelala huku akiwa na hasira sana baada ya chama chake kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Wakati naendelea kuichana picha ile nikasikia mlango unafunguliwa, nikiwa naangalia vizuri ili nimjue aliefungua mlango nikakutana uso kwa uso na baba huku akiwa ameshika silaha mkononi na mimi nikiwa nimeshika vile vipande vya ile picha... Hapo sikutaka hata kujiuliza mara mbili, kwani kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu baba na kwa ile sura yake nilivyoiona kwa muda ule {sura yake ilikuwa imesawijika kama mtu aliekuwa analia} na akiwa na silaha mkononi, kengele ya hatari iligonga kichwani kwangu hivyo nikaanza kukimbia. Kwa vile nilikuwa bado mdogo nilikuwa na uwezo wa kukimbia ndani ya sekunde chache nilitoweka machoni mwake na asiweze kuniona tena. Wakati hayo yakitokea mama yangu alikuwa yuko jikoni akiosha vyombo na hivyo hakuwa akijua kinachoendelea.
Nitaendelea...
Nnaona umeamka na storeƴ ya wƙend
 
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
14,430
Likes
37,848
Points
280
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
14,430 37,848 280
.....Wakati hayo yakitokea mama yangu alikuwa yuko jikoni akiosha vyombo na hivyo hakuwa akijua kinachoendelea.

Naendelea

Kwahiyo baada ya mimi kukimbia mzee alirudi ndani na kwenda moja kwa moja hadi jikoni alipokuwa bi mkubwa na kumkaripia sana hadi alifikia hatua ya kutamka "huyu mpumbavu wako nitamuua leo", maneno haya yalichoma moyo wa bi mkubwa kwa vile hakuwa akijua kinachoendelea. Hivyo aliwaataarifu kaka na dada zangu ambao hawakuwa wakiishi nje ya mji na muda usiozidi masaa mawili wote wakawa wameshapata taarifa. Muda ule mimi nilipokimbia nilikwenda maeneo ya mbali kidogo na nyumbani kiasi hata nyumbani hakuna aliejua nilikimbilia wapi. Kwavile watu walikuwa wanasherehekea ushindi hakuna hata mtu mmoja mtaani aliekuwa anajua kinachoendelea. Baada ya shamra shamra kupungua ndipo watu wakapata habari kuwa mimi nimepotea na sijulikani nimepotelea wapi, hivyo sasa juhudi za kunitafuta zikaanza lakini hata kule nilipokimbilia nikapata taarifa kuwa natafutwa kupitia kwa marafiki zangu na hivyo kunifanya nikimbilie mbali zaidi, na kila nilipokuwa nikisikia kuwa natafutwa nikawa nazidi kukimbilia mbali zaidi hatimaye siku ikapita. Siku ya pili nikiwa niko mbali na nyumbani sasa ndipo akili ikanikaa sawa na kuamua nirudi nyumbani lakini kwa umakini mkubwa ili nisikutane na baba njiani kwani japokuwa nilikiwa mdogo lakini nilikuwa naelewa jinsi mzee anavyokuwa na hadira zake zilivyo, hivyo nilirudi nyumbani na kuwakuta majirani pamoja na ndugu jinsi walivyochoka kunitafuta na baada ya kuingia nyumbani kuna kaka yangu mmoja alikuja na kunichukua na kukaa kwake. Hayo yote wakati yakiendelea mzee yeye alikuwa wala hajali {kuanzia kupotea kwangu mpaka niliporudi nyumbani}, hivyo nilikaa kwa kaka yangu mpaka baada ya muda ndipo nikarudi nyumbani.

Baada ya kurudi nyumbani nilikuwa naishi kiumakini sana kwa kudhani huyu mzee muda wowote anaweza kutekeleza azma yake aliyoiweka kwangu. Hivyo nilikuwa najitahidi kumkwepa kwa kadri nilivyoweza ili tusikutane sehemu yoyote ile au nyumbani tukiwa ni mimi na yeye tu, niliishi hivyo kwa muda usiopungua miaka miwili hadi mwaka 1998, ndipo niligundua kuwa kipindi kile wakati mimi nilipokimbia kumbe mama kwa kushirikiana na kaka na dada zangu walikwenda Polisi, hivyo mzee asingeweza kunifanya kitu chochote kibaya au laiti kama angenidhuru basi na yeye angeishia ndani, hivyo hapo baada ya kulijua hilo ndio kidogo na mimi nikawa na amani na hata hivyo mwaka 2000 niliondoka nyumbani na kwenda kuishi kwa kaka yangu. Niliishi kwa kaka yangu hadi mwaka 2002 ndipo nikarudi nyumbani na kipindi hiki nilimkuta baba tayari akiwa ameshaanza kupoa pamoja na umri kuwa umekwenda hivyo hapa ndio tukawa marafiki na vile ikawa tayari nimeshaanza kujiajiri hivyo ikawa tukikaa kuna urafiki pamoja na kugongeana hela za sigara. Ilikuwa nikirudi nyumbani kama hana hela ya sigara nampatia lakini hela za matumizi nilikuwa namuachia bi mkubwa. Huu mkasa ulinipa athari kubwa sana kwenye kumbukumbu zangu kwani hata shuleni somo la Civics nilikuwa nalichukua hasa kwa kugundua kipindi kile nilikuwa mdogo na matokeo ya uchaguzi ndio yalikuwa yanataka kuondoka na uhai wangu, na hata shuleni kwenyewe nilikuwa nasoma kwa ajili ya kujibu mitihani tu. Mbali na athari hizo lakini pia mkasa huu ulifanya ufahamu wangu shuleni kuporomoka kwani kila nilipokuwa nakumbukia hili tukio basi nilijikuta nazidi kupoteza uwezo wa kiakili. Nilikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi waliokuwa wanafanya vizuri shuleni lakini
Tukio lile limenifanya mpaka sasa nimejikuta naichukia sana SIASA na wala mambo yote yanayohusu siasa siyapi umuhimu kwenye maisha yangu.

Kwa hivi sasa mzee umri umeshamtupa mkono na hata nikienda nyumbani huwa nakaa nae na kuongea mawili matatu na muda mwingine huwa nikiwa nipo mbali na nyumbani mzee huwa anawaambia kaka zangu kuwa hawana maana yoyote na wala sio msaada kwake na mbele yao huwa ananisifia mimi, huwa nikizipata hizo nabaki nashangaa na kujiuliza maswali mengi kichwani ambayo hadi leo hii sijapata majibu yake, miongoni mwa maswali ambayo najiuliza ni:-
1. Hivi kweli baba alikuwa anataka kuniua?
2. Kama angeniua inamaana na yeye angekuwa wapi hadi muda huu?
3. Kipindi kile alitaka kuniua na je kama angeniua angekuwa anamsifia nani sahivi?
4. Inamaana mi sahv ningekuwa marehemu?
5. Kweli matokeo ya uchaguzi ndio yapelekee kumuua mwanao?

Naamini hivi sasa mzee amepata funzo kwa ile dhamira yake kwangu na nafsi yake inamsuta kina anaponiona, najua nilimkosea sana mzee kwa kitendo kile lakini si kwa akili yangu na wala sikudhamiria bali ni akili ya utoto ndio iliyokuwa inaniongoza.

Kwetu sisi wazazi, tulee watoto wetu katika malezi yaliyo bora na hata kama wakiwa wanatukosea tupime uzito wa kosa kulinganisha na adhabu tutakazowapa, tusiwe wepesi kuwahukumu watoto wetu kwa kuwa na haraka ya kutoa hukumu bila kupima uzito wa kosa na kiwango cha uelewa wa mtoto kwa kuzingatia umri. Katika maisha yangu siku zote najiapiza sitokuja kumwadhibu mtoto wangu kwa adhabu yoyote kubwa kama iliyotaka kunikuta mimi, hata nikitaka kumwadhibu basi nitapima ukubwa wa adhabu ili ilingne na kosa lake alilotenda.
Naomba kuwasilisha.

Natumai kuwa kila ambaye ataipitia hii post atapata mafunzo ndani yake na wale wanaohisi ni porojo wataacha kejeli na dharau zao kwangu
Historia ya kweli by Alibakari.
 
Padri Mcharo

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2015
Messages
1,931
Likes
3,351
Points
280
Padri Mcharo

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2015
1,931 3,351 280
Story ya kipumbavu tu...
Story yenyewe fupi unajifanya kuikuza iwe ndefu... Story Nusu nusu.
Pumbavu kabisa.
 
Queenever

Queenever

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2017
Messages
1,101
Likes
1,395
Points
280
Queenever

Queenever

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2017
1,101 1,395 280
Ndo nini sasa umehadithia
 
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
5,144
Likes
3,966
Points
280
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
5,144 3,966 280
Wapendwa habari, ni matumaini yangu mko vyema mkiendelea vizuri na majukumu ya ujenzi wa taifa kwa ustawi wa taifa letu na familia zetu. Kuanzia sasa na kuendelea kila nipatapo nafasi nitakuwa nikisimulia huu mkasa uliotokea miaka 21 iliyopita ambapo M/Mungu alininusuru, na laiti kama nisingenusurika basi leo hii nisingekuwepo kwenye hii dunia. Nisiwachoshe kwa huu utangulizi, karibuni sana.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa uchaguzi ulioshirikisha vyama vingi vya siasa kufanyika, hivyo mvutano ulikuwa ni mkubwa kwa wagombea wa nafasi mbali mbali mbali za uongozi pamoja na wanachama wao. Kipindi cha kampeni kilipita na sasa ikawa kinachosubiriwa ni siku ya kwenda kupiga kura, siku ikawadia ambapo watu wengi walijitokeza kwenda kupiga kura na baada ya hapo kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ilikuwa ni kutangazwa kwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi huo uliofanyika.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumanne ya tarehe 31Oktoba majira ya saa 10 jioni ambapo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa kipindi hicho alipokuwa akisika kupitia STZ alikuwa akitangazia matokeo ya uchaguzi huo, baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye alimtangaza Dr. Salmin Amour kuwa ndie mshindi wa kiti hicho hivyo nderemo, vifijo na shamra shamra zikalipuka kwenye mitaa, watu wakafurahia na wengine kupita mitaani huku wakicheza beni na ngoma nyingine wanazozijua wao. Hapo ndipo siku ikageuka chungu kwangu kwani kwenye ukuta wa mbele nyumbani kwetu kulikuwa na picha ya aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia chama cha upinzani kipindi hicho, kwa vile nilikuwa bado ni mdogo na sielewi uchungu/hasira za mtu alieshindwa kwenye uchaguzi basi nilikwenda hadi ilipo ile picha na kuichana, kipindi naichana picha ile baba yangu alikuwa ndani amelala huku akiwa na hasira sana baada ya chama chake kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Wakati naendelea kuichana picha ile nikasikia mlango unafunguliwa, nikiwa naangalia vizuri ili nimjue aliefungua mlango nikakutana uso kwa uso na baba huku akiwa ameshika silaha mkononi na mimi nikiwa nimeshika vile vipande vya ile picha... Hapo sikutaka hata kujiuliza mara mbili, kwani kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu baba na kwa ile sura yake nilivyoiona kwa muda ule {sura yake ilikuwa imesawijika kama mtu aliekuwa analia} na akiwa na silaha mkononi, kengele ya hatari iligonga kichwani kwangu hivyo nikaanza kukimbia. Kwa vile nilikuwa bado mdogo nilikuwa na uwezo wa kukimbia ndani ya sekunde chache nilitoweka machoni mwake na asiweze kuniona tena. Wakati hayo yakitokea mama yangu alikuwa yuko jikoni akiosha vyombo na hivyo hakuwa akijua kinachoendelea.
Nitaendelea...
Ungesema sasa hiyo episode ya pili utaitoa lini ili wasomaji wako wajue hizo series zako.
 
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
14,430
Likes
37,848
Points
280
Beberu Mwitu

Beberu Mwitu

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
14,430 37,848 280
Ungesema sasa hiyo episode ya pili utaitoa lini ili wasomaji wako wajue hizo series zako.
Ndugu, kumbuka hii siyo stori ya kutunga, nimegusa maisha yangu
 
Forum statistics

Threads 1,213,291
Members 462,055
Posts 28,472,820