Jinsi nilivyonusurika kifo kwa kipigo baada ya kujitambulisha kazi yangu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Ilikuwa siku ya jumamosi tulivu ambapo jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla macho na akili zao zilikuwa zimeelekezwa wilayani Temeke kushuhudia mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga wakichiana kugombea ngao ya Jamii.

Mimi na rafiki yangu Dr. Gill Biz na mkewe Hawa, tulikuwa pande za Buguruni tukiburudika na vinywaji laini anga hizo.

Kuna jamaa yetu mwingine Dr. Ally Na, yeye alikuwa Vinginguti, akatupigia simu kuwa amenunua nusu mbuzi hivyo tukamchakate na kumfanya kitoweo.

Basi tukaenda huko kujumuika. Tulipofika huko Mambo yalikuwa mazuri kwelikweli, chupa za kijani na za kahawia zilikuwa zimetamaliki zikitungoja.

Tukala, tukanywa, na tukahamia kwenye bar nyingine huko huko.

Njia ya kwenda huko ilikuwa imejaa vichochoro na kona nyingi, na baada ya dakika 7 tukafika.

Tukakaa huko hadi mida ya saa nne usiku, na tukaamua turudi zetu Makongo Juu tunakoishi.

Tukiwa tunachoronga vichochoro, kwa bahati mbaya tukapotea na tukajikuta tuko katikati ya nyumba ya watu na kuna wanawake wanne wakisukana.

Basi tukawasalimia na kuwaomba msamaha na kuwaomba watuelekeze njia ya kutokea barabara kubwa .

Mmoja kati ya wale wanawake akasema kina baba kwani nyie mnafanya kazi gani?

Wenzangu wakajibu kwamba ni madaktari. Wakaniuliza wee baba Mbona hujitambulishi?

Nikajibu Mimi ni Askari polisi hapo Buguruni.

Basi baada ya hapo, mmoja wa wamama wale akasema "Hapa ni mbali na barabara kubwa na vichochoro ni vingi mtapotea, ngoja nikuitieni kijana awaongozeni njia"

Basi yule mama akatoka na akaenda huko nyuma.

Baada ya dakika tano akarudi yule mama akiwa ameongozana na vijana watatu wenye magongo, na mmoja wao akasema "Yuko wapi huyo polisi?"

Wakanaanza kunipiga, wakaongezeka na wengine wengi kama kumi na nane au ishirini, nikapigwa kikamilifu.

Jamaa zangu wakajaribu kujisaidia na kuwasihi wapigaji wasinipige, lakini haikusaidia kitu. Nilipigwa nikapigika, nikaiva.

Nilipigwa Sana Hadi nikapoteza fahamu. Nikazinduka baada ya siku tatu nikiwa nimelazwa hospitali ya Amana.

Namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuninusuru na kifo.

Wito wangu kwa Askari Polisi, mkiwa uswahilini hakikisheni mnaficha utambulisho wenu kwa ajili ya usalama wenu.
 
Ilikuwa siku ya jumamosi tulivu ambapo jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla macho na akili zao zilikuwa zimeelekezwa wilayani Temeke kushuhudia mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga wakichiana kugombea ngao ya Jamii.
Chai ya rangi bila sukari kumbuka huwa hainyweki
 
Ilikuwa siku ya jumamosi tulivu ambapo jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla macho na akili zao zilikuwa zimeelekezwa wilayani Temeke kushuhudia mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga wakichiana kugombea ngao ya Jamii.

Mimi na rafiki yangu Dr. Gill Biz na mkewe Hawa, tulikuwa pande za Buguruni tukiburudika na vinywaji laini anga hizo.

Kuna jamaa yetu mwingine Dr. Ally Na, yeye alikuwa Vinginguti, akatupigia simu kuwa amenunua nusu mbuzi hivyo tukamchakate na kumfanya

Habari hii isiache kumfikia Sirro na wenziwe
 
Back
Top Bottom