Jinsi nilivyolipiza kisasi baada ya Kuliwa nauli (kisa cha Kweli)

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,276
2,000
Nilikwenda kumtembelea mwanangu shuleni mkoa fulani, nikakutana na walimu wake ili kutambuana na nilitambulishwa kwa mwalimu wake wa darasa, alinisalimia kwa uchangamfu wa hali ya juu na kiukweli ana sifa zote za kuitwa mwanamke mrembo niliomba mawasiliano yake kwa ajili ya “kufuatulia maendeleo ya mtoto”,

Baada ya siku kadhaa nilimpigia simu na kumueleza kwamba pamoja na kwamba nilikuja shuleni kufuatilia maendeleo ya mtoto, ila moyo wangu kwake umepata udhaifu, dada yule alionesha ushirikiano chanya na kuafikiana kama akipata muda atanijulisha ili aje kunitembelea, siku moja alinipigia simu kuwa amepata muda hivyo nimtumie nauli, bila kusita nami nikafanya hivyo (nauli ya ndege toka mkoa wa jirani) tangu siku hiyo hakuwahi kupokea tena simu zangu na hata kufikia hatua ya kuni “block”

Nilifanya maamuzi ya haraka ambapo nilimpigia simu mwalimu mkuu na kumuuliza mbona mwanangu hajapata Sare mpya hata baada ya kulipa hela? Akaniuliza hela nilimpa nani? Basi bila kusita nikamtumia jumbe ya na mtoto alipata seti nzima ya sare.

Mwisho
 

Kingfisher

JF-Expert Member
May 22, 2015
3,574
2,000
Huwa tunatuma tickets na sio hela
IMG_3990.jpg
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
552
1,000
Haahahaaaha we jamaa,kwahiyo ndo kusema ulitaka ule tunda kimasihara,ukaishia kuliwa hela na kula Block matata!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom