Jinsi nilivyokuwa nadhani nimeokoka kumbe ni wakala wa ibilisi kanisani

Mwaka 2017 nilipata neema ya wokovu, niliombewa sala ya toba na nikakaribishwa rasmi kundini, kwenye kuitenda kazi ya BWANA.

Maisha yangu kabla ya wokovu yalikuwa ni maisha meusi, ulevi, umalaya, uvutaji wa mioshi mbalimbali, uhuni, udhalimu, uporaji, udhulumaji, na ubazazi usiolezeka.

Maisha yangu yalinifanya nichukiwe na wengi, ila wengi waliniogopa na waliogopa kunisema na kunikosoa.

Ukiwa mwovu, fanya urafiki na polisi, hii ilikuwa ndio njia yangu kubwa ya kupata ulinzi.
Ukinipeleka polisi utalala mahabusu wewe huku Mimi mtuhumiwa nikikuletea chai na bigijii.

Maisha yangu ya mwanzo ya wokovu yalikuwa mazuri, hakika hata Mimi mwenyewe nikajiona hakika nimebadilika.

Hamna kitu kibaya kwenye maisha ya mwanadamu kama mazoea. Siku zilienda na Mimi nikazoea wokovu, nikalizoa na jina la YESU.

Taratibu taratibu nikaanza ku slide back na kuurudia utu wangu wa kale.

Kanisani nikaacha kutoa sadaka, nikawa naiba sadaka nikipewa zamu ya ukisanyaji. (Nilipewa uzee wa kanisa)

Nikaanza kunyandua binti mmoja baada ya mwingine. Nikaanza kuwafundisha mabinti walokole kunywa pombe, wengine nikawafundisha na uvutaji wa sigara na mioshi mingine, nikawafundisha maisha ya starehe za usiku.

Miingoni mwa mabinti niliowapeleka puta ni binti wa mchungaji, mwanafunzi wa kidato cha tatu tu.

Nikaanza kuwatapeli waumini wa kanisa. Wengine niliwadanganya kwamba Mimi naweza kuwaagizia Magari mazuri kupitia kampuni ya SBT.

Waliponipa pesa zao nikazitumia.

Wengine niliwauzia Beach plots feki wilayani Mkuranga na Bagamoyo.

Mchungaji nilimrubuni anipe milioni 50 nimletee mganga kutoka Nigeria atakayempa nguvu za kuvuta watu wengi na kutenda MIUJIZA mikubwa. Licha ya kukataa sana, mwisho wa siku nikafanikiwa kumrubuni na akakubali.
Jina langu likaanza kupata rangi nyeusi, Mambo mengi niliyoyatenda sirini yakaanza kuonekana hadharani.

Mabinti wanne walitengwa na kanisa kwa kushika ujauzito nje ya ndoa, zote zikiwa ni mimba zangu.

Kanisa nikawa nimelichafua kwelikweli. Nikaacha kusali na nikabadilisha namba za simu.

Wito wangu kwa umma usiwaamini watu haraka haraka. Hata Biblia inasema msiziamini kila roho ila mzichunguze
Yaacheni magugu yaote pamoja na ngano..yatapepetwa siku ya mavuno.

Mrudieni Mungu.

Jina la Yesu lihimidiwe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wewe mzee sasa unazeeka vibaya!!! kwa nini umeamua kusema uongo namna hii ???!!nakuuliza weye? na unijibu ili uwe salama! hivi kweli wewe uingie kanisani na Mungu huyu! ! nae mjua huyu!! akuvumilie kiasi hicho kweli? kwanza njoo hapa, na fimbo zako kabisaa!

tena unyooke!! Macho chini matako juu! ukishika nimefuta! ndo ujue Mungu hadihakiwi!!!
Baa yesu alikuwa km wewe!! kumbe bado mpo wengi humu Duniani sasa subiri!!...... vingi nevyo utubu haraka na Hadharani, kabla mda haujaisha!
 
Back
Top Bottom