Jinsi nilivyojinasua na mtego wa Al Shabaab

Watu wa Facebook bana kwani Lazima mucomement? Why msisubiri amalizie story? Walishazoeana Na wote Ni wa kike hutokea sana.Kama Dada tu naweza safari umbali mkubwa kumfuata Me hawajawai onana Ndo first date mnashangaa sometimes inatick sometimes no.That is lifeee.Tusibiri mwendelezo. Mamie wasikukatishe Tamaa vyeti feki wana Stress humu
Kweli wewe ni kiazi yaani unasafirishwa kama parcel,nategemea mwendelezo wa story yako utaonesha jinsi ulivyoingiliwa kimwili kwa nguvu huko kwa wasomali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa mwezi wa 11/2019 nikiwa zangu kwenye mitandao ya kijamii,hasa Instagram, kuna mdada alini-follow lakini nikamsoma jina ila sikumjua ni nani, nikahisi haya ni mambo ya mtandao kila mtu anajivinjari kwa raha zake.

Baada ya wiki moja yule mdada anaitwa Husna alinitext basi nami nikareply, basi tukaanza kuchat nikamwambia nipo Tanzania yeye akaniambia yupo Mombasa, tukawa tunachat kawaida kama marafiki wa mitandaoni na kupeana namba za WhatsApp.

Siku moja akanitumia SMS WhatsApp, akanambia kuna mchongo wa hela kama unaweza nikushirikishe maana huu mchongo hauhitaji pesa kutoka kwako yaani ni wewe tu, na wala si kazi ya kuuza mwili lah! Hasha ni kazi fulani hivi ya kufanya kazi kwenye kampuni ya Fulani hapa Mombasa.

Ghafla akanitumia picha zake akiwa kwenye nyumba fulani ya kiwango na gari akiniambia kutokana na kazi anayofanya kwenye hiyo kampuni ya usafirishaji sasa hivi ana magari 3 ya kutembelea, nyumba tatu za kiwango na moja ipo Tanga.

Baada ya siku kama tatu hivi akanitumia sh laki moja za Kitanzania kwa airtel money, na akanambia kwa vile wewe shost yangu kila wiki hasa jumamosi lazima anitumie laki 120000 ya kula, nikawa naanza kumwamini huyo mdada.

Tarehe 23 mwezi Desemba aliniomba niende tukutane Arusha, ila kwa sababu ya shughuli za hapa na pale nikamwambia fanya tarehe 3 January, basi akakubali, kama tarehe 28 hivi Desemba akanitumia laki 3 nauli.

Tarehe 1 nikawa Arusha, nilipofika Arusha nikamtext nimeanza safari, na yeye akasema basi na mimi ngoja nianze safari.

Kesho yake asubuhi akaniambia hawezi akaja Arusha mjini badala yake tukutane Namanga, nikakubali,akaniuliza kama nimefika Arusha mjini nikamwambia nimefika.

Asubuhi nikachukua usafiri nikafika Namanga, akaniambia nivuke boda niende upande wa pili, nikaenda tukakutana naye ila alikuwa na wadada wawili wenye asili ya kisomali, basi tukapanda kwenye gari lake tukaondoka kama km 2 hivi tukaingia hotel moja hivi.

Akaagiza supu ya nyama kuku tukawa tunakula pale basi tukizidi kufahamiana zaidi, akanambia wale wadada wengine ni marafiki zake wanaofanya kazi kampuni moja ila wao wanakaa Nairobi Estate Nairobi city.

Naye akanitambulisha kwao, akawambia ni rafiki yangu Mtanzania anakaa Mwanza kwa sababu ni rafiki yangu nataka tumuingize kwenye kampuni yetu si ndio jamani, wale wakaitikia ni kweli Manager hamna shida.

Tukiwa tunaendelea na ile breakfast Dada mmoja akapokea simu, akawa anaongea kisomali nikawa nasikia maneno kama Nairobi, Kisumayu na Lamu na salamu ya asalam allekhum.

Baadae wakaanza kuongea hicho Kisomali, nikawa najiuliza kwa nini hawaongei Kiingereza na huku ni Wakenya au Kiswahili lakini sikupata jibu.

Wakanigeukia mimi, mmoja anaitwa Ashura akaniambia sasa sister tutaenda Nairobi na wewe ili tukafanye mpango wa kukuingiza kazini, na ukishaingia kazini manager atakupa pesa utarudi Tanzania ili ufanye mpango wa kuhamia Mombasa kikazi, nikasema hamna shida.

Yule Husna akatoa nauli, akampa Ashura sh elfu 50 za Kenya akampa Aisha sh elfu 45 na mimi akanipa elf 30, yeye akadai kuna mambo anayaweka sawa hapo Namanga, ila akawambia kwa kuwa mimi sina passport inabidi nisiwe muongeaji sana kwenye basi, na mtu akaniuliza nisijibu, hao wengine watanijibia, nisiwe na wasiwasi.

Itaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe unaoneka unapenda safari nitakutumia tiketi uje IRAN Kutembea
 
Cute Love unapenda sana kusafiri safiri kuonana na memba mbalimbali wa JF dah!

Next time aisee ufunge safari uje tu unitembelee na mimi kwa sababu hakuna namna sasa

Ila uzi wako huu hapa chini ulinifurahisha sana siyo kama wa hawa wachovu wa Alshabab...Na una bahati sana kwa sababu wangekuwa watu wabaya wangeweza kukufanya cho chote wanachotaka. Wangekuwekea sumu kwenye chakula ukapoteza fahamu ungekuja kupata fahamu uko kwenye kambi zao Mogadishu. Jaribu kuwa mwangalifu na hizi safari zako za mara kwa mara kwenda kukutana na watu usiowajua...

Acha tu ,nimekoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom