Jinsi nilivyojifunza uchawi nikiwa ningali mdogo shuleni

Sina nia ya kudanganya chochote ila kupitia kisa changu cha ukweli kilichonikuta mimi mwenyewe jaribu kuzijua nyendo na tabia za mwanao asije kuharibika ama kuharibiwa.

Nilianza elimu ya msingi miaka ya 80 katikati ila nilianza kwa kuchelewa kwani kijiji chetu na vijiji jirani havikuwa na shule na pia mwamko wa elimu ulikuwa mdogo sana.

Nikiwa na miaka 11 nilichukuliwa na shangazi yangu ambaye alikuwa anaishi tarafani. Huko kulikuwa na shule na shughuli za kiserikali tofauti na kijijini kwetu.

Shangazi alinipeleka shule na kwa kweli darasa zima mimi ndiye nilikuwa mkubwa zaidi kwa umbo na umri.

Nilikuwa na vipaji vingi ikiwemo kucheza ngoma za asili, kucheza mpira nk.

Darasani sikuwa kubwa jinga, nilifanya vizuri sana. Licha ya kuanza shule kwa kuchelewa niliweza kushika kwa haraka na kuwapita walionitangulia.

Nilipoingia darasa la nne nilikuwa na umri wa miaka 15, nilikuwa nachezea timu ya shule ya mpira wa miguu.

Siku moja asubuhi tukiwa mstarini baada ya ukaguzi wa usafi, mwalimu akawa anaita barua, ukisikia jina la mtu unayemfahamu unamchukulia barua yake. Kijiji kizima hakikuwa na sanduku la pasta na wanakijiji wote walitumia anwani ya shule.

Barua zilikuwa nyingi na kuna barua mwalimu akaitenga na kuisoma mwishoni kabisa. Ilikuwa inahusu mechi ya kirafiki kati yetu na shule jirani iliyokuwepo katika kijiji kingine.

Baada ya kumaliza kuisoma mwalimu mkuu msaidizi akaagiza Myebusi Mweusi nimfuate ofisini kabla ya kuingia darasani.

Basi mimi nikatangulia ofisini kwa mwalimu mkuu msaidizi na akanikuta mlangoni.

Nilikuwa mvulana mwenye tabia njema, nilipendwa sana na wenzangu, walimu, wazazi na wote pale kijijini.

Mwalimu mkuu msaidizi alipofungua mlango nikamfuata na kuingia ndani ya ofisi yake. Akanikaribisha kiti kisha akaanza kunipa historia ya vijiji jirani kwa ufipi.

Miongoni mwa vijiji alivyonipa historia yake ni pamoja na kijiji ambacho wiki mbili zijazo tutakuwa na mechi nao.

Mwalimu mkuu msaidizi akaniambia kuwa kile kijiji ni cha magwiji wa uchawi na ndio maana wanaturoga ili shule yetu tusifaulu. Tangu uhuru hadi miaka hiyo shule yetu haikuwahi kutoa hata mtoto mmoja kwenda sekondari ya serikali.

Pia aliniambia kwa kipindi cha miaka yote hiyo hiyo shule haijawahi kufungwa na timu yoyote ya vijiji vya jirani. Hivyo basi akaniuliza je nina msaada gani kwa timu ya shule yangu?

Kwangu lilikuwa swali gumu sana, hadi nikakuna kichwa lakini sikupata jibu.

Nikiwa kwenye lindi la mawazo akanishtua, vipi uko sawa Myebusi? Nikajibu niko sawa.

Akakohoa kidogo kisha akaanza kunipa historia nyingine ya mganga mahiri aliyepo kijiji kingene mbali na kwetu, kama kilometa 50.

Akaniambia lazima twende kwa mganga yule tukachukue dawa ya kuizindua shule yetu kitaaluma na kimichezo ili tuwe tunafaulu sana na pia ili shule iwe inafanya vizuri kwenye michezo.

Akaendelea mbele, akaniambia wewe na akili zako zote hautafaulu darasa la saba kama hatujaondoa mirogo tuliyorogwa.

Akasema ataandika barua kwa shangazi kumjulisha kuwa naenda kwenye shindano la kitaaluma la mkoa sitakuwepo nyumbani kwa siku tatu, gharama zote zitalipiwa na shule, akaigonga barua muhuri, akaiweka kwenye bahasha, akalamba utepe wa gundi kisha akaifunga barabara, na kugonga tena muhuri nyuma ya bahasha. Akanipa niipeleķe nyumbani huku akinionya tena nisimwambie mtu kuwa twaenda kwa mganga, maana pia ni kwa faida yangu .

Basi asubuhi hiyo nikarudi nyumbani na barua mkononi, nikamkabidhi shangazi kisha nikaanza kupanga nguo zangu kwenye mfuko na madaftari matatu la hisabati, sayansi na Kingereza.

Kesho yake asubuhi safari ikaanza mapema. Tukapanda basi la ushirika wa wafugaji na safari ikaanza. Barabara ilikuwa ni lami tupu hadi kufika kijiji tulichokusudia.

Baada ya dakika 60 tukawa tunaremka. Tukatembea tukifuta barabara ya vumbi kisha tukachepuka na kuingia kweye njia nyembamba ambayo tuliifuata tukikatiza kwenye pori kubwa lenye miti ya mibamiba ya ki savanna.

Baada ya kama lisaa limoja tukaanza kuona kwa mbali mabendera mengi yenye rangi nyekundu , bendera zilikuwa nyingi kuliko zilizopo MSIMBAZI makao makuu ya Simba.

Tulifika na kukaribishwa na wasichana wawili wadogo, miaka chini ya kumi na nane, wakatuambia tuingie kwenye kibanda kimoja cha msonge tusubiri kuhudumiwa.

Kibandani mle uliletwa aina fulani ya uji wa mtama uliokuwa umechanganyikana na madawa, tuliambiwa tuunywe huo uji ili ututakase, kama tulikuwa tumerogwa, au tumelishwa kitu kibaya basi kianze kutoka chenyewe kabla hatujaonana na mganga.

Uji ulikuwa na ladha mbaya sana, pia ulikuwa na harufu isiyovumilika. Ninajihisi tumbo linanikoroga, nikaanza kujisikia kushikwa na tumbo la kuhara.

Nikakimbilia maporini, niliharisha sana na kutapika sana kwa zaidi ya dakika kumi hadi nikaishiwa nguvu kabisa. Nikachuma majani na kujisafisha.

Kwa kupepesuka nikarudi kibandani, ticha akaniambia umeona, wewe unarogwa sana, je umejikinga? Nikamuuliza kujikinga ni kupi, sijui. Nilikuwa sijawahi kwenda kwa mganga, sisi na ndugu zangu tumekulia kwenye familia ya kisabato.

Nilikuwa najisikia kiu kali, nimechoka sina nguvu na niko taabani. Nikaomba maji na binti mmoja kati ya wale wawili akaniletea mtungi na kata yake.

Nilianza kuyanywa maji kwa pupa, ticha akanizuia, akanisihi ninywe taratibu na kwa vituo. Nikanywa hadi nikamaliza mtungi mzima peke yangu.

Baada ya muda, tukaja kuitwa na mabinti twende tukaonane na mganga.

Tuliingizwa ndani ya kachumba kadogo kenye mwanga hafifu na harufu zisizoeleweka, famu, madawa, ubani yaani vurugu mechi.

Mganga akaanza manyanga yake na manyimbo ya ajabu akaanza kunitabiria akiwataja mababu zangu wa upande wa baba na mama, akaelezea mengi kuhusu ukoo wangu na ndugu zangu, kisha akaniambia "wakubwa" zake wamenipenda na wanataka wanilinde popote niendapo kwani nina nyota kali sana ya fedha, uongozi na mvuto hivyo bila ya ulinzi nitakuwa na vita kubwa sana.

Kwa muda wote niliokuwa kwa mganga, mwalimu mkuu msaidizi alikuwa bize na mganga, hatukuongelea mechi ijayo wala kuizidua shule, mimi ndiye nilikuwa mlengwa.

Niluchanjwa Chale mwili mzima, nililishwa madawa, na nikaambiwa nikalale nisitoke nje mpaka nitakapoamshwa.

Mabinti wakanipeleka kwenye kibanda kilichukuwa kando kabisa. Nikapewa ugali na nyama ya kuku, nikala nikashiba, nikalala fofofo kama nimepigwa nusu kaput.

Nilishtuka usiku mkubwa, pembeni yangu alikuwepo ticha na mganga wote wakiwa uchi. Mimi pia milikuwa uchi, sijui nilivuliwa nguo saa ngapi.

Mganga kwa usinga wake akanirushia aina fulani ya dawa wa maji, akanipaka dawa ya unga mweupe mwili mzima. Mganga akapiga mbinja kali sana, ghafla akatokea mbwa mwenye madoa tukapanda. Ticha mbele, mimi katikati a mganga nyuma huku akiwa amegeukia tunakotoka.

Mnyama yule alikuwa na kasi sana, ndani ya muda mfupi tukashuka katikati ya kusanyiko kubwa sana la watu.

Nikatambulishwa hapo, tukala nyamavza watu waliokuwa wavelets wakiwa wafu.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wangu, lakini nikaja kupanda vyeo hadi nikafika cheo cha juu sana. Nitakuja bkuwasimulia shughuli na wajibu wangu wa kila siku.

Sio kila mchawi anatokea kwenye ukoo wa kichawi
...Hujaenda kwenye Mkutano na ukatubu???....
 
Back
Top Bottom