Jinsi nilivyoibiwa pesa kwa kuahidiwa utajiri

Maybe2021

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
688
1,000
Wakuu salama! Mungu wetu mwema napenda kutoa stori yangu kuhusu jinsi nilivyopoteza pesa kwa kuahidiwa utajiri

Ilikuwa mwaka 2002 kipindi hicho nikiwa under 18 ilikuwa siku ya Jumapili basi Kama kawaida ya familia yetu tuna utamaduni wa kwenda kuabudu tulijiandaa mapema tayari kabsa kwa kwenda kanisani kwani kanisa halikuwa mbali Sana hvyo ilikuwa rahisi tu kwenda kanisani.

Niliamua kutembea kwenda kanisani nikiwa na rafiki yangu jina Zacharia bas tukiwa njiani karibu kufika kanisani tukaona watu wamekusanyika nikamwambia rafiki yangu Zacharia hebu tupite tuone hapo Kuna nini tulipofika pale tuliwakuta jamaa Kama watatu na mwanamke mmoja wanawaelezea watu kuhusu maswala ya kutaka kufanikiwa kwamba wao wanagawa utajiri kwa mtu yeyote aliyepo tayari basi kidume kimoyo moyo nikasema uwiii leo naboa nakwa kuwa akili na zenyewe zilikuwa za sungura nikawa Makin kusikiliza bas jamaa akauliza walio tayari kupokea utajiri wapite mbele ili wapewe dawa ili wapelekwe mahali bas kidume nikajitosa huku Zacharia akinizuia mimi nikamwambia nataka kuwa kama bakhesa.

BasI nikapewa dawa kwenye kiganja pamoja na wenzangu wasiopungua 50 hvi tukawekewa dawa kwenye kiganja na wale jamaa wanaojiita waganga kwa ajili yakuondoa umasikin baadaye wakatuambia bas saiv tunaenda tulipofika ili mkapewe masharti yakutumia hzo dawa kwa kila mtu kulingana na nyota yake ilivyo na wakatutahadhalisha hzo dawa Tulizopewa kwenye kiganja hutakiwi kizimwaga na ukizimwaga unakuwa kichaa bas jamaa wakatuongoza Hadi Gest walipofikia na wote tukaingia Kwan ndani ya nyumba hyo ya Gest kulikuwa na uwani mkubwa tu hvyo tulitosha wote tuliopewa dawa hizo.

Bas baada yakufika pale walipofikia tukaambiwa kuvua masharti na hapo wale jamaa wakawa wakali nikajisemea kimoyomoyo mmh maji ukiyavulia nguo shariti uyaoge bas wote tukatoa mashart nakuelekezwa kwamba hakuna kupiga kelele Wala kuongea chochote na tukawa tumepangwa mstari mmoja nakuambiwa tutakuwa tunaingia ndani mmoja mmoja ili ukapewe masharti yako ya Siri kwa ajili ya utajiri Kumbuka hapo tulikuwa watu wengi watu wazima na watoto.

Mmoja wa wale jamaa akatuambia ukiingia ndani baada yakusomewa masharti ukitoka nje tutamke neno hili ASANTE DOKTA na ukitamka hakikisha unatoa sauti Hadi wenzako ambao wapo kwenye foleni wanasikia! Na wale jamaa ukiwaangalia wapo smart Sana! Kimoyomoyo nikasema siwez kushindwa kutamka Hilo neno.

Bas zam ikaanza akaingia mtu wa kwanza mtu mzima mmoja akakaa Kama dakika tano hivi baadaye akatoka akatamka Hilo neno kwa sauti ASANTE DOKTA )ya furaha bas kidume nikajisemea kimomoyo jamaa kashatoboa hyo.foleni ikaenda Hadi mm nikafikiwa aise niliingia mle ndani na tambasam la kufa mtu.

Ile naingia tu nikasikia sauti inaniuliza Nan wewe bas nikajikakamua nikataja jina.
Swali lilofuata toa kila kitu ulichonacho ubaki na nguo tu tunapokusomea mashart ya dawa zetu mm nikajibu Sina kitu aiseeee wakati naongea hvyo nyuma yangu kulikuwa na mmoja wa hao jamaa akanitia banzi nakwasauti ya ukali inamaana wewe huna chochote ...kwa uoga nikamjibu Nina hela ya sadaka tu akasema mbwa wewe inamaana ukiambiwa toa kila kitu ulichonacho huwa unaelewaje bas kidume kwa uoga huku mkojo unataka kunitoka nikaitoa hyo sh Mia pamoja na saa!

Baadaye nikafungashiwa dawa za mitishamba namasharti nakumbka moja ya sharti Ni kutokuiangalia dawa hyo mpka nikifika nyumbn niiweke kwenye begi nanitaiangalia kesho yake na tayar zitakuwa pesa nanihskikishe naenda kuiweka kwenye begi au mfuko kwani Kama nitaweka kwenye begi bas begi hilo kesho yake asubhi litakuwa limejaa pesa.mm nikasema sitoweka kwenye begi nitaweka kwenye mfuko mikubwa hii yakunzia nafaka ili ziwe pesa nyingi

Itaendelea...
 

Maybe2021

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
688
1,000
Inaendelea sehem ya pili!

Bas kweli nilipofika nyumbn nilitafuta mfuko wa kuhifadhia nafaka kimyakimya nikaiweka hiyo dawa bila kumwambia mtu yeyote huku nikiwaza kesho nikiamka tu nitachukua pesa zangu zote nakuzipeleka bank kwa usalama wangu na baada ya hapo nitafanya mpango niwe nafanya biashara yakuuza magari, hapo Nina furaha balaa! Yaan najisemea napata utajiri kwa kuwaachia sh 100 na saa.bas dawa yangu nikaiweka nakukaa kimya.

Ilipofika saa moja jion Zacharia akaja nyumbni kuja kufuata saa yake ambayo alikuwa ameniazima siku hyo tunaenda kanisani bas akaniambia aisee nimefuata saa yangu nikamwambia saa ipo atakuja kuichukua kesho bas kwa kuwa tulikuwa marafiki wa mda akanielewa na akaniuliza vp kule mlienda mmepewa pesa?

Nikamwambia bwana mm hata sikufanikiwa kufika nikiwa njian tunaenda kwenye eneo walipofikia niliteleza nakudondoka hvyo nilikosa sifa maana nilimwaga dawa zao yaan nilivunja mashart yao bas jamaa akanicheka nakuniambia yeye baada yakutoka pale alienda kanisani hata hvyo alifika amechelewa.bas baada ya stori mbili tatu Zacharia akaondoka .na mm nikajisemea ee kesho atakuja kunikuta nishakuwa tajiri kuhusu saa yake nitamnunulia maana nitakuwa na pesa zakutosha.

Bas Giza likaingia tukalala mm usiku mzima nawaza hzo pesa hata usingizi haupiti hatimaye kukakucha ilipofika saa moja tu nikausogelea ule mfuko nilipoweka dawa zangu kuushika hvi mfuko upo vilevile nikajisemea kimoyomoyo labda muda bado mpka mchana itakuwa tayar.

Itaendelea soon.
 

Maybe2021

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
688
1,000
Inaendelea sehem ya pili!

Bas kweli nilipofika nyumbn nilitafuta mfuko wa kuhifadhia nafaka kimyakimya nikaiweka hiyo dawa bila kumwambia mtu yeyote huku nikiwaza kesho nikiamka tu nitachukua pesa zangu zote nakuzipeleka bank kwa usalama wangu na baada ya hapo nitafanya mpango niwe nafanya biashara yakuuza magari ,,,,,hapo Nina furaha balaa! Yaan najisemea napata utajiri kwa kuwaachia sh 100 na saa.bas dawa yangu nikaiweka nakukaa kimya.

Ilipofika saa moja jion Zacharia akaja nyumbni kuja kufuata saa yake ambayo alikuwa ameniazima siku hyo tunaenda kanisani bas akaniambia aisee nimefuata saa yangu nikamwambia saa ipo atakuja kuichukua kesho bas kwa kuwa tulikuwa marafiki wa mda akanielewa na akaniuliza vp kule mlienda mmepewa pesa? Nikamwambia bwana mm hata sikufanikiwa kufika nikiwa njian tunaenda kwenye eneo walipofikia niliteleza nakudondoka hvyo nilikosa sifa maana nilimwaga dawa zao yaan nilivunja mashart yao bas jamaa akanicheka nakuniambia yeye baada yakutoka pale alienda kanisani hata hvyo alifika amechelewa.bas baada ya stori mbili tatu Zacharia akaondoka .na mm nikajisemea ee kesho atakuja kunikuta nishakuwa tajiri kuhusu saa yake nitamnunulia maana nitakuwa na pesa zakutosha.

Bas Giza likaingia tukalala mm usiku mzima nawaza hzo pesa hata usingizi haupiti hatimaye kukakucha ilipofika saa moja tu nikausogelea ule mfuko nilipoweka dawa zangu kuushika hvi mfuko upo vilevile nikajisemea kimoyomoyo labda muda bado mpka mchana itakuwa tayar.

Itaendelea soon.
Inaendelea sehem ya tatu

Wakuu labda niseme tu hapa silazimishi mtu kusoma Ila hiki ninachokisimulia hapa kilishawahi kunitokea!
Tuendelee bas muda ukafika saa sita mchana nikatudi Tena kuangalia Kama mzigo umeshajaa lakin nilikuta upo vilevile tu dah nikajisemea mmmh hapa nitakuwa nimekosea masharti ngoja niende kwa wenzangu tuliokuwa nao!

Bas nikaenda kwa jamaa mmoja jina makima nikamuuliza vipi Ile Mishe yetu ya kwa ASANTE DOKTA ameshaichek alipowka akasema hamna kitu chochote alichopata na akanipa stori kwamba siku hyo yeye alikuwa anaenda kununua mipunga kijijin hvyo alipoingia kwenye kile chumba Cha asante doktar walimwambia atoe kila kitu hvyo pesa zote ambazo alikuwa nazo aliacha mle nikamuuliza kwani ilikuwa shiling ngap akaniambia Ni lak 525000/ nikashika kichwa nikamshaur twende tukawaangalie maana hata mm walichukua pesa yangu ya sadaka Kia's Cha sh 100 pamoja na saa yangu na yeye akasema tukampitie na jumanne tuone na yeye yametoa majibu gan bas akanibeba kwenye baiskel Hadi kwa jumanne tulipofika tukamuuliza vp majibu ya asante doktar kwako! Naye alijibu hakuna chochote hvyo tukawa watu watatu tukakubaliana kwenda Hadi wapofikia kwenye Gest hyo! Yaan kwa ASANTE DOKTA

Bas Safari ikaanza tulichukua Kama dakika chache tu tukafika tukamuuliza yule mhudumu wa Gest ile vp dokta tumemkuta akasema dokta ameshaondoka kaenda kigoma kikaz Kuna watu walimwita, Bas tukiwa pale tunajuliuliza Cha kufanya wakaja wengne wanne na wao wanamuuliza doktar makima akawauliza Wana shida gan na doktar? Wakamwambia kwamba aliwapatia huduma lakin bado hawajaona matunda kimoyomoyo nikasema mmmh Hawa watukuwa wamepewa huduma Kama yetu

Bas tukaanza kuulizana Kias gan na vitu walivyochukuliwa wale watatu mmoja aliacha sh 5000/ mwingne 34200 na mwingne 10900/ bas tukashauriana tuchange nauli ili mmoja wetu amfuatilie kwani aliacha namba ya simu amfuate hukohuko kigoma..kumbka mm hii inshu nilifanya Siri hakuna yeyote anayefaham nyumbn bas wenzangu kwa kuwa walikuwa watu wazima walichanga na hatimaye pesa ilipatikana ya kwenda kigoma!

Baada ya pesa kupatikana mmoja wetu akatoa wazo kwanini asitumiwe hyo pesa yeye dokta ili aje kutuhudumia hukuhuku nyumbn hatimaye mwafaka ukapatikana kwamba atumiwe pesa kwa njia ya bus na kweli pesa zikaenda na baada ya siku kadhaa alikiri amepokea pesa hzo nakaahid atakuja watu tukakaa kusikilizia,

Baada ya siku Kama mbili hvi Zacharia akaja Tena nyumbn kufuatilia saa yake nikajisemea hapa bila kuwa msiri sitoboi nikamwambia rafiki yangu Jana wakati nachota maji saa yako ilidumbukia kisimani hvyo nitakununulia nyingne tu mda huo kimoyomoyo nikasema doktar atarud nakunifanya tajiri saa haiwez kunishinda!

Itaendelea.....
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
32,059
2,000
Vile team konda msafi wanawahi kwenye huu uzi kuja kudai kuwa hii stori ni fake na imetolewa kwenye kitabu cha darasa la pili cha hadithi za watoto!
2021041122000.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom