Jinsi Nilivyofedheheka: ....ikawa mwisho wa UKUWADI wangu....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Nilivyofedheheka: ....ikawa mwisho wa UKUWADI wangu....!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by gambachovu, Mar 10, 2012.

 1. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa kijana niliyehitimu kidato cha nne mwaka 1990. Baada ya kusota bila kazi kwa miaka mitatu(3),nilikuja kupata kwenye kampuni moja ya Wahindi jijini Dar.
  Katika kampuni hiyo,palitokea mtoto wa bosi mwenye kampuni kunipenda na kuelekea kunizoeazoea.

  Wakati wafanyakazi wenzangu wa Kiswahili wanatoka yeye alipenda kuniambia nibaki,huku akisema kama nina haraka basi naweza kwenda. Nami kwa woga wa kuwazoea mabosi,naondoka.

  Siku moja aliniambia nibaki,la kushangaza silijui hata ni kwanini safari hii sikukataa. Baadaye,tulikaa ofisini hadi takribani saa 12 jioni,ndipo nilimsaidia kufunga ofisi. Akanituma nikachukue taxi maana aliniomba nikamsindikize mahali.

  Baada ya kupanda kwenye taxi ile,akamwambia dereva kuelekea Tandika. Nikajawa na mshangao,bosi wa kihindi anatafuta nini Tandika? Naona alinielewa,akawa anasema,"..hapana sema juu ya hii safari..mi mependa veve rafiki yangu,tunza siri..."

  Tulifika mahali penye kituo cha mafuta,akamwambia dereva atafute pa kupaki. Haikuchukua muda mrefu,akatokea dada mmoja ninayemfahamu,akafika na kumpa mkono,akachungulia zaidi ndani ya gari,akaniona,alinisalimia ingawa hakufurahia kuniona.
  Yule dada anafanya kazi kampuni nyingine kama mesenja,na huwa anakuja pale ofisini kwetu kwa kukabidhi na kupeleka vifurushi.Ukweli ni kwamba dada yule hata kama ni mapenzi,hakuwa wa kutembea na kijana yule wa kihindi. Hakuwa na mvuto hata kidogo!

  Tulikaa kwenye baa moja ya jirani na kuagiza vinywaji baridi. Mpaka muda ule sikuwa nimeelewa maana ya kuniita pale. Baadaye walinong'onezana na walipomaliza,yule bosi akatoa noti kama kumi hivi akampatia dada yule.
  Wakati wa kurudi alinipa kama sh 5,000/-

  Kesho yake akaniomba nibaki tena.
  Nilibaki,na akaniambia yeye anapenda wasichana wazuri wa Kiswahili. Na yupo tayari kugharamia matumizi hadi ampate. Kwa hiyo akanielekeza kwa dada mmoja wa kampuni jirani,kwamba nimuunganishie. Kwa kazi hiyo alinipa Sh 15,000/-

  Nilichuku elfu 5 nikaweka nyumbani. Nikajua elfu kumi itanitosha.. Kwa umahiri wangu wa kuongea nilifanikisha kumfikisha hoteli ambako alikutana na bosi,mi nikapewa posho nyingine ya sh 5,000/-.

  Kesho yake alinisifu sana kwamba mi hodari.
  Baadaye ikawa kama ndiyo kazi yangu,kwani ilikuwa inanipa kipato kuliko kazi niliyoajiriwa! Nilianza kupendeza kupitia kumkuwadia mabibi mtoto wa bosi! Sikuwa na shida ya hela ndogondogo.. Kuna wakati nilipanga kuandaa mazingira kuchukua hela nyingi kwake kwa mtindo huo kisha niache kazi.

  Ni kuhakikisha katika wiki kuna wanawake walau wawili wa kuwafukuzia,ambao mpaka wiki inayofuata watalala na Mhindi wangu. Wakati mwingine naomba fedha nyingi za maandalizi ya kumtafuta na kum-intertain msichana hadi kumfikisha hoteli nako nalipwa tena.

  Siku moja niliamua kumuingia dada mmoja ambaye huwa tunakutana kituo cha basi cha Posta mpya. Alinishangaa kidogo,lakini akasema kwa maongezi zaidi,niende kazini kwake kesho yake mitaa ya Oysterbay.Alikuwa zamu ya mchana,hivyo ilibidi kutafuta uongo ili nikatimize ahadi,maana dada alikuwa hotelier.

  Alinipokea vizuri na dada alikuwa mrembo kweli. Nami niliomba hela nyingi za "promo" kwani nilimsisitizia huyu wa safari hii ni baab kubwa. Nikala lunch na kunywa. Baada ya kumwaga sera zangu,alionekana kushangaa,mshangao ambao sikuupenda..
  Kisha akaniambia"Mbona we ni kijana handsome tu,ya nini utumike na mtu namna hiyo?" nilijibaraguza sana,ingawa sikuweza kuukwepa ukweli kuwa tabia ile si nzuri.
  Akasema atanipa jibu kesho yake.

  Tulipokutana akasema amekubali,na kwa kuwa anapenda kutunza heshima yake,basi huyo "bwana wake" achukue chumba,kwenye hoteli moja ya ghorofa,maeneo ya River Side.

  Bosi kawaida alikuwa anatangulia,mi nikamchukua dada yule hadi chumba alichokuwa bosi wangu. Nikawatambulisha na kabla sijapewa bahasha yangu ili niondoke,paligongwa hodi.

  Nikaona ngoja niwasikilize kwanza wahudumu. Nilipofungua,nilishangaa kuona majibaba matatu! mawili ya miraba minne..Moja likaingia kabisa,lingine likaingia na kubaki linaulinda mlango mtu asitoke..
  "inaonekana umezoea kazi ya ukuwadi,sasa utakoma!!" aliongea yule mwembamba nadhani mume mtu. Wakati huo Mhindi naye jasho linamvuja..akaniruka kimanga kuwa alishaniambia hataki wake za watu. Wakaliona briefcase wakalifungua ambako ndani yake mlikuwa na minoti mingi sana!

  Kabla sijakaa sawa,nilipigwa mtama ambao sijawahipigwa tangia nizaliwe! Nilirushwa juu sana,kabla sijatua,suruali ilikuwa tayari ishararuriwa! Mengine nadhani msomaji unaweza kuhisi kilichoendelea...
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Khaaaa! Gambachovu!!
   
 3. S

  SI unit JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .
  Pole nyingi zikufikie kwa kupata dhahama ya kuraruliwa marinda yako..
   
 4. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Pole kaka kwakweli si tabia nzuri
   
 5. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Heeh kwahiyo... wakakunaniliu.. Oh POLE SANA!
   
 6. S

  SI unit JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .
  Drive slowly, men at work of DAVID CAMEROOOON
   
 7. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ok......
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  waliku-cameron?
   
 9. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Hilo jibu.
   
 10. Gabmanu

  Gabmanu Senior Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya mtama kilichoendelea ni mangumi ya tumbo,mateke ya kichwa n.k
  pole sana nafkiri ulikoma.
   
 11. s

  shosti JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hahahahhha kwan hiyo ukicheka unahema?
   
 12. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Hii imekaaje tena? Is it really?
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  uwiiiiiiiiiiiii kwa hiyo washaharibu?
   
 14. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Inamaana walikula jicho ?
   
 15. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Hahahah kaaazi kweli kweli!
   
 16. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Maskini walikua Mobitel ya Baaz, mtandao wenye promo nyingi .
   
 17. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kilichoendelea hapo kwa mtazamo wangu waliku CAMEROON. Ila ni mtazamo wangu tu.
   
 18. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni copy and paste kutoka katika magazeti ya Mshauri wako/Jitambue!
   
 19. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,681
  Likes Received: 871
  Trophy Points: 280
  dah..!! Inamaana kijana wa watu alitolewa bikira siku hiyo..!! Nampa pole sana.
   
 20. vanmedy

  vanmedy JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 2,245
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Daah bila shaka walikula kiboga wewe na muhindi wako na briefcase wakaondoka nayo..
  USIJALI USIPOCHAFUKA UTAJIFUNZAJEE
   
Loading...