Jinsi nilivyofanikiwa kutengeneza Sh. Milioni 19.9 ndani ya siku 35 kwa kutumia Milioni 3.8

Salute!

Nimefurahi sana kurudi tena JF baada ya kukatika kwa muda kiasi. Wengi mlinizoea kule 'Jamii Intelligence' na thread zangu za kusisimua za 'money hunters', na nilitoa ahadi ya kuwaonesha baadhi ya fursa za pesa ambazo wengi huzipuuza either kwa dharau ama kwa kutokuwa na taarifa sahihi.

Binafsi nina msemo wangu "If you're on the rise towards success, don't leave others behind - it can be boring being alone up there!" - "kama upo safarini kuelekea kwenye mafanikio, usiwaache wenzio nyuma, uwapo juu pekee yako panaweza pasinoge". Hivyo hua najisikia faraja sana kuShare fursa na ndugu zangu wa karibu - Jamii ya JF ni kama familia moja, tunatofautiana mitazamo lkn siku MaxMello akiguswa wote tunapaza sauti km familia kwa umoja hadi kieleweke.

Upana wangu wa biashara - kwa ufupi tu

Ifikapo trh 27 Nov mwaka huu nitasherehekea rasmi miaka miwili tangu nianzishe kampuni yangu binafsi - tuseme kijikampuni.

Nikiwa chuo UDSM, mimi na class yangu tulikuwa intake ya kwanza kabisa kusoma mojawapo ya course mpya kabisa Tanzania ya Gas na Mafuta. Mapema kabisa machale yalinicheza kuwa course hile yaweza ikawa imeanzishwa kisiasa hivyo kuna uwezekano mkubwa hata future yake isiwe ya kuaminika. Hivyo nikaona ni vyema nianze kuchonga njia ili siku nikianza rasmi kuipita nisiishie kwenye miba.

Yani niseme nilitumia 70% ya muda wangu wa chuo kufanya biashara nje ya masomo. It's wasn't easy balancing the two, but that was the only option I had. Kwahiyo nilizidi tu kujikita kwenye mipango ya biashara, chuo nikawa nadonoa donoa.

Mambo yalikuwa upande wangu kiasi, changamoto zilikuwa ni nyingi sana, ups and downs, vyote hivi havikukwepeka, lakini mwanga niliuona kwa mbali - sikurudi nyuma. Nikiwa mwaka wa 2, biashara ilininyookea sana, sijui ni bahati ama jitihada lkn kiujumla niliExperience 'super exponential growth'. Mwezi wa 10 nilabahatika kutoka nje ya E. Africa kwa mara yangu ya kwanza - nilienda Jozi. Kiufupi nilichaguliwa kama mmoja wa mjasiriamali bora Africa mwenye umri mdogo chini ya miaka 22 ( wakati huo nikiwa na miaka 21).

Tuzo hii ilikuja na fursa nyingi sana - tuseme ikanifungulia chemchem ya mafanikio. Nikaweza kusafiri nchi nyingi za watu (Russia, Morocco, England, France, USA), nikakutana na watu influential, nikapata networks za biashara, Donors, media exposure. Yani niseme hii tuzo ilikuwa ni 'point of no return'. Tufupishe ufupisho, hapa biashara yangu ikakomaa zaidi, nikaanza kuona matunda, ndipo nilipoamua kuisajili kampuni yangu kisheria. Mpk kufika hatua hii, biashara yangu iliweza kujiendesha na faida ilikuwa ni ya kuridhisha.

Changamoto ndogo tu niliyoibadili kuwa fursa ya kibiashara kwangu

Katika operations zangu za kila siku za biashara niligundua kuna changamoto 1 inayoniathiri sana, kuanzia muda, nguvu, morali ya kazi na hata pesa. Na changamoto hii iliwaathiri wengine ambao wapo kwenye biashara yangu.

Nikaona mbona kitu chenyewe ni kidogo tu, na kinatutesa hivi. Kwanini nisitafute uwezekano wa kutatua hii changamoto ili kila mtu kwenye cycle yangu afanye biashara yake kwa ufanisi zaidi - why don't I turn black into pink at same time nigonge pesa nzuri tu ya ziada.

Nikasuka ramani nzima ktk karatasi - from A to Z, kilichobaki ni utekelezaji tu. Nilikua naingia kwenye kitu kipya kabisa ambacho sijawahi kukifanya ktk operations za kampuni yangu, hivyo nilikuwa makini sana kuepuka kuchoma pesa kizembe.

Mwezi Aug 2016 ndio rasmi nilimaliza masomo yangu, kwahiyo nilikuwa na muda mwingi zaidi wa kufanya shughuli za kibiashara. Hapa kati nikawa na visafari safari vya nje - lkn Oct nilisettle rasmi.

Tuendelee...

Utekelezaji ukaanza | Kiteto-Manyara trh 22 Jan 2017

Nilidraft kuanza kufanya huu mchongo mwezi wa pili, hivyo maandalizi niliyaanza mapema kukwepa usumbufu ambao ungejitokeza.

Trh 22 Jan nikafika sehemu 1 inaitwa Matui, huko Kiteto mkoani Manyara. Kikubwa kilichonipeleka Kiteto ni kutafuta uwezekano wa kukodi trekta la kulimia ambalo nilipanga kulitumia mkoa wa Pwani.

Tarehe 23 nikaibukia ofisi za Kata ya Matui kuongea na wazee kuhusu mpango wangu, hapa nilipata dira. Nikaelekezwa kwa mkulima ambae anamiliki matrekta lakini ameacha shughuli za kilimo.

Nilimfikia yule mkulima, alikuwa ana Massey Ferguson 690 Turbo, ilikuwa imechoka kiasi. Yule mzee alidai angeweza kunikodishia kwa mil 4 - kutokana na uchakavu nikamkomalia anifanyie kwa mil 2 na ningeirudisha ikiwa safi kabisa (kama mpya). Yule mzee akakubali, tukaandikishana ofisini, akabaki na kadi.

Baada ya makabidhiano, nilimsaka fundi mzuri na hatimaye trh 27 nilimpata akaanza kazi. Pale jumla ilinitoka laki 7.2, tulibadili vitu vingi sana mpaka chombo ikawa freshi.

Dereva nilimpata kulekule, kijana mmoja makini sana wa kigogo, alikua anachoma wida lakini ikifika muda wa kazi 'anasimamia ukucha' adi unampenda bure.

Tarehe 30 saa 10 jioni tukaanza safari kutoka Matui kuitafuta Moro. Nilipendekeza kusafiri usiku ili kupunguza usumbufu wa barabarani na matraffic. Moro tukafika kesho asubui ya saa 4.

Ile trekta ilikuwa ina jembe la 'chapa samaki' lakini disk zilikuwa zimeisha. Basi kufika Moro tukapaki kisha nikaenda kununua disk (hizi ni zile sahani za kulimia), pale ilinitoka 570k pamoja na vifaa kama bolts, grease na service ya kuchomelea vyuma vilivyolegea

Kufikia hapo tayari lile trekta lilikuwa lipo tayari kwa ajili ya kazi. Roho yangu ilisuuzika sana sana. Tukapumzika na dereva wangu pale Msamvu hadi usiku saa 5, kisha tukaanza safari ya kuitafuta Chalinze, then baada ya Chalinze tuingie Msata. Tulifika Mandera saa 12 asubui ya tarehe 1 Feb. Safari nzima kutoka Kiteto hadi hapa Mandera ilinigharimu 310k. Hivyo kwa jumla nilikuwa nimetumia 3,580,000.

107e372c495ccb2e884b5cbcbab63711.jpg
service ndogo ndogo zikiendelea.

Hapa Mandera ndio nilipanga pawe kituo changu cha kazi, tayari nilishafanya utafiti wa kujiridhisha kuwa biashara itakuwepo hadi nitaikimbia. Baadhi ya wateja tayari nilishawaandaa. Trekta ilivyofika tu, nikaingia ofisi za kijiji nikajitambulisha, wazee wakanipokea kwa bashasha kabisa, wakanikaribisha na kunipa 'go ahead'. Nikaona si mbaya niwape hela ya soda, nikachomoa 55,000 wakagawana. Jumla nikawa nimetumia approximately 3.7 mil.

Kazi inaanza rasmi

Keshowe tarehe 2 kazi niliianza rasmi biashara niliyoipanga kwa muda mrefu. Nilikuwa nalima hekari 1 (70m x 70m) kwa 50,000 - 60,000 kutegemea na usafi/uchafu wa shamba. Asubuhi saa 11 tuliamkia hekari 5 za mwenyekiti wa kijiji. Dogo Mzuzu (Dereva wangu) aliseti jembe kwa ufasaha kabisa, akapiga kete 1 kisha akakamata chombo. Saa 3 asubuhi kazi pale iliisha, dogo alilima vzr sana kama nilivyokuwa nataka yani 'kumwaga unga au kushona mkeka' (wakulima watakua wananisoma) - yani hapa shamba linalimwa linakuwa kama uwanja wa mpira, linanyooka flat kabisa bila tuta/mfereji, ni unaweza kusema limepigwa 'Harrow'.
e852643df3efbee3618b054832a3fca5.jpg

Kumaliza hapo tukawa na mteja mwenye heka 12. Ni kijiji cha jirani kinaitwa 'Mungu atosha' - pale tulianza kama saa 4:30 asubui. Dogo mzuzu kama kawaida, akashtua kidogo kisha akaingia mzigoni, pale tuligonga hadi saa 6 usiku. Sikuamini kama tungelimaliza lile shamba.

Mimi 'expectations' zangu zilikuwa tulime wastani wa hekari 10 kwa siku. Nilishangaa sana kuona tumeweza kulima hekari 17, japo tulipitiliza muda wa kazi ambao tulijipangia. All in all dogo alikuwa yupo motivated sana. Hii siku ya kwanza nilipiga 910,000, kisha nikatoa 93,000 ya mafuta coz kuna mafuta yalibaki kwenye tank wakati tunasafiri ndio tulianzia zile heka 5.

Makubaliano yangu na dereva yalikuwa nimlipe 4000 kwa kila hekari atakayolima, lakini baada ya kuona utendaji wake, nikampandishia hadi 5000 kwa kila heka 1. Hii siku dogo aligonga 85,000 - ilimpa sana morali ya kazi, tukawa marafiki hasa ukizingatia tulikua ni watu wa rika 1, so hapo hakuna boss wala nini, coz hata utingo nilikua nakomaa kibishi. Degree ya gas na mafuta tupa kule. Hii siku baada ya kutoa gharama zote nililaza 708,000. Nami niliopata motisha sana ya kuchapa kazi.

Keshowe pia tukakomaa tukagonga hekari 14, nikalaza 498,000 na kesho kutwa tukagonga heka 13. Bado tulikuwa tuna pumzi 'ya kufa mtu' - mimi na dereva wote tuna njaa ya pesa.

Tukaja tukalamba bonge la deal, tuseme 'jackpot'. Kuna afisa wa Jeshi wa JWTZ alikuwa ana hekari 170 maeneo ya Lugoba ndani ndani kabisa kijiji cha kioma. Huyu mzee alipata taarifa kutoka kwa mdogo wake ambae tulimlimia shamba lake. Tukaelewana 55000 kwa kila heka coz shamba lake lilikuwa jipya (yani linalimwa kwa mara ya kwanza), yule mjeda wala hakuwa mtata tofauti na 'wanajeshi uchwara'.

Kwanza tukaenda msata mjini pale, tukapiga service ya nguvu, piga vyuma vya kutosha, oil, grease, kaza kila chuma. Yani tulijiandaa 'kamili gado'. Tukaingia mzigoni. Niliamua sasa kutafuta utingo wa kumsaidia dogo Mzuzu ambae yeye nilimlipa 12,000 kwa siku. Yule askari akaniita Pub ya kambini pale juu ya mto wami, tukapiga story nyingi sana za maisha - he was so much proud of me. Kimahesabu ilibidi anilipe 9,350,000 lkn yeye alinipa 9.5 mil. Siachagi hela mimi , tena akanipa cash. Nikachukua gari hadi chalinze nikatia bank mil 7 nikabaki na 2.5 kwa ajili ya mafuta, repair, posho ya dereva na utingo pa1 na gharama za kujikimu. Nilishapiga hesabu kua dereva atapata 880,000 na mafuta itakuwa 1,400,000. Hizo chenji ndio zilikua 'miscellaneous'.

Kazi ilianza, ratiba ilikuwa ni kuanzia 11:30 alfajiri hadi saa 2 usiku. Na tulitegemea tufanye kazi kwa siku 17 lkn dogo aligonga siku 13 tu. Dogo huyu ni balaa, tukaanza kumwita 'bulldozer' - ukimpa sifa ndio anagonga gear kama hana timamu.

Hakuna kulaza zege - chai haichachi

Wazungu wana kamsemo kao kwamba "Life begins at the end of comfort zote". Niliona hii fursa tamu 'mpaka kisogoni', nikaamua nitoke nje ya 'comfort zone'. Nikawaaga wale vijana wangu kuwa nitatoka kwa siku 6, wao waendelee tu na kazi - uzuri walikua wanalala na kuamkia pale pale shambani kwa mjeda, hivyo sikuwa na presha yoyote.

Mimi nikakimbia chalinze kwenda benki, account ilikuwa na 9.4 mil nikachomoa 4.4 mil, nikakimbia kiteto. Wao huko kiteto shughuli za kilimo zilishaanza kuisha, so matrekta yakawa yanapigwa 'doro'. Kuna tajiri mmoja alikuwa ana mahindra HP 75, iko vizuri afu mpya kabisa, watoto wa mjini wanasema - imenyooka. Akataka 5 mil kwa mwezi, mimi nikalia nae pale nikampa 3.9 mil.
bd83894f7fd8940cd01b5c31e0a19c95.jpg

Hii haikuwa na milolongo ya repair, so tuliandikishana pale na tayari nilikuwa nafahamika pale ofisi ya kata wala haikuwa na asumbufu. Ilikuwa ni kufika na kuondoka, nikapata dereva ambae niliunganishwa na Dogo Mzuzu, kama kawaida tukaanza safari. Jumla ya mizunguko yote hii nilichukua siku 3 tu.

Nikafika Msata yule mjeda akaniunganisha na jamaa yake mkulima, yeye alikuwa Miono kijiji cha machalla, huyu jamaa alikua ni mtu wa TRA Bagamoyo nahisi. Yeye alikua ana hekari 148 machalla na 87 kwa msisi kama unaelekea Tanga - pia tulimlimia kwa 55k.

Sasa nikawa nasimamia trekta 2 zote kwa pamoja. Kazi juu ya kazi yani 'bampa to bampa'. Hakuna kupumzika zaidi ya Jumapili. Tukimaliza hapa tunaitwa hapa, tukawa hadi tunagombanisha wateja.
4df3148fd418647a98a8c9851e72b0a9.jpg

Kazi tulipiga kuanzia kwa Makocho, Chaula, Pongwe, Miono, Machalla, Kimange, Lugoba, msisi, manzese, msata hii barabara ya kuingia bagamoyo (hapa katikati sasa). Yani kwa kifupi niligonga kazi kama mtumwa. Haikuwa rahisi kusimamia trekta zote 2, lkn hakukuwa na room ya kujifanya nimechoka. Siku 4 bila kuoga halikuwa jambo la kustaajabisha. Kuna hii jinzi ya kazi, niliivaa hadi ikawa imekakamaa kama gazeti. Kazi tulipiga hasa, vijana wale wakaanza kuchoka, nikawa natafuta madereva wa pembeni 'day worker' - kwahiyo dereva wangu nampa mapumziko huku mimi nafukuzana na madeiwaka.

Pia nilipata mwenyeji mmoja ambae nae tuseme alikuwa kama msaidizi wangu, kuniongoza mashambani, kunitambulisha, usimamizi nk. Huyu nilikuwa nampa 2000 kwa kila hekari tutakayolima - kwa siku kule vijijini kulaza elfu 20-30 ilikua ni 'kismati' sana, so huyu mzee alikuwa motivated vibaya mno.

Niligonga kazi Feb yote, saa zingine nilikuwa nachomoka hata siku 3 kuja kusimamia shughuli za kijikampuni changu, na mambo mengine mfn nilikuwa nafanya documentary na Deutsch Welle (DW TV) ambayo tumemaliza rasmi Jana.

Kazi za shamba kuelekea hii March zikaanza kupungua, nikarudisha hile tractor ya kwanza ambayo niliitumia kwa siku 35, na hii Mahindra nikairudisha baada ya kuitumia kwa siku 29.

Mizunguko yote ya hiki kiproject cha mwezi 1 kiliniingizia jumla ya Mil 23.7, na niliingia nikiwa na mil 3.8. So, niligonga 'net profit' ya 19.9 mil ndani ya wiki 5 tu. Kwanza nikachomoa laki 9 nikaenda zangu Prison Island, Zanzibar kujipongeza, maana ule msoto wa siku 35 haikuwa wa 'hapa na pale'.
a89c4e67ac2dba7c797837e20737d2da.jpg

Mbinu 'zangu' rahisi za kutusua

1. Dirisha 'kubwa' la usajili.

Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa ligi za mpira za ulaya, sana sana EPL na La Liga. Timu yoyote imara ni ile ambayo 'dilisha la usajili' likifunguliwa wanazama sokoni mapema, anachukua vifaa -quality players, wanaimarisha kikosi. Hii hutokea mara 1 tu msimu mzima wa ligi. Timu isiyosajili vzr kama timu yangu Arsenal inamaliza msimu ikiwa kibonde - nyweshwa goli 10 kipuuzi puuzi tu.

Maisha nayo yako vivyo hivyo, mara chache sana maisha yanakufungulia pazia la dirisha la fursa, fursa zinamwagika, nyingi sana. Watu wengi hupotezea, hawa ndio wale wanaishia kunyukwa bao 10, hawa ndio wanabaki kutukana kina bashite, hawa ndio mwisho wa msimu wanakua vibonde wanashuka daraja.

Lakini kuna wale wanaoamua kujilipua, akiona fursa anafuta dhana zote na hofu ya kupoteza (fear of failure), wanazama dirishani wanajipakulia fursa, hawapo tayari kucheza kamari na maisha, watu hawa wana slogan 1 - life is too short to take little shots. Hawa ndio mwisho wa ligi unakuta kanyakua UCL, anaingia mtaani kunyimwaya mwaya.

Kumbuka dirisha hufunguliwa mara chache sana, likifungwa hua ni ngumu sana kulifungua. Inabidi usote kwanza ukiambulia vichapo hadi baadae litakapofunguliwa.

Mimi kwenye suala la kuchangamkia fursa hua 'sinaga ushemeji'.

2. Mafanikio yanalemaza sana - kuwa makini.

Nimekuja kujifunza kuwa hakuna kitu kinapumbaza maishani kama mafanikio. Mafanikio siku zote yanampa mtu kiburi, maringo, majivuno, mtu anajisahau, mtu anajipenda kuliko kiasi. Mafanikio yanamfanya mtu aache kuwa mbunifu, mchapa kazi, yanamfanya mtu aridhike na asitoke nje ya box.

Kuna kaka yangu huko 'celebrity forum' naona saa zingine mnamjadili. Kaenda Joburg, kalamba bingo kama $300k, haya ni mafanikio makubwa sana kwa umri wake (hii ni kama mil 600+). Lkn ona mafanikio yalivyompumbaza, akalewa mpk akalemaa akili. Kashikwa shikwa kidevu na le mbebez, kapakwa shombo saivi yupo hoi (no disrespect).

Chunga sana usizame kwenye huu mtego. Yani mimi nikishaanza kuona kitu kinafanana na mafanikio, ndio nakua kauzu, kama nilikua naamka saa 1 basi naanza kuamka saa 11 alfajiri.

3. Mikono izame kwenye tope - fukua 'nyungunyungu'.

Maisha hayana njia ya mkato - haijawahi kutokea. Ukitaka kumfukua nyungunyungu kwa kijiko basi jua umeshakwama. Wenzetu wazungu wanasema "Getting your hands dirty".

Mtu leo anamwangalia Juma wa Maxcom anavyogonga pesa kiulaini akiwa anaSip coffee pale ofisini kwake au Bruno wa smartcodes anavyoingiza mkwanja kiutani utani basi anadhani nae ataanza soon kugonga pesa kama hao. Kwa taarifa yako hiyo ni ndoto, hawa watu wamesota sana, wamechafuka mikono miaka na miaka, wamefukua nyungunyungu 'si wa nchi hii'. Hadi kufika hapo wamekwepa mishale mingi zaidi ya udhaniavyo.

Hakuna 'danga' atakayekutajirisha, hakuna cha mkekabet wala premier bet. Bong'oa, Zama chini toa vya uvunguni - sharti kukunja goti km kweli unania ya kusakata rhumba. Yani suala la kuhustle halina alternative.

4. Kupiga 'kakobe'.

Hapo nyuma kidogo enzi zangu za 'ubashite', nilicheza sana pool table, nimegonga sana watu 'woshi' (yani unazamisha kete zote kabla mwenzio hajaingiza hata 1), nilivyoona uwezo umekua mzuri nikaingia kwenye 'kila' (kamari ya pool table). Huko kwenye kila kuna kitu kinaitwa 'kupiga kakobe', yani unapiga kete zinaingia ovyo kwenye mashimo bila mpangilio, tena zinaeza ingia hata mipira mi4 kwa pamoja.

Mpaka mtu agonge kakobe ujue alikaza mkono haswa, akakomaa, akajikakamua, akabutua kete kwa nguvu sana, akachafua meza nzima, ndipo mipira inaanza kuzurura kutafuta mashimo. Watu wengi wanasema kubahatisha - mimi sioni km ni bahati. Mtu kajikunja, katumia nguvu zote, tena kapanga tokea kichwani kua anabutua kete zitafute shimo, hakuna bahati hapo.

Same in life, hakuna kubahatisha kwenye mafanikio. Wenzetu wanasema "The harder he works, the luckier he gets". Wewe ndugu yangu siku nzima umetegesha macho Shilawadu, jukwaa la mambo ya kikubwa, ukienda extra mile unaangukia kwa page ya Mange - tena bado unategemea bahati. Mtu ana GPA ya 2.1 ana karibu miezi 6 au hata mwaka anasaga lami kutafuta internship, siku kapata kazi, wewe na 3.4 yako anaanza kusema - dah jamaa ana kismati sana, chuo alikua kilaza lkn kapata ajira ya milioni.

Hata bahati inatafutwa. Get out and chase it.

5. Hifadhi mioyo yao - waachie akili zao.

Concept hii niipata kwenye movie 1 maarufu sana ya Denzel Washington (hapa The Boss atakua kanielewa), inaitwa 'Remember the Titans'.

Hii ni trick rahisi ya business management. Mimi vijana wangu wa kazi huko kwenye matrekta nilikua nakula nao chakula kimoja_sahani 1, tunaloa wote mvua, tunavyonza jua wote, tunalala chini ya miti pa1, tunakunywa maji ya tope pamoja, na uvunguni mwa trekta nazama. Ningeweza kua nanunua dasani, na kukodi pikipiki ya kunichukua na kurudisha guest house.

Lkn nilifanya yote haya ili kuwateka miono yao, kuwaPossess, kuwamiliki. Hii iliwafanya wajihisi they're part of me, and I'm part of them. Hata mtu awe nunda kiasi gani, ukimteka moyo hawezi kwenda against na kile mnachopanga - hawezi kuAfford kukudisappoint. Mwisho wa mchezo wewe ndio mshindi. Akili yake mwachie.

Kuna watu wanalima kilosa, lkn wanaishi Mbezi, kwanini vijana wasikunyooshe?! Umewaachia moyo na akili unategemea nini?!

6. Jimegee 'kakibangala' chako

Nilivyomaliza form 6 nilienda Jeshi_JKT - kazi za majeshi kugangamala, kazi za 'kibeto'. Nimenyoa sana vipara, foot drill, mabanzi ya utosini, si mchezo.

Kuna hiki kitu kinaitwa 'kukata kibangala', yani kwenye kundi la 'kombania' nzima afande akichukizwa anamega portion ndogo ya watu kwenye kombania, watu kama 30 kati ya 150 hivi, kisha mnapigwa 'tifu' la kibabe, yani ukitoka hapo huwezi tembea kwa miguu, bora utambae na tumbo. Nyie wengine mnaachiwa bila hata kuguswa, kamanda anajua fika atashindwa kuwamudu nyie wote 150, hivyo anawachukua wachache anawahenyesha kisawasawa - yani mnahemeshwa hadi unajihisi umepigwa 'nusu kaput'.

Biashara nayo iko hivyo hivyo upande wa ushindani/competition. Huwezi ukawa perfect kwenye kila kitu, yani uwe perfect jumla jumla ni ngumu sana. Jimegee kibangala chako kifanyie kazi haswa. Yani uwe vzr hakuna competitor atakayechokoma.

Tenga kitu ki1 tu ambacho utaweza kukimudu, kuwa super perfect kwenye hicho kitu, acha maswala ya kuwa general. Mimi niliamua kujijenga vzr suala la 'kumwaga unga - kulima mashamba kwa ustadi wa juu', nikashikilia hapo. Bei zangu zilikuwa juu sana, kulimiwa on time haikuwa guaranteed, hakuna mambo ya negotiations, ardhi napima kwa hatua zangu. Nilijua nisingemudu kutimiza vyote, nilitafuta ki1 tu afu nikawa 99% perfect kwenye hicho, sikujali competitions wangu wameshikilia nini. Mimi nilijali suala la 'kumwaga unga' tu. Yani nilijikatia hiko kibangala nikakisimamia ipasavyo.

Kwenye competition tafuta kuwa strong kwenye kitu fulani, na uwe strong kweli kweli. Ukitaka vyote utakosa vyote.

Angalia watu kama Clouds, hawajataka kuwa general ndio maana leo ni 1 kati radio station bora zaidi, wao waliamua kubase kwenye burudani tu. Wakawagonga wapinzani wao wote.

Salute
ONTARIO.

Uzi mrefu achana na ubashite wa kuquote.
Safi sana jamaa, nakukubali sana maana unahamasisha hata mtu huchoki kutiririka na uzi, ni bonge la elimu!
 
Here is where I belong... Hapa ndipo ninapopigiaga Pesa.. Kiteto ndio mitaa yangu... Nalima pia.. Jumatatu naenda kiteto kuvuna.. Tutafutane tupeane fursa mkuu.. I own tractors too japo sio zangu ni za baba yangu ila ndio napigia kazi. Tutafutane mkuu kama hutojali... Sitakupm maana umesema hutak PMs ila mm naomba yako... Pambana mkuu... I'm a University graduate too ila kazi zmekua ngetwa na ukibahatika mshahara wa hovyo sana...
Mkuu
 
Mkuu njoo pm
 
Naomba kuuliza ni Traktor gani zuri kwa kulimia,kuanzia Horse Power(HP),jina la traktor na uhimilili wake kikazi...
 
Asante ndugu Ontario. Nimemega kitu hapa. Nitarudi na mrejeshi. Big up. Stay blessed.
 
Nimekulia kwenye kilimo, lakini niko hivi,

Aisee haiwezekani, nami nanunua mabawa nimfukuzie ONTARIO kama mwewe anavyofukuzia vifaranga vya kuku.

Salute sana boss
 
Bro ONTARIO tuko the same age lakini umeshaniacha kimafanikio.....

Daah! Sio fair kabisa...

Ila hakuna namna itabidi nijifunze kupitia kwako.

Hongera sana Serjeff Dennis, najiuliza imewezekana vip kwa mazingira yetu ya kibongo!!

Kwa kweli nadhibitisha kwa kusema Mungu ameweka kitu ndani yako. Appreciate bro!

Bado naendelea kujifunza Forex Trading.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daahhh!

Hii dose ni balaa, imepenya hadi kwenye mifupa.

Ahsante sana Mkuu ONTARIO
 
Kuna wakati hadi najiona mpuuzi yaani! Eti JF nimeingia zamani sana (sijui 2011)halafu madini kama haya ndo nayashtukia karne hii ya August 2017!?! Huu si upuuzi kweli!?! Eti jamani, yaani kila siku nakesha na siasa tu!?!

Poor me! Asante dogo ontario, tangu wiki mbili zilizopita nimeanza kupekua uzi wako mmoja baada ya mwingine na nimeahidi akili na utashi wangu kwamba nikitoka bure bila kufanyia kazi, Sina sababu ya kuendelea kuwa member wa JF!

Thanks much, ngoja niendelee kukusoma kimya kimya uzuri nimeshajithibitishai kuwa uyasemayo yote yana usahihi wa 100 %maana nimeona baadhi ya kazi zako hope ni Dw - YouTube!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAJINGA NDIO WALIWAO

ENDELEA KUWATAPELI MAANA KILA SIKU WATU HAWAJIFUNZI

NIMEPENDA NJIA YAKO YA KUTAPELI , UMEJITOFAUTISHA SANA NA MATAPELI WENGI WA HUMU
Unajifanya unajua kuanalyze kumbe we kapuku tu, watu wako serious na maisha bana, akutapeli wewe una kipi sasa cha kutapeliwa? labda akutapeli tigo yako ndo kitu unachomiliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta pesa mkuu, usiweke chuki kwa wengine wanaotafuta. Huu uzi una views 52000+, sema ni nani nimemtapeli - taja mtu mmoja tu. Nimepokea PM zaidi ya 200, sijajibu hata 1 - sio kwamba sizioni.

I'm not a big fan of mediocres, boss bora kuuliza kitu kuliko kujifanya unajua kila kitu. Ndio Nimemaliza chuo, UDSM mwaka 2016, course ya Gesi na mafuta (Petroleum Chemistry). Kwa kua wewe ni kilaza huwezi kutofautisha Pet. Chem na Pet. Eng.

Jeshi nimeenda 2013 JKT Kanembwa - KJ 824, intake ya kwanza 'operation miaka 50 ya JKT'.

Boss! Sikusoma CoET, na hata ningesoma CoET bado nisingedisco kwa vyovyote vile. My level of intelligence is untouchable, sio kwa kujisifu, but kwa hali niliyopitia chuo kama ingekua ni kilaza kama wewe, ungedisco semester ya 1.

Boss mimi hua naamini kua, kila binadamu aliumbwa na kiwango fulani cha upvmbavu, lkn kuna wengine wanajivunia huo upvmbavu hadi kuamua kuuonesha mbele za watu. You must not misuse your stupidity bruh.

Work hard, pray often, slay forever.
Mkuu achana na Huyo ana hisia za kike aende zake akaimbe mipasho na kina mama nasma, huku atuache wajasiriamali wenye kiu ya maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa napenda sana kusikia motivated story kama hizi, kutoka kwa motivated people kama huyu Ontario. Thanks bro, wewe umeshathubutu umeweza, bado ngoma ipo kwetu kutekeleza yale uliyosema, maana tatizo la Wabongo wengi lipo kwenye utekelezaji tu. Kiufupi nimekuelewa sana chief kwa jinsi ulivyotuonyesha sayansi ya kusaka mafanikio. Nitaku-Pm coz nakaproject nategemea kukafanya.
 
Mkuu kuna huu msimu wa mwezi wa 6-8 kule kilombero kwenye uvunaji wa mpunga. Unafunga teller unasomba mizigo kutoka kule mashambani kuleta town kwenye magodown na mashine za kukoboa.

Ule ndio msimu wa pesa, achana na huu wa kulima. Nausubiria vby mno hapa.
Vp broo ...miezi hyo njia hua zinapitik kwa gari kama fuso uko?
 
Back
Top Bottom