Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa mzee Natepe kushika Uwaziri wa Mambo ya ndani ya nchi.

Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka Waziri aliyemtangulia kutoka katika nyumba ya Waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama Waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana Waziri aliyeondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka na Natepe kutoka.

Ikampasa Mzee Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya Serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya Serekali kweli mzee Mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee mwinyi akateuliwa kuwa Rais Zanzibar. Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia Mzee Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea Mzee Mwinyi.

Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la Mawaziri akamteua tena Natepe kuwa Waziri palepale Mambo ya Ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja Mzee Mwinyi yupo Ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie?

Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe Mzee Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.
 
Uongo tu. Hakuna ukweli. Mwinyi alijiuzuru 1977 na aliyembadili ni Hassan Moyo.

Mwinyi alipelekwa kuwa Balozi. Sio kweli kwamba hakuwa na kazi.

Hassan Moyo Ali kuwa waziri mambo ya ndani muda mfupi.

Mwinyi alirudi kuwa waziri 1983

Stories za vijiweni
Ahsante kwa inputs zako
 
Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka zanzibar anaitwa mzee natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Natepe alipoingia tu officen alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri alieondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.

Ikampasa mzee mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee mwinyi akateuliwa kuwa Rais zanzibar Natepe wakati ana jifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee mwinyi.

Mzee mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa natepe mzee mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

Kwa viongozi wa sasa hilo ni nadra sana kutokea. Wamekuwa watuwa kulipiza visasi sana.
 
MAFISADI PAPA ni MTUPOLI/LIJIZI na kundi lake/MIJIZI linalo MUABUDU na KUMSUJUDIA la wazalendo Feki, walikua wanapatikana pande zipi ”nyakati” hizo?! nauliza tu. ..
Wametupora Tanganyika yetu, wanatuteka, kuua, kututesa na kutupiga risasi, wanajifanya wanauchungu nayo saaaana.
 
Uongo tu. Hakuna ukweli. Mwinyi alijiuzuru 1977 na aliyembadili ni Hassan Moyo.

Mwinyi alipelekwa kuwa Balozi. Sio kweli kwamba hakuwa na kazi.

Hassan Moyo Ali kuwa waziri mambo ya ndani muda mfupi.

Mwinyi alirudi kuwa waziri 1983

Stories za vijiweni
Ni kweli aliyempokea ni mzee Hassan Nassor moyo.

Ni kweli mzee mwinyi alikwenda kuwa balozi nchini misri baada ya kujiuzulu uwaziri.
 
Back
Top Bottom