JINSI MWANGA KUTOKA KWENYE SIMU, KOMPYUTA NA TV UNAVYOWEZA KUPELEKEA UPOFU KATIKA MACHO YETU

James88

JF-Expert Member
May 14, 2017
1,700
1,754
Habari Wanajukwaa

Siku ya leo asubuhi katika pitapita zangu youtube nikakutana na video moja kutoka kwenye channel inaitwa Unbox therapy( Kwa wale ambao mtakuwa mnafatilia unboxing za simu mpya basi ni lazima utakuwa unamfahamu huyu jamaa).

Hiyo video ilikiwa na title ambayo imeandikwa hivi, " Your smartphone is blinding you, here is what to do" nmeiangalia ile video yote halafu nikashtuka, kilichonishtua ni kwamba mimi shughuli zangu za kila siku zinanifanya nikae kwenye laptop na simu yangu kwa muda mrefu kwa siku.

Vitu alivyovielezea mle ndani kwenye ile video ni kwamba Mwanga wa blue kutoka katika smartphones, tablet na computer unaweza kisababisha upofu na hiyo ni kutokana na utafiti ambao ulifanywa na chuo kimoja nchini Marekani na hiyo makala iliandikwa katika page ya USA TODAY.

Nililazimika kwenda kuitafuta hiyo makala katika hiyo page ya USA TODAY ili nione wanalizungumziaje hilo swala na ndipo nilipokutana na hiyo makala. Hiyo makala inaeleza hivi,

"Kwa kifupi ni kwamba mwanga wa blue huwa unafanya reactions za kikemikali na molecules za retina na kama unavojua kwamba retina ndiyo inayotuwezesha kuona. Hii retina huwa inatumia photoreceiptors, kwa hiyo sumu inayozalishwa kutokana na reaction ya molecule za retina na huo mwanga wa blue hupelekea kufa kwa hizo photoreceiptors na once zikifa haziwezi kuzailishwa zingine.

Na hiyo Huenda ikasababisha ugonjwa wa macho usiotibika ambao utapelekea upofu mtu atakapofikia umri wa miaka ya 50s au 60s, Watafiti hao walisema.

Watafiti wanajifunza jinsi mwanga wa blue kutoka kwa TV, smartphones na tablet ili kujua nini athari zake kwa watu ambao wako exposed kwenye vitu hivyo kila siku. Wanashauri watu kuvaa miwani ya jua kuchuja UV na mwanga wa bluu, na kuepuka kutumia vifaa vyao vya digital katika giza.

Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni kama Apple, Amazon na Google imeanzisha filters za mwanga wa bluu ili kupunguza uwezekano wa watumiaji. Kwa mfano, IOS na MacOS ina kitu kinaitwa Night Shift ambapo watumiaji wanaweza kurekebisha jinsi vile screen zao zinavoonesha na hivyo kupelekea kutowaumiza macho.

Mwanga wa blue pia unaweza kuathiri usingizi wako. Wanashauri kukaa mbali na vifaa angalau dakika 30 kabla ya kulala"

Hivyo basi kutokana na hiyo makala kitu ambacho unaweza kufanya kwa wale ambao wana devices ambazo unaweza kucalibrate settings za mwanga wanaweza wakaset devices zao kwenda kwenye hizo settings.

Mfano Iphone wana hiyo night shift, pia huawei wana eye confort(huawei za kuanzia mwaka 2016), pia katika laptop yako unaweza kukalibrate settings hizo kwenye display settings(setting yake inaitwa calibrate colour), bado nafatilia kwenye TV unakalibrate vipi.

Kwa simu zingine sijajua kama kuna hizo settings, lakini nina uhakika kwamba simu nyingi za bei rahisi hazina hizo settings. Na hapo ndipo yanapokuja madhara ya watu kupenda quantity kuliko quality.

Vitu ambavyo watu huwa wanaviangalia katika kununua hizi simu huwa mara nyingi havina mantiki na wanaacha vitu vidogodogo sana ambavyo ndio vya muhimu.

Nawasilisha.
Screenshot_20180818-072136.jpg
 
Tecno inachujio automatic kazi kwenu, na wanetu wanaotumia smartphone hawa tangu age 5 bila shaka wote watakuwa vipofu kufikia miaka yao ya 45-50
 
Bahati mbaya mm nimeshaanza kuathirika na hili tatizo ktk maa24 ya siku mm karibu masaa18-macho yangu yapo ktk mwanga wa hizo device ,na tayali sshvi nikiangalia mwanga kwa nusu saa tu macho yangu kwa juu kuelekea kichwani pamoja na kichwa huwa vinaniuma sana hdi nitoke kwenye mwanga sasa naomba ushauri ili kurudi ktk hali yangu ya kawaida na kuepuka upofu siku chache zijazo ,pia asante kwa elimu hii ndio faida social network
 
Tumia App iitwayo Night Screen(kutoka Google play store),inasaidia kupunguza mwanga.

Picha ya iyo App ni hii
IMG_20180818_083353.JPG
 
Logically inamaanisha nchi zilizoendelea zina vipofu wengi sasa hivi au kuna mwaka utafika watazalishwa vipofu wengi.

Simply kwa sababu tekonolojia zimeanzia kwao ama sivyo?

Kwenye usa today wamekadiria idadi ya vipofu? Au wamekadiria mwaka ambao vipofu watakua wengi?
 
Huu utafiti unaweza kuta umefadhiliwa na kampuni pinzani za Simu ili kuua ushindani.
 
Logically inamaanisha nchi zilizoendelea zina vipofu wengi sasa hivi au kuna mwaka utafika watazalishwa vipofu wengi.

Simply kwa sababu tekonolojia zimeanzia kwao ama sivyo?

Kwenye usa today wamekadiria idadi ya vipofu? Au wamekadiria mwaka ambao vipofu watakua wengi?
wamezungumza kwamba watu wengi watakapofikia umri wa miaka 50s au 60s... huenda wakabiliwa na upofu kutokana na exposure ya blue light....
 
wamezungumza kwamba watu wengi watakapofikia umri wa miaka 50s au 60s... huenda wakabiliwa na upofu kutokana na exposure ya blue light....
Watu wengi kutokea eneo gani? Europe, China, Africa, Australia, Africa?
 
Tecno inachujio automatic kazi kwenu, na wanetu wanaotumia smartphone hawa tangu age 5 bila shaka wote watakuwa vipofu kufikia miaka yao ya 45-50
Hata mm tecno yangu inajicalbrate yenyewe japo kuna muda inakera unastukia mwanga unapungua, tu ila inasaidia, natumia tecnol9
IMG_20180818_101027_834.jpg
 
Bahati mbaya mm nimeshaanza kuathirika na hili tatizo ktk maa24 ya siku mm karibu masaa18-macho yangu yapo ktk mwanga wa hizo device ,na tayali sshvi nikiangalia mwanga kwa nusu saa tu macho yangu kwa juu kuelekea kichwani pamoja na kichwa huwa vinaniuma sana hdi nitoke kwenye mwanga sasa naomba ushauri ili kurudi ktk hali yangu ya kawaida na kuepuka upofu siku chache zijazo ,pia asante kwa elimu hii ndio faida social network
Mm pia nishaanza kuathirika coz na professional yangu, maumivu ua shingo na mgongo pia. Maana muda wote wa kazini nimeangalia computer
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom